GE2025 Chege Wambura aongoza kwa kura 7,866 jimbo la Rorya - Mara

GE2025 Chege Wambura aongoza kwa kura 7,866 jimbo la Rorya - Mara

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

CHEGE WAMBURA AONGOZA KWA KURA 7,866 JIMBO LA RORYA - MARA​

Mbunge aliyemaliza muda wake katika Jimbo la Rorya Mkoa wa Mara, Jafari Chege Wambura ameongoza katika kura za maoni kwenye jimbo hilo baada ya kupata kura 7,866.

Chege amewashinda makada wenzake wanne aliokuwa akigombea nao kwenye kinyang'anyiro hicho kufuatia uchaguzi uliofanyika nchini kote Agosti 4, 2025.

Katibu wa CCM Wilaya ya Rorya, Hassan Moshi amesema nafasi ya pili imekwenda kwa Sango Kasera aliyepata kura 4,785 huku Nyihita Wilfred akishika nafasi ya tatu baada ya kupata kura 1,034.

Nchama Wambura amekuwa wa nne katika uchaguzi huo baada ya kupata kura 380 huku nafasi ya tano ikienda kwa Peter Sarungi aliyepata kura 183.
 

Attachments

  • Screenshot 2025-08-06 at 15-57-20 Instagram.png
    Screenshot 2025-08-06 at 15-57-20 Instagram.png
    626.1 KB · Views: 38
Back
Top Bottom