KERO Chemba inayotiririsha maji taka eneo la Shoppers -Mikocheni, pembezoni mwa barabara inachangia mitaro kuziba

KERO Chemba inayotiririsha maji taka eneo la Shoppers -Mikocheni, pembezoni mwa barabara inachangia mitaro kuziba

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
photo_2026-05-13_12-55-30.jpg


Mitaro iliyopo kwenye barabara kutoka Shoppers Mikocheni Dar es salaam kuelekea Hospitali ya Kairuki imejaa maji machafu na taka, hali inayosababisha harufu mbaya na kuwa kero kwa wakazi wa maeneo hayo, hususan wafanyabiashara.

Hali hiyo pia inachangiwa na chemba inayotiririsha maji taka katika eneo la Shoppers, pembezoni mwa barabara hiyo. Chemba hiyo inatoa maji taka mengi yanayoelekea kwenye mitaro iliyoziba kwa uchafu, hivyo kusababisha maji machafu kutuama.

Hali hiyo ni hatari kwa afya za wananchi. Hivyo, nitoe wito kwa wasimamizi wa Shoppers pamoja na mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto hiyo, ikiwemo kufanya ukarabati wa chemba hiyo pamoja na kusafisha mitaro iliyoziba.
photo_2026-05-13_12-55-26.jpg

photo_2026-05-13_12-55-24.jpg

photo_2026-05-13_12-55-20.jpg
 
Back
Top Bottom