Mzee wa ubwawa wa Chauma Kwa mara ya kwanza amenyakua ushindi wa mgombea wake kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mtaa Jijini Mbeya.
Ikumbuke Mbeya Kwa kina Sugu ndiko Chadema wanajifanyaga ni ngome Yao lakini Wameambulia Sifuri yaani zero huku nafasi zote zikienda Kwa Tulia-CCM na Chauma ππππ.ππ
View attachment 3164865
My Take:
Ukiweka Wagombea wenye staha na maadili Wananchi wanakuchagua maana Viongozi wa Mitaa tunaishi wote huku huku tunatambuana sio sawa na Wabunge au Madiwani Hadi tuhadithiwe.
======
WENYEVITI WA MITAA MBEYA WABEBESHWA JUKUMU LA WATOTO WA MITAAN.
Wenyeviti wa Mitaa 181 ya Jiji la Mbeya kutoka vyama vya CCM na CHAUMA pamoja na wajumbe 905 wanaounda uongozi wa serikali za Mitaa, wameapishwa baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika na kutangazwa kuwa washindi kwenye nafasi hizo.
Wenyeviti hao 181, kati yao 180 wanatokana na chama cha mapinduzi CCM huku mmoja kati yao akitokana na chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMA, wamehimizwa kuzitumia nafasi hizo vyema ikiwa ni pamoja na Kupambana na ongezeko la watoto wa mitaani.
Mohamed Aziz ni Katibu tawala wa Wilaya ya Mbeya, anasema Kama viongozi wa serikali za Mitaa wakishindwa kusimamia usalama kwenye Mitaa yao hakutakua na utulivu hivyo ni jukumu lao kuyasimamia hayo, huku msimamizi msaidizi wa uchaguzi Ally Nnunduma akiwataka kuchangia mawazo yao katika maendeleo ya Jiji la Mbeya.
Nae mwenyekiti pekee anayetokana na chama cha ukombozi wa Umma, (CHAUMA) Brayan Mwakalukwa kutoka mtaa wa Soko kata ya Ruanda amesema anayofuraha kubwa kushinda nafasi ya mwenyekiti kupitia Chama hicho na anaahidi kutoa ushirikiano kwa wenyeviti wenzake, Diwani wa kata Ruanda na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt Tulia Ackson.
View: https://www.instagram.com/reel/DDADK0HIyvb/?igsh=ajJtc3Q0aGowZ29k