Chemsha bongo: Shilingi 100 iko wapi?


Jamaa walikukopesha jumla ya shilling 10,000/= Hii inamaana kwamba kila mmoja alikukopesha shilling 5000/=. Mpaka hapo tuko sawa na maelezo yako.
Sasa basi kama ulipunguziwa ukauziwa kwa shilling 9700/= maana yake ni kuwa kila mmoja alikuchangia shilling 4850/=. Hivyo basi kama ungerudisha bila kubaki na hela yoyote ungemrudishia kila mmoja shilling 150/= (kwa watu wawili inakuwa 300/=) Ila wewe ulirudisha shilling 100/= kwa kila mmoja ambayo ambayo inaleta jumla ya shilling 4950/= kwa kila mmoja(4850/= + 100/=) Hivyo kila mmoja alibaki anakudai shilling 50 ambayo jumla yake ni 100/= ndo ile 100/= uliyobaki nayo. Hivyo bas ulitakiwa kabla ya kurudisha change uhjue mchango wa kila mmoja kwa kwenye ile bei uliyo nunulia i.e (9700/2 = 4850). Kama ungejua hilo basi inamaana kuwa ungegundua kuwa kila mmoja anastahili kuata shilling 150/= kwenye ile change yaanai shilling 300/= iliyobaki ila wewe ukawapa shilling 100/= ambayo inaleta jumala ya shilling 4950/= maana yake ni kuwa kila mmoja alibaki anakudai shilling 50/= amabayo ndo ile inakupatatia shilling 100/= uliyobaki nayo.
 
Bado unadaiwa .
Unapomrudishia kaka sh 100 na dada sh 100 kutoka kwenye punguzo la sh 300 ,unabakiwa na sh 100 yako mwenyewe.
dada na kaka wote wanakuwa na sh 4,900 kila mmoja. Hapo bado unatakiwa urudishe deni la sh 200 yaani sh 100 kwa kaka na sh 100 kwa dada. Kwa hiyo bado unadaiwa sh 200 ila ukiongeza na ile ya kwako sh 100 uliyoichukua kutoka kwenye punguzo unabaki na deni la sh 100.
 
Hili swali mbona lisharudiwa sana kule kwenye jukwaa la jokes na mazagazaga!
 
Subiri Kongosho akuje yeye ni bingwa wa Maths sana!
 
Last edited by a moderator:
Subiri Mwanaasha aje akujibu....
 

Nimekuelewa. Ila unatakiwa ufuate mgawanyo nilioutumia mm kisha unioneshe hiyo 100 inapunguaje, kama nilikosea kimahesabu nk
 
Nimekuelewa. Ila unatakiwa ufuate mgawanyo nilioutumia mm kisha unioneshe hiyo 100 inapunguaje, kama nilikosea kimahesabu nk
Logic unayotumia siyo sahihi. Logic ya Chona ndiyo sahihi. Hesabu ni logic.
 

Sasa kama wewe uliekopeshwa hujui ilipokwenda,
mimi ambae sikuwepo nitajua ilikoenda?
 
Khaa! Hili swali sasa mpaka linaboa. Kila siku linaulizwa!
 
Iko hivi -5000+100=-4900 deni kwa kaka ambalo ni sawa na deni kwa dada. 300 tunaita pato au +300. Deni halisi ni -4900-4900+100= -9700. Assumption yako hapa siyo sahihi yaani -4900-4900+100 NOT EQUAL TO - 9900.
 
Hapa wangu umeniacha hoi sana!
Ila kweli ukiangalia utajua jamaa hayuko makini anapo pewa pesa!
Sasa kama wewe uliekopeshwa hujui ilipokwenda,
mimi ambae sikuwepo nitajua ilikoenda?
 
utadaiwa 9800 na kaka na dada,hutakiw ku add ile 100 uliyo baki nayo ni punguzo na si deni..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…