Cheki Masanja anavyohaha, kweli kutunza mke si mchezo!

Hata kama masanja angekuwa kaandaa semina ya jinsi ya kutunza Pesa ni jambo LA hero na pia anastahili kufanya hivyo. Hii ni kutokana na historia ya maisha yake alikotoka ,kiwango kidogo cha elimu ya darasani na alipo sasa.

Kwa mtazamo wangu, si lazima mtu asomee Finance kuweza kumshauri mtu masuala ya fedha hasa fedha binafsi hizi tunazochangachanga. Katika maisha halisi tumeshuhudia wasomi wakubwa wa uchumi na mambo ya fedha wameshindwa kuishi taaluma zao lakini kuna watu kama masanja wanaweza kusaidia kwa kuwa wamepitia magumu na wamefanikiwa kwa kutunza na kukizalisha kidogo wanachokipata na sasa wako juu.

Sio kila jambo litahitaji maprofesa ,Tz ina maprofesa wangapi lakini wengi wao hawana msaada kwa Taifa. Bungeni tunao tele wanalala usingizi tu.Sana sana wanajua nadharia za kutunza fedha lakini mtu kama masanja anajua namna ya kutunza fedha kwa vitendo.
 
Husilazimishe kuelewa hujaelewa, umekurupuka
 
Mkuu unamchukia masanja sana. Sijui amekukosea nini.
 
Kodofan nadhani hujauelewa ujumbe wa Masanja...
Anawashangaa hao wanaolipa hiyo 100,000/=
 
Kwa vyovyote vile huwezi kumfikia masanja.Mwenzako ana Gari ya milioni70,mashamba na nyumba ikiwemo ghorofa
Ni sahihi akiwapa watu mbinu za kifedha hata kama ni mbinu pori kuliko wewe mwenye chuki binafsi
 
Mtu wa kwanza asiyeeleweka ni mleta thread hii
Kajiamiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiini kuleta pumba zake hapa
KASOMA BILA KUELEWA HALAFU ANATULAZIMISHA NA SISI TUSIELEWE KAMA YEYE...idiot...
 
Mtoa mada hakumuelewa Masanja ,yani unatoa laki kwenda kufundishwa namna ya kutunza kuanzia sh mia(
100)
 
Yani mleta thread hakuelewa masanja anazungumzia nini na alimaanisha nini na wachangiaji wengi nao hawasomi wanachangia tu
 
Ww nawe bure kabisa ...jua kutofautisha na kubainisha mambo.....the guy just joked.
 
asante kwa kumuelewesha vizuri..............anazani maisha yalivyomshinda yeye na wenzie ndo ivoivo.
 
Sio lazima sote tuwe waanzisha thread, ona sasa nini hiki.
 
mleta uzi ni KILAEIZA!...acha chuki binafsi fanya kaz uwe km masanja!...."au mke wa masanja alikuwa dem wako nn?" maana siyo kwa CHUKI hii ya waziiii! mfyuuuuuuu
 
hivi vijicho haviishi humu ndani eee, masanja kashachanja yuko mbali nyie vijicho tuuuu
 
Mtu akikuchukia hata ukicheza kwenye maji yeye atadai unamtimulia vumbi.

Umetumia nguvu nyingi bila sababu ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…