Chemsha bongo: Kusafiri baba na mtoto wa kike wa miaka 10

Chemsha bongo: Kusafiri baba na mtoto wa kike wa miaka 10

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,475
Salaam

Naleta mada hii kama chemsha bongo. Huwa natafakari Sana.

Je kama Baba napenda mwanangu wa pekee wa kike mwenye umri Kati ya miaka minane na kumi nambili, napenda kwenda nae safari ya mbali kwa sababu mbalimbali ukiwa ni pamoja na holiday tu.

Napenda kusafiri na mwanangu, pengine kwenda nae mikoa yenye utalii, kutazama vivutio vya utalii kama wanyama na kadhalika. Safari ambayo itatufanya tulale nyumba ya wageni ama hotelini. Tufanye uwezo wa kulala hoteli ninao.
  1. Sasa huwa najiuliza je ikifika muda wa kulala itakuaje?
  2. Je utachukua vyumba viwili kimoja changu na kimoja Cha mtoto?
  3. Au utachukua chumba kimoja chenye vitanda viwili?
  4. Au utachukua chumba kimoja na kulala na mwanao kitanda kimoja?
Hali hii kwa mama na mtoto wa kiume haina shida, shida iko kwa baba na mtoto wa kike.
Je ni sahihi baba kusafiri na mtoto wa kike?

Chemsha bongo ndugu zangu.

1621492685472.png

 
Hii tunaita, akinya kuku sawa ila akinya bata ni tatizo. Kwa mama umeona sawa, kwa baba umeona ni tatizo.
 
Ushasema mtoto ndugu yangu. Hata angekuwa na miaka 24 tafuta room moja lala pamoja kama wewe ni baba kweli wa mtoto. Chuchu zake saa sita kukuchoma mgongoni hiyo si kazi yako kuziwazia waachie wapenzi wake.
 
Duuh hili nalo tulijadili? Basi lala nao wote
 
Ushasema mtoto ndugu yangu.Hata angekuwa na miaka 24 tafuta room moja lala pamoja kama wewe ni baba kweli wa mtoto.Chuchu zake saa sita kukuchoma mgongoni hiyo si kaz yako kuziwazia waachie wapenz wake
Unatania najua
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ushasema mtoto ndugu yangu.Hata angekuwa na miaka 24 tafuta room moja lala pamoja kama wewe ni baba kweli wa mtoto.Chuchu zake saa sita kukuchoma mgongoni hiyo si kaz yako kuziwazia waachie wapenz wake
 
Ushasema mtoto ndugu yangu.Hata angekuwa na miaka 24 tafuta room moja lala pamoja kama wewe ni baba kweli wa mtoto.Chuchu zake saa sita kukuchoma mgongoni hiyo si kaz yako kuziwazia waachie wapenz wake
Shida sio chuchu,shida Ni usalama. Mtoto wa kike wa miaka 24 anaweza kulala chumba Cha pekee yake.
Mwanangu wa miaka 10 Nitakua na wasiwasi kulala pekee yake.hoteli au gesthouse.
 
Shida sio chuchu,shida Ni usalama.
Mtoto wa kike wa miaka 24 anaweza kulala chumba Cha pekee yake.
Mwanangu wa miaka 10 Nitakua na wasiwasi kulala pekee yake.hoteli au gesthouse.
Wababa siyo wa kuwaamini ndugu, achukuliwe tu chumba tofauti. Uchungu wa mwana aujuae mwanamke.
 
Hii tunaita, akinya kuku sawa ila akinya bata ni tatizo.
Kwa mama umeona sawa, kwa baba umeona ni tatizo.
Mama zetu wanatuhudumiaga watoto wote, wa kike na wa kiume hata tukifika sekondari, lakini baba kumhudumia mtoto wa kike mwisho miaka miwili.
 
H
Wababa siyo wa kuwaamini ndugu,achukuliwe tu chumba tofauti.Uchungu wa mwana aujuae mwanamke
[/ QUOTE]
Japan hoja yangu iko kiusalama zaidi,sasa ntakua na hofu kabinti langu ka miaka 10 kulala pekee yake,usalama na sita kuwa naamani.

Kumfanyia ubaya binti yangu Wala sifikirii Kabisa,hofu Ni kulala pekee yake.akipata shida usiku itakuaje.

Kama baba Ni mbaya hasubiri mpaka wasafiri,anaweza mfanyia ubaya hata akiwa nyumbani.
Hebu fikiria Gest umweke mtoto chumba Cha pekee yake unazingua akilini kweli? Tena katoto ka kike.
 
Kila mtu chumba chake
Hata kama ni mama na mwana

ila usalama sijui utalinda vp
Labda umfungie ndani
Milango ya kadi ile kufunga kwa ndani utakwama
 
Generally sio salama
Nishasafiri na mshua zamani sana nna miaka 12 kutafuta shule hzi form one

kila mtu chumba chake
Sa 4 or so mtu anagonga
Akili yangu ya kitoto japo timamu nikaita baba ni wewe?
Kimyaaa
Sikufungua lakini kdogo nifungue mana he was next door
Kiusalama sio nzuri

heri apartment or so
 
Haina tatizo, kabisa, kwanza mtoto hasa wa kike anamuamini Sana baba,Kama yeye anakuamini, nadhani na wewe inatakiwa ujiamini,uonyeshe Imani yako kwake,Mimi katoto kangu kako standard four,ten years,kakija kanataka kulala na Mimi,na hakuna tatizo,hata kakiwa na shida kananiambia baba,nataka taiti au huku na huku kamenizoea na kananipenda Sana Kama baba yake,kuliko hata mama yake nadhani.
 
Kama ni hoteli, chukua chumba kimoja vitanda viwili. Mtoto wa miaka 10 kumuacha alale peke yake hotelini kama mama sikubaliani, haijalishi wa kike au kiume. Nahofia usalama.
 
Bora uchukue chumba kimoja chenye vitanda viwili tu kwa usalama zaidi.
 
Back
Top Bottom