Ahsante kwa taarifa hii muhimu. Na pia, kusema kwangu CHADEMA wana mashabiki wengi mitandaoni sikumaanisha pia kuwa hawana mashabiki huko mitaani, kwenye ground. Nilitaka tu kusema kwenye mitandao karibu yote, inaonesha CHADEMA ina wapenzi wengi zaidi kuliko CCM.
Ushahidi mzuri ni hapa JF. Kipimo kimojawapo ni ule ushindani wa Juzi kumpata Mwanachama Bora wa mwaka 2022 kati ya Erythrocyte (Kada wa CHADEMA) na Pascal Mayalla (kada wa CCM). Pamoja na ukongwe alionao Pascal, bado ilishindwa na Erythrocyte. Hii inadhihirisha kuwa JF ina wapenzi wengi wa CHADEMA kuliko CCM.
Uwe na siku njema, Senior. Heshima kwako Mkuu.