Su-75 Checkmate sio ya kutisha sana hata. Waingereza wanakuja na 6th generation jet inaitwa Tempest, Wakorea kusini wanakuja na 5th generation jet, Wajapan wanaileta 5th generation yao. Hizi zote naamini zitaizidi Checkmate
China inazo stealth J-20 na kuna nyingine inatengengezwa na Shenyang kwa ajili ya Navy. Hawa wakizipa injini kamili nazo zitakuwa na maana kuliko Su-75
US wana F-22 na F-35 ziko kamilifu na Checkmate haiwezi zikaribia. Su-57 ndio itashindana nazo ila nayo haijapata powerful engine ya Izdeliye 30, kwa sasa inatumia AL-41 ambayo haifiki supersonic speed bila afterburners na haiko stealth
US pia wana NGAD (Next Generation Air Dominance) iko mbioni ilikuwa siri mpaka mwaka huu. Muhimu zaidi US wana advanced secure datalink kamili kuliko Urusi ingawa mpaka leo F-22 na F-35 haziwezi communicate ni mpaka zitumie relay nyingine mfano kupitia U-2 reconnaissance plane. Datalink inasaidia kushare target na guidance ya radar, etc. Bado wana projects kadhaa za stealth drones
Checkmate inaletwa kama stealth flani ya kuwauzia wateja wasio na uwezo wa kumudu gharama kubwa za stealth jets zilizoko sokoni, au wateja wasioruhusiwa kunua stealth zilizopo mfano Turkey ambayo inakufa na project yake ya stealth jet pia. Ikumbukwe Su-57 haijapata foreign customers na bado iko kwenye development, mpaka ifikie maturity sio leo. Checkmate wanadai mpaka 2022 utaanza initial production ila siwaamini Warusi huwa wana estimations za uongo. Checkmate ndio ndege pekee ya Urusi kwenye karne ya 21 iliyotengenezwa kwa lengo la wateja tu, hata jeshi lao halijui kama ipo
Possible customers wa Checkmate ni kama Algeria, Egypt na India lakini haitakiwi ichelewe. Na hilo jina litabadilishwa, wakati Sukhoi wanatengeneza Su-57 walikuwa wanaiita PAK-FA ila MoD ikaibadili jina ilipotoa order
Mambo ni mengi