Chato: Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, atembelea kaburi la Hayati Magufuli

Chato: Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, atembelea kaburi la Hayati Magufuli

Nadhani hapa ndipo palipo na siri kubwa inayowahusu waTanzania kwa ujumla wao.

Tungekuwa na jukwaa hasa la GTs, hii ingekuwa ndiyo mada motomoto sana kujaribu kutafuta jibu la hizi tofauti tunazoziona waziwazi wakizionyesha waTanzania kwa viongozi hawa.

Mimi nitakwenda mbele zaidi, na kusema kuwa ukipata jibu sahihi linalowatofautisha Mkapa na Magufuli, jibu hilo hilo linaweza kuwa ni sahihi pia kwa chama kama CHADEMA kutoweza kuwashawishi waTanzania hadi sasa, ili waiondoe CCM madarakani.
WaTanzania wanaendelea kuing'ang'ania CCM, pamoja na madhaifu yake mengi, kuliko kuwaamini CHADEMA!

Magufuli alikuwa na makandokando mengi, lakini inaonekana kundi kubwa linayaweka pembeni, kwa sababu zilizomtofautisha yeye na wenzake, akina Mkapa na Kikwete na hata Mzee Ruksa.
Kiufupi ndugu Kalamu ni kwamba "ujinga" ndio adui mkubwa.
 
Nimekuelewa sana Kalamu,
Lakini kwa jinsi ninavyokuheshimu kwa michango yako humu, utakuwa hujatufanyia jambo jema kama wewe binafsi utshindwa kuanzisha hii hoja,

Nadhani ni jambo muhimu sana, kuna vitu ambacho Watanzania wa kawaida wanavihitaji kutoka kwa mtu kama Magufuli, hata uwaambie nini hawatakuelewa,

Labda huwa kuna viongozi ambao ni katana Mwenyezi Mungu, na wengine huwa ni viongozi wa kulazimisha na ujanja ujanja tu, the same kama CHADEMA,

Nikivyomwona Kardinali Pengo hapo, ndio hapo vilevile I nakuja hoja yako hapo, kwamba uongozi ni karama, maana hata mtoto anamfahamu Pengo, pamoja na kwamba kastaafu ni muda sasa, kuliko huyu wa leo
Nimekusoma kwa makini na uangalifu mkubwa sana mkuu'Mwitore'.
Niwe mkweli, nimekusoma zaidi ya mara moja kutokana na mtindo wa uandishi wako unaoonekana kuficha halisi ya maana ya unachokusudia kuwasilisha.
Angalau nilielewa hivyo, kama siyo upungufu tu wa kawaida kutokana na staili ya uandishi wenyewe.

Kwa mfano, maana hasa ya uwepo wa Pengo unahusiana vipi na nilichoandika na wewe ukakinukuu hapo?
Sikutaja mahali popote uwepo wa Pengo na aina ya uongozi unaoashiria kuwakoga waTanzania.

Na hata huyo Magufuli mwenyewe, siamini kuwa waTanzania wengi walipenda matendo yote aliyoyafanya akiwa kiongozi, lakini inaelekea yale waliyoyapenda yaliwavuta zaidi kwake, na pengine kutojali mabovu aliyotenda.

Kwa hiyo, kama ni ujumbe ulitaka kunifikishia, nasikitika kwamba njia ya uwasilishi uliyotumia haikunipa nafasi ya kuupokea vizuri ujumbe huo.
 
Kiufupi ndugu Kalamu ni kwamba "ujinga" ndio adui mkubwa.
Unasema kweli?

Ni mara nyingi sana hata mimi nimekuwa mmoja wa hao wanaoamini kama wewe, kwamba waTanzania tunasumbuliwa na "ujinga", ndiyo maana tunakuwa wavumilivu wa mambo mengi ya hovyo wanayofanya CCM.

Lakini ukiangalia kwa makini, na kuacha mivuto ya kimakundi inayotupofusha akili mara nyingi, utaona kwamba kuna 'pattern' isiyoyumba waliyonayo waTanzania wengi kwa viongozi wa nchi yetu.
Kushindwa kwetu kuelewa 'pattern' hiyo ndiko kunakotufanya tukimbilie haya ya "ujinga"
 
Hiyo ni ishara ya kukumbuka mema ya Hayati JPM aliyolitendea taifa hili na Kanisa kwa ujumla. Mwenyezi Mungu amlaze pema peponi. Amini.
 
Back
Top Bottom