PreGE2025 CHAUMMA: Suala Siyo wingi wa watu bali wana hoja gani?

PreGE2025 CHAUMMA: Suala Siyo wingi wa watu bali wana hoja gani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kuna watu wanaiangalia CHAUMMA kwa jicho la mikutano yao kujaza ama kutokujaza watu. Na bahati mbaya na CHAUMMA nao wameingia kwenye mtego huo.

Nadhani chama cha siasa hakitambuliki kwa wingi wa watu wanaohudhuria mikutano yake, bali kwa hoja za chama husika kama zina manufaa kwa wanaohudhuria mikutano yao.

Jee hoja za CHAUMMA ya Sasa zina mashiko kwa watanzania na watoa hoja hizo wana maadili ya yasiyotiliwa shaka ili hoja zao ziaminike kwa watanzania?
Yani issue ya watu siyo kwenye chama tu, hata ufunguwe Pub kama haina vibe la watu itakuwa ya kawaida tu hiyo.

Nenda kitambaa cheupe ndio utaelewa naandika nini.

Mtaji wa siasa ni watu, hakuna Peoples power bila watu.

Chauma imekataliwa, tena bora Chauma ya Mzee Rungwe tupo tulikuwa tunamkubali mzee wetu anawafuata watu walipo masokoni anapiga mkutano, lakini baada kuwaribisha hawa njaa 55 hata Mzee Rungwe namuona ni mzee wa hovyo tu sasa hivi.
 
Acha kupindisha ukweli... Kipimo sahihi cha mikutano ya chama chochote ni idadi ya watu waliohudhuria, sio kwamba kila aliyehudhulia anakiunga mkono chama hko, hapana ila ujumbe unakuwa umefika.
Hawa wanasiasa wa mtandaoni dawa yao waambie tukutane site kwenye field ndipo wanakuja kugunduwa kumbe kujenga taasisi ni shughuri.

Halima Mdee yule akagombee Kawe nje ya Chadema muone kama atatobowa.

Jimbo liko wazi lakini ccm tayari kuna mitandao kama yote na hakuna ushindi wa mezani.
 
Hakika, na ndo maana hawataki kusikia habari ya reform, wanajua hawatapata ushindi wao wa goli la mkono
 
Kuna watu wanaiangalia CHAUMMA kwa jicho la mikutano yao kujaza ama kutokujaza watu. Na bahati mbaya na CHAUMMA nao wameingia kwenye mtego huo.

Nadhani chama cha siasa hakitambuliki kwa wingi wa watu wanaohudhuria mikutano yake, bali kwa hoja za chama husika kama zina manufaa kwa wanaohudhuria mikutano yao.

Jee hoja za CHAUMMA ya Sasa zina mashiko kwa watanzania na watoa hoja hizo wana maadili ya yasiyotiliwa shaka ili hoja zao ziaminike kwa watanzania?
Shida ya hiki chama ni cha wanafiki hawasaidiani hata kidogo mtu akipata shida wanaenda kufungua cham kingine what the hell.
 
Kuna watu wanaiangalia CHAUMMA kwa jicho la mikutano yao kujaza ama kutokujaza watu. Na bahati mbaya na CHAUMMA nao wameingia kwenye mtego huo.

Nadhani chama cha siasa hakitambuliki kwa wingi wa watu wanaohudhuria mikutano yake, bali kwa hoja za chama husika kama zina manufaa kwa wanaohudhuria mikutano yao.

Jee hoja za CHAUMMA ya Sasa zina mashiko kwa watanzania na watoa hoja hizo wana maadili ya yasiyotiliwa shaka ili hoja zao ziaminike kwa watanzania?
Chama ni watu; usijidanganye
 
Mbona ubwabwa wenyewe haujaliwa? Hata hao wachache hawajapata.
 
Mtaji wa chama chochote ni wanachama wake, sasa hata kama wana sera nzuri lakini wanahutubia watu 30 na ng'ombe wanne hizo kura watazitoa wapi ? Wingi wa watu ni ishara ya kukubalika.Nilichokiona jana pale Furahisha ni aibu kubwa, hata arusi ya kitaa tu ina watu na shamra shamra
Chama bado kipya tukipe muda.
 
Chama bado kipya tukipe muda.
Bado miezi 4 kuingia uchaguzi muda utoke wapi tena. Ishu ni kuwa hawa wahuni walijiaminisha kuwa walikuwa na uwezo wa kushusha tanga na kuapandisha tanga kama alivyfanya Marehemu Maalim Seif alivyotoka na nyomi yake ya CUF na kwenda ACT Wazalendo. Hawa kina Mrema na wenzake walikuwa desk officers pale Chadema HQ hawana uzoefu na siasa za majukwaani na ushawishi ndiyo maana wameshindwa kuondoka na nyomi, na pia ukweli kuwa wamefadhiliwa CCM nayo umewaharibia sana hakuna mpinzani mwenye akili anaweza kuwaamini na kuwafuata.
 
Mtaji mkubwa wa chama ni hoja (sera) kwanza - siyo watu!

Chama kikishakuwa na sera kabambe, hakiwezi kukosa watu.

Ndiyo maana wanaoanzisha chama siyo umma wa watu bali mtu au kikundi fulani cha watu wachache - ndipo watu wengine hujumuika kulingana na sera husika.

Ukiona chama kinakosa watu, au kinalazimisha watu wakipende, ujue sera zake zimeshachakaa - hazikubaliki kwa umma.
Sera ni muhimu ila kuna sababu nyingi zinazofanya watu wakipende chama. Hata haiba ya kiongozi ni muhimu. Mtu kama John Mrema na lafudhi yake ya kichaga hana kabisa haiba ya kuwa kiongozi mkubwa wa chama. Lowassa alikuwa anasimama jukwaani dakika chache na kusema tu elimu! Elimu! Elimu! Ila nyomi sio la kitoto.
 
Na ile interview ya juzi ya Mrema pale Clouds ambapo alishindwa kabisa kutoa tafsiri ya kiswahili ya No Reforms No Electinion ilimmaliza kabisa kisiasa.
 
Hoja yao kubwa jana ilikuwa helikopta 😅
Hata mie ndio nimeona imetajwa kwenye mitandao ya jamii! Wasife moyo, wawaombe wafafhili wao wawagawie wasanii kadhaa wapige show kabla ya kuhutubia majungu yao wataona turn up itakavyo kuwa. Hawaoni wafadhili pamoja na kuwa mikutano yao ni pumba tupu za kiwango cha juu lakini watu wanakuja ingawa show ni mwishoni ili wahorojoke kwanza
 
Ccm uko saa hizi wanapigana miguu ya shingo kugombea ubunge na Udiwani, huko ndio sahau kabisa watu wana mitandao yao huwezi kuingia leo ukatobowa.

Huyo Msigwa akigombea Iringa mjini kura za Maoni anapigwa na Mtambazavangu mapema asubuhi tu.
Anaweza kuteuliwa kuwa Afisa Tarafa/DAS/DED/DC
 
Allen nawewe naye, nilijua kichwani kwako zipo, kumbe mweupe hivi? Huoni hao ni kama olivyo ng'ombe wametawanyika kutafuta malisho? Hapo wanachotaka ni nafasi za udiwani na Ubunge, hakuna cha sera wala nini. Wasipopata, utaona wanakiacha hiko chama walichokipa umaarufu wa mpito, na huo ni mkakati tu.
Allen anajua sana… Shida ya waandishi ni moja tu washajua ChAUMMA kuna fungu limepelekwa hivyo wanajaribu kuandika andika ili waitiwe bahasha.

Waandishi wengi hufanya hivi.
 
Ni jambo la kusikitisha kuona hoja rahisi kama hii watu wanashindwa kuijadili kiufanisi.

Nimeona ni kama watu wameweka mkokoteni mbele ya punda ili auvute, haiwezekani.

Watu kujaa kwenye mikutano ya vyama vya siasa ni jambo Moja, na watu hao kuwa wafuasi wa chama husika ni jambo jingine tofauti kabisa.

Mikutano ya CCM huwa inajaa watu lakini unadhani ni kwa nini CCM hao hao wanaiogopa mikutano ya CHADEMA. Jee ni wingi wa watu ama ni kile kinachosemwa na watu wa CHADEMA kwa umati unaohudhuria mikutano yao?

Hoja ni kama sumaku, ukipata watu 100 na ukawaambia mambo ya maana siku nyingine hao watu 100 watawaalika watu wengine waje wakusikilize.

Lakini kama huna hoja kila wakati idadi ya wanaokufuata hupungua. Nani amesahau jinsi Lipumba wa CUF ya zama zile alivyokuwa anajaza watu. Jee Leo hii Lipumba ana uwezo huo?

Hoja yangu ni kwamba hao CHAUMMA wanatakiwa wawe na hoja kwanza kabla ya kufikiria kujaza viwanja vya mikutano ya hadhara.

Mwaka 1995 wakati Tanzania nzima tunadhani NCCR - Mageuzi ndicho kitakuja kuwa chama kikuu cha siasa, Mwalimu Nyerere aliiona CHADEMA kupitia sera zake na viongozi wake kuwa ndiyo itakuja kuwa chama kikubwa cha siasa baada ya CCM.

Lakini miaka kumi baadaye (2005) wakati tunamnadi Freeman Mbowe kwenye nafasi ya Urais, CUF ilikuwa mbele ya CHADEMA kiumaarufu. Leo hii CUF haipo ila CHADEMA imekuwa kubwa kiasi cha kutishia uhai CCM.

Hoja yangu ni kwamba CHAUMMA hawana Cha kuwaeleza watanzania hata kuwafanya watu waone umuhimu wa kujiunga kwenye chama chao.
 
Kuna watu wanaiangalia CHAUMMA kwa jicho la mikutano yao kujaza ama kutokujaza watu. Na bahati mbaya na CHAUMMA nao wameingia kwenye mtego huo.

Nadhani chama cha siasa hakitambuliki kwa wingi wa watu wanaohudhuria mikutano yake, bali kwa hoja za chama husika kama zina manufaa kwa wanaohudhuria mikutano yao.

Jee hoja za CHAUMMA ya Sasa zina mashiko kwa watanzania na watoa hoja hizo wana maadili ya yasiyotiliwa shaka ili hoja zao ziaminike kwa watanzania?

..katika mkutano wao wa Mwanza nimeona Chaumma wametumia muda mrefu kuwapondaponda Chadema.

..Chaumma wanatakiwa watengeneze identity / brand yao wenyewe, na sio kujinasibisha tu kama chama cha upinzani dhidi ya Chadema.
 
Back
Top Bottom