Chemba iliyokuwa inatiririsha maji taka kando ya Soko Jipya la Kariakoo yasafishwa

Chemba iliyokuwa inatiririsha maji taka kando ya Soko Jipya la Kariakoo yasafishwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
photo_2026-04-01_13-23-32.jpg
Juzi niliona mdau wa JamiiForums.com analalamikia kero ya chemba inayotililisha maji taka kando ya Soko Jipya la Kariakoo, ambalo lilizinduliwa katika siku za hivi karibuni.

Ilivyokuwa awali Chemba inayotiririsha maji taka kando ya Soko jipya la Kariakoo ni tishio kwa afya

Leo nimefanikiwa kupita mitaa hiyo, ambapo nimeona walau hali ni shwari tofauti na nilivyoikuta juma lililopita. Nimeuliza jamaa yangu anayefanya biashara eneo hilo; anadai mamlaka husika zilifika na kusafisha uchafu uliokuwa umesambaa, pamoja na kufanya ukarabati mdogo kwa kutumia vifaa vyao na kunyonya maji taka.

photo_2026-04-01_13-23-30.jpg

photo_2026-04-01_13-23-24.jpg
Wito wangu kwa mamlaka, baada ya kuwajibika katika suala hilo, ni vyema waendelee kuchukua hatua za kusafisha na kukarabati chemba korofi ambazo zimekuwa zikililisha maji taka, hali inayohatarisha afya za wananchi katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo. Miundombinu ya maji taka iboreshwe ili kupunguza kero na kulifanya eneo hilo la kibiashara kuwa safi muda wote.
 
Back
Top Bottom