Chato: Msanii wa nyimbo za asili aliyemtumkana Rais Samia ahukumiwa miaka 6 jela

Vipi angemtukana mzazi wako ungesema kaonewa,hivi kila mtu asimame tu atoe wimbo kutukana tutakuwa na jamii gani.
Haki za binadam isiwe kichaka Cha kuumiza hisia za wengine
 
Anastaili hiyo adhabu kwa sababu analeta ukabila.
Kuna siku gani bei ya mafuta ilikuwa shs 100 au bei ya sabuni ilikuwa shs 200?
 
Halafu ukiona kijana anaendekeza kuongea kikabila uhue huyo ushamba haujamwisha na kachelewa kufika mjini.
 
Vipi angemtukana mzazi wako ungesema kaonewa,hivi kila mtu asimame tu atoe wimbo kutukana tutakuwa na jamii gani.
Haki za binadam isiwe kichaka Cha kuumiza hisia za wengine
Tusi lipo wapi hapo?
 
Mkuu kwa public interest, ni wapi unachora mstari kati ya uhuru wa msanii na kuvunja sheria kwa kutukana/kudhalilisha mtu mwingine?

Mimi nadhani kama ni msanii angeweka hata tafsida au "fumbo" kama Roma tu yaani inafanya ridicule au satire ila bila kumtaja mtu Moja kwa Moja. Sasa kumuita mtu directly kwamba Msanii ana mapunye kichwani". Sidhani kama ni usanii Bali ni matusi yaliyojificha kwenye nyimbo.
 
Kwaiyo anataka awe ananunua mafuta ya kula kwa sh 100..?😁😁
 
Kiukweli nimetafuta tusi hapo sijaliona mpaka leo tangu uzi ulipopandishwa.
 
Kwa mtu anayejitambua,kama raisi anaimbiwa huu wimbo,wazazi wake na majirani wana hali gani?
 
Walimwonea tu. Mbona ney wa mitego hajafungwa
 
Huyu mwamba bado yupo jela hadi leo?
 
Hivi adhabu ya viboko corporal punishment ilifutwa??!! Wangemuongezea na viboko 40 hivi 30 akiingia jela 10 akitoka akamuonyeshe mkewe
 
Mpeleke huyo Dawa Ufaransa kwa Macron ili akampige kofi na afungwe kifungo kifupi
 
Matusi siku hizi yamebadilika nini, yamekuwa mapya eeh...nimesikiliza hadi mwisho sijasikia tusi hata moja angalau kwa yale tuliyoyazoea toka utotoni.
Hebu andika matusi hapa unayoyajuwa wewe!!
 
Hii nyimbo mbona kali sana ilitakiwa iwe trending song u tube
 
Naruhusiwa kuweka ringtone hii,
Ila nikipita pale lugalo, ama navy pale lazima simu niitoe sauti. 😂🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…