Chato: Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, atembelea kaburi la Hayati Magufuli

Kiufupi ndugu Kalamu ni kwamba "ujinga" ndio adui mkubwa.
 
Nimekusoma kwa makini na uangalifu mkubwa sana mkuu'Mwitore'.
Niwe mkweli, nimekusoma zaidi ya mara moja kutokana na mtindo wa uandishi wako unaoonekana kuficha halisi ya maana ya unachokusudia kuwasilisha.
Angalau nilielewa hivyo, kama siyo upungufu tu wa kawaida kutokana na staili ya uandishi wenyewe.

Kwa mfano, maana hasa ya uwepo wa Pengo unahusiana vipi na nilichoandika na wewe ukakinukuu hapo?
Sikutaja mahali popote uwepo wa Pengo na aina ya uongozi unaoashiria kuwakoga waTanzania.

Na hata huyo Magufuli mwenyewe, siamini kuwa waTanzania wengi walipenda matendo yote aliyoyafanya akiwa kiongozi, lakini inaelekea yale waliyoyapenda yaliwavuta zaidi kwake, na pengine kutojali mabovu aliyotenda.

Kwa hiyo, kama ni ujumbe ulitaka kunifikishia, nasikitika kwamba njia ya uwasilishi uliyotumia haikunipa nafasi ya kuupokea vizuri ujumbe huo.
 
Kiufupi ndugu Kalamu ni kwamba "ujinga" ndio adui mkubwa.
Unasema kweli?

Ni mara nyingi sana hata mimi nimekuwa mmoja wa hao wanaoamini kama wewe, kwamba waTanzania tunasumbuliwa na "ujinga", ndiyo maana tunakuwa wavumilivu wa mambo mengi ya hovyo wanayofanya CCM.

Lakini ukiangalia kwa makini, na kuacha mivuto ya kimakundi inayotupofusha akili mara nyingi, utaona kwamba kuna 'pattern' isiyoyumba waliyonayo waTanzania wengi kwa viongozi wa nchi yetu.
Kushindwa kwetu kuelewa 'pattern' hiyo ndiko kunakotufanya tukimbilie haya ya "ujinga"
 
Hiyo ni ishara ya kukumbuka mema ya Hayati JPM aliyolitendea taifa hili na Kanisa kwa ujumla. Mwenyezi Mungu amlaze pema peponi. Amini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…