Chato yatangazwa kuwa kitovu cha Utalii Kanda ya Ziwa

Chato yatangazwa kuwa kitovu cha Utalii Kanda ya Ziwa

Kwanini isiwe wilaya ya Serengeti, Bariadi au Musoma.
Wanasumbuliwa na ugonjwa wao wa kibaguzi tu, hakuna lolote la maana Chato. Historia itamuhukumu Magufuli.

Watakao jaaliwa uhai watayaona MAGOFU ya Magufuli Chato.
 
Waziri wa Utalii na Maliasili, Dkt. Damas Ndumbaro akiwa ziarani Mkoani Geita ametangaza rasmi kuwa Chato ndio kitovu cha Utalii Kanda ya Ziwa....
Magereza ya kisasa na mochwari ya kisasa
 
eti chato kuna vivutio vingi vya utalii ikiwepo utalii wa maji na utalii wa mashamba ya miti pia Chato kuna amani na utulivu sana kitu ambacho kinawavutia sana watalii [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
Sasa kilichokuchekesha ni nini kama siyo umbea?
 
Hata mbuyu ulianza kama uyoga!!

Serengeti, Ngorongoro, mikumi na manyara hivi zilianzaje mkuu?
Unategemea kuna siku Burigi itakuwa kama Serengeti?

Serengeti, Ngorongoro na Mikumi sio za kutengenezwa kama Burigi, mbuga zake ni za asili uoto wake ni wa asili sio wa kupanda, wanyama wake ni wa asili sio wa kusombwa kwenye fuso.
 
Kwa yanayoendelea chato ili Magufuli aeleweke anapaswa kupeleka miradi mikubwa pia kwa watangulizi wake tofauti na hapo dhana ya upendeleo itapata nguvu na kuwapa cha kusema wenye nia ovu.
Kusema tu hakumzuii mtu kifanya yake mzee bora mpeleke wazi kuwa kuanzia sasa kila urais uwe wa mzunguko kutoka kila mkoa kwa awamu moja atakayeshindwa kuendeleza mkoa wake basi.

Kila mtu atakula alichopanda waliopita wanakula walichopanda na walishabugi aisee.
 
Dr Ndumbaro, tangazo la kufanya Chato kituo cha utalii liendane na kujenga ofisi kubwa hapo ya Kanda ya ziwa ya TTB/TANAPA kutangaza utalii. Hapo utakuwa umeweka uendelevu wa kivutio hicho. Hili ni muhimu mno.
 
Kamanda hapo anamsikilizaza mheshimiwa, huku moyoni akiguna duuuh, jamani Chato hii!

1610528063779.png
 
Back
Top Bottom