Chato: Rais Samia kuongoza kumbukizi mwaka mmoja kifo cha Magufuli

Chato: Rais Samia kuongoza kumbukizi mwaka mmoja kifo cha Magufuli

Mnazubaa tu anatukwa na ndio aliyemuinua huyo wanaemsujudia mnaacha Mkapa anadharaulika Yani jina kubwa like mmezubaa tu. Mnakubaliana na hii double standard wakati Mkapa ndio hata alisema apewe urais huyo????

Mnazubaa mno hata mkiamua kunishambulia huu ukweli hamuwezi kuukataa, wake up.
 
Rais Samia Suluhu kuongoza kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha hayati Magufuli itakayofanyika kwenye uwanja vya Magufuli uliopo Chato, March 17 mwaka huu.

Naona ndugu kmbwembwe sasa atashiriki mwaka mmoja wa Samia..

========

Geita. Rais Samia Suluhu Hassan atashiriki na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Geita katika hafla ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli itakayofanyika Machi 17, 2022 katika Uwanja wa Magufuli uliopo mjini Chato.

Baadhi ya viongozi watakaoshiriki hafla hiyo ni makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi pamoja na viongozi mbalimbali wa nchi.

Hayo yameelezwa leo Jumapili Machi 13, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyemule wakati akiwasalimia waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Upendo mjini hapa na kuwataka wajitokeze kushiriki hafla hiyo.

Senyamule amesema Serikali kwa kushirikiana na familia ya hayati Magufuli wamekusudia kufanya kumbukumbu ya mwaka mmoja ikiwa ni njia ya kumkumbuka kiongozi huyo.

Rais Magufuli alifariki dunia Machi 17 mwaka 2021 katika Hospitali ya Mzena iliyopo jijini Dar es salaam baada ya kuugua maradhi ya moyo.

Mwananchi
Ingekuwa mapumziko basi, lakini afadhali Chato International Airport (CIA) itatumika
 
Mkapa mnamuenzi vipi achimwene?
Rais wa nchi anaenziwa kitaifa, siyo kikabila au kikanda. Unataka kila kabila wawe wanaenzi watu wao?
Ungekuwa na point nzuri kama ungeshauri marais wote waliofariki waenziwe kitaifa na kwa utaratibu maalumu; lakini siyo kusema watu wa kusini tumekaa kifala. Huwezi kuwatukana kundi la watu kwa jambo ambalo liko nje ya uwezo wao bwashee!
 
Wakati wananchi wanaumia na mfumuko wa bei, Viongozi hawaathiriki na huo mfumuko kwani wamejiwekea utaratibu wa kufanya sherehe na kujilipa posho kila kukicha!
Hakukua na haja ya sherehe ya kumkumbuka dikteta ni upotevu wa rasilimali.
 
Hahaha nadhan hata msemeje lakini huyu bwana JPM alishaingia mioyoni mwa wananchi over 80%..kwa hiyo mnapoamua kumdhihaki muwe makini sana...mama Samia Rais wetu alisema viatu vya JPM havimtoshi..alikiri Rais wetu..ni ukweli ...na muungwana sana..Rais wetu ametokea kwa JPM..means bila JPM tusingekuwa na mama Samia..hivi unadhan ataachaje kushiriki kikamilifu shughuli ya kumbukumbu....nyie kaeni mchambanee lakini mjue JPM na Samia walikuwa kitu kimoja.....na ndio maana aliendelea nae hata awamu ya pili kidogo..nyie wengine mnaotafuta fursa za kupiga hela eti kwa mgongo wa Rais,. Mmechina..hamtafanikiwa..msidhan Rais hajui kinachofanyika..kama Hamna kazi nendeni hata mkalime mashamba yapo tele kule
Unafikiri mimi ni chawa wa kusifia huto mama yenu nipate posho?

Sioni umuhimu wa kupoteza pesa kwa dhifa zisizohitaji matumizi makubwa hivyo huo ni upotevu wa pesa.

Halafu hiyo 80% ya watanzania unawazungumzia wastaafu walionyimwa mafao yao, wafanyabiashara waliopewa kesi bandia za uhujumu uchumi, unazungumzia wizi wa kura kwa kuzima mitandao ya kijamii siku 6, unazungumzia watu waliofukuzwa kazi bila taratibu kufuatwa?

Unazungumzia watumishi wa umma walionyimwa nyongeza ya mshahara miaka 6 ilhali ni haki yao ya msingi, jumlisha wote hao na waliosahaulika ukumbuke wana chain ya familia na wategemezi.
 
Unafiki ndio adui mkubwa wa Taifa la Tanzania, hususan wanasiasa ambao wamewaambukiza wanataaluma sasa
 
Hahahahaha

Taifa letu huenda linaongoza kwa Unafiki Duniani kwa sasa

Namsoma Lemutuz muda huu anamuasa Makonda kutulia kwa kuwa sasa hivi analipia gharama za udhalimu wake wakati enzi zile ilikuwa haipiti siku hajaandika Le commandant Field Mashal sijui kanyaga twende tumechelewa sana na fyoko fyoko zingine kibao…walio madarakani wana cha kujifunza
Dementia ni maradhi yanayowapata over 60’s, usishangae sana.
 
Back
Top Bottom