PreGE2025 CHAUMMA: Suala Siyo wingi wa watu bali wana hoja gani?

PreGE2025 CHAUMMA: Suala Siyo wingi wa watu bali wana hoja gani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kuna watu wanaiangalia CHAUMMA kwa jicho la mikutano yao kujaza ama kutokujaza watu. Na bahati mbaya na CHAUMMA nao wameingia kwenye mtego huo.

Nadhani chama cha siasa hakitambuliki kwa wingi wa watu wanaohudhuria mikutano yake, bali kwa hoja za chama husika kama zina manufaa kwa wanaohudhuria mikutano yao.

Jee hoja za CHAUMMA ya Sasa zina mashiko kwa watanzania na watoa hoja hizo wana maadili ya yasiyotiliwa shaka ili hoja zao ziaminike kwa watanzania?
Acha kupindisha ukweli... Kipimo sahihi cha mikutano ya chama chochote ni idadi ya watu waliohudhuria, sio kwamba kila aliyehudhulia anakiunga mkono chama hko, hapana ila ujumbe unakuwa umefika.
 
Mtaji mkubwa wa chama ni hoja (sera) - siyo watu!

Chama kikishakuwa na sera, hakiwezi kukosa watu.

Ukiona chama kinakosa watu, au kinalazimisha watu wakipende, ujue sera zake zimeshachakaa - hazikubaliki kwa umma.
Kajaribu kugombea hata udiwani na sera zako bila kuwa na kundi la watu....ndo utajua hujui
 
CHAUMA hoja yao ni Ubwabwa,sasa sijui wewe kenge unataka kuwabadilishia hoja?
Sera ya Ubwabwa ni sera kubwa sana kwa nchi hii.

Hii sera ilikaribia kuteka fikra za watanzania serikali ikapiga marufuku uwepo wa ubwabwa kwenye kampeni wakidai ni Rushwa, wakati ambapo viongozi tofauti wa CCM wameshawahi kuonekana wakishiriki kupika ubwabwa kwenye kampeni zao.
 
Kajaribu kugombea hata udiwani na sera zako bila kuwa na kundi la watu....ndo utajua hujui
Kwani watu hao unaozungumza nao unakuwa umezaliwa nao?

Kabla ya kuwapata, nini kinachowavuta waje kwako kama siyo sera, msimamo, mahusiano, ubia, ushirikiano, misingi?

Mpaka mtu anakuwa na kundi la watu nyuma yake, linalomwamini, hapo lazima sera zake zinajulikana kwao.
 
Na ndiyo maana, wale jamaa huwa WANASOMBA WATU, hata kwa malori!
Umeona ee
Kwani watu hao unaozungumza nao unakuwa umezaliwa nao?

Kabla ya kuwapata, nini kinachowavuta waje kwako kama siyo sera, msimamo, mahusiano, ubia, ushirikiano, misingi?

Mpaka mtu anakuwa na kundi la watu nyuma yake, linalomwamini, hapo lazima sera zake zinajulikana kwao.
Haya baba kajaribu kugombea utajionea mwenyewe,africa siasa ni watu sera peleka ulaya
 
Ndo maana wa akina msukuma hawana sera lakini Ana watu,so ubunge anaupata kiurahisi
 
Kuna watu wanaiangalia CHAUMMA kwa jicho la mikutano yao kujaza ama kutokujaza watu. Na bahati mbaya na CHAUMMA nao wameingia kwenye mtego huo.

Nadhani chama cha siasa hakitambuliki kwa wingi wa watu wanaohudhuria mikutano yake, bali kwa hoja za chama husika kama zina manufaa kwa wanaohudhuria mikutano yao.

Jee hoja za CHAUMMA ya Sasa zina mashiko kwa watanzania na watoa hoja hizo wana maadili ya yasiyotiliwa shaka ili hoja zao ziaminike kwa watanzania?
Hoja ya Chaumma ni ubwabwa, je katika wapya wote waliojiunga nacho kuna aliyezungumzia lishe kwa Watanzania? Ajabu wote wamezungumzia vyeo na namna wanavyojipanga kutafuta vyeo vingine katika Uchaguzi Mkuu ujao!
 
Kuna watu wanaiangalia CHAUMMA kwa jicho la mikutano yao kujaza ama kutokujaza watu. Na bahati mbaya na CHAUMMA nao wameingia kwenye mtego huo.

Nadhani chama cha siasa hakitambuliki kwa wingi wa watu wanaohudhuria mikutano yake, bali kwa hoja za chama husika kama zina manufaa kwa wanaohudhuria mikutano yao.

Jee hoja za CHAUMMA ya Sasa zina mashiko kwa watanzania na watoa hoja hizo wana maadili ya yasiyotiliwa shaka ili hoja zao ziaminike kwa watanzania?
Hoja yao kubwa ni kuipasua CHADEMA baada ya kula hela kutoka CCM na mama Abdul.
Ikajikuta CHADEMA haipasuki hovyo; Mfano hata baada ya kuondoka Dr. Slaa mtu ambaye alikuwa maarufu ndani ya chama kuliko hata chama chenyewe ndio kwanza chama kikazidi kuimarika. Sembuse huyu Mrema wa Bonyokwa ambaye hata akihojiwa na media aeleze nini maana ya "No reforms no election" kwa kiswahili hajui
 
Mtaji mkubwa wa chama ni hoja (sera) kwanza - siyo watu!

Chama kikishakuwa na sera kabambe, hakiwezi kukosa watu.

Ndiyo maana wanaoanzisha chama siyo umma wa watu bali mtu au kikundi fulani cha watu wachache - ndipo watu wengine hujumuika kulingana na sera husika.

Ukiona chama kinakosa watu, au kinalazimisha watu wakipende, ujue sera zake zimeshachakaa - hazikubaliki kwa umma.
Hata mimi nina sera za maana sana ila sina uungwaji mkono,

Usipuuze nguvu ya uungwaji mkono.
 
Hata mimi nina sera za maana sana ila sina uungwaji mkono,

Usipuuze nguvu ya uungwaji mkono.
Ukiwa na sera nzuri bila uungwaji mkono, jilaumu wewe mwenyewe kwa kushindwa kuziwasilisha kwa umma.

Huna tofauti na mfanyabiashara asiyetaka kutumia gharama za matangazo wakati ana bidhaa za mamilioni stoo.

Unadhani wateja watanusu kwamba una bidhaa ulizozifungua ndani?

Biashara ni matangazo!

Kama bidhaa (sera) zako ni nzuri na ukajua mbinu bora za kuzitangaza kwa watu, lazima wakuunge mkono tu.

Ukiona huungwi mkono licha ya juhudi hizo, bila shaka hizo sera ni mbaya mbovu!
 
Sababu vyama vimeshakuwa ni Platforms za watu kupata Kura ili waende Kula kwahio its all about people na hata hoja unazoleta zinakuwa ni uongo unaweza kuingia AI na kushusha nondo au kama Trump (Populist) kuwaambia watu wanachotaka kusikia na sio vitu practical na sustainable...
 
Walikosea timing,huwezi ukatafuta washabiki kipindi Cha miezi minne kabla ya uchaguzi. Ukifanya hivyo ni wazi nia yako ni kutaka wafuasi wakutafutie ubwabwa 🙂🙂
 
Allen nawewe naye, nilijua kichwani kwako zipo, kumbe mweupe hivi? Huoni hao ni kama olivyo ng'ombe wametawanyika kutafuta malisho? Hapo wanachotaka ni nafasi za udiwani na Ubunge, hakuna cha sera wala nini. Wasipopata, utaona wanakiacha hiko chama walichokipa umaarufu wa mpito, na huo ni mkakati tu.
 
Hapo wapo njiani kuelekea CCM
 
Back
Top Bottom