Chemsha bongo: Shilingi 100 iko wapi?

we inaonesha hata bam 2 hukuxoma!!wanahexebu huwa ha2complicate lugha!!xo gpange bc
JF jamani kuna watu wa marika yote ni muhim basi kutumia lugha fasaha badala ya alama za ajabuajabu kulikuwa na haja gani ya kutumia hizo alama kufupisha post au ni ku-save muda au herufi s haipo kwenye iyo nanii yako .....naomba jamani kwa nia njema tu....hii sio facebook.....au kama vipi mode aanzisha majukwaa maalumu kwa lugha kama hizi...ni angalizo tu
 
Hapo unge-include na waliosoma Book keeping, Accounting, Finances...
 
safi kijana hapa kila mtu atakuelewa sio ile staili ya x badala ya s
 

mkuu unabishana na aliyesoma BAM advance naye anataka kuonesha kua anajua math.
 
mkuu unabishana na aliyesoma BAM advance naye anataka kuonesha kua anajua math.

Mkuu nimekupata, hapa tatizo sio BAM ni basic mathematics knowledge tu inatosha. hata kijana alie fanya mtihani wa hesabu form four jana anatakiwa kujibu seali hili,sio mpaka asome BAM au Advanced Mathematics A-Level
 

kaka maelezo mazuri ila hapo kwenye bold nadhani ilipaswa kuwa "pesa uliyo nayo (+) na sio (-)" otherwise umesomeka ipasavyo.
 
Eti kwa mfano upo sokoni ukapenda nguo ya sh. Elfu kumi (10,000) ila huna hata senti ukakopa kwa dada elfu tano(5000) na kwa kaka elfu tano(5000) baada ya kufika kwa muuzaji ukamuomba akupunguzie na akakupunguzia sh 300 ukanunua kwa elfu tisa mia saba(9700) baada ya kurudi nyumbani ukaamua kupunguza deni dada ukampa mia moja(100) na kaka ukampa mia moja(100) kwahvyo wote wakawa wanakudai 4900 kwa kila mmoja ambapo jumla yake ni elfu tisa na mia nane(9800) ukijumlisha na mia uliyobakiwa nayo inakuwa elfu tisa mia tisa(9900) sasa je ili kukamilisha hesabu ya sh elfu kumi mia inashort je hiyo mia imepotelea wapi?
 
ka swali kanachangaja
ila in accounting view hiyo inaitwa trade discount
itakuwa imepotelea kwa aliyekuuzia
dr.discount allowed
dr.bank/cash
cr.account receivable
kama nimekosea niambieni maana nilisha sahau kufunga vitabu!siku hizi tuna sign cheque tu
naomba aje mwingine na mathematics view!
 
, Hkuna hela iliyopotea,hapo ni suala la assets na liability,deni ni liability na hiyo pesa nyingine ni assets,huwezi kuchanganya asset na liability ukapata jawabu.
 
its very simple hyo pesa haijapotea wala nini iko ivi chukua hyo pesa ambayo ulinunulia nguo ambayo ni 9700 ukiigawanya kwa mbili ni 4850 ambayo kila m2 alikuchangia katika kununua ivyo ukiizidisha mara mbili unapata 9700 ukijumlisha mia mia uliyoirudisha inakuwa 9900 na ile mia iliyobaki inakua 10000
 
,Hkuna hela iliyopotea,hapo ni suala la assets na liability,deni ni liability na hiyo pesa nyingine ni assets,huwezi kuchanganya asset na liability ukapata jawabu.
sijakupata ndugu yangu dadavua vizuri!
siunajua hesabu imepita kushoto
 
sijakupata ndugu yangu dadavua vizuri!
siunajua hesabu imepita kushoto

Anachosema i believe ni kwamba, mfano mimi nina sh 1 wewe unanidai sh 3, siwezi kuongeza sh 1 yangu niliyonayo kwenye deni la sh 3 ikawa sh 4. Ndo kilichofanyika hapo juu deni ni 4900 kwa kila mmoja ambao jumla wanakua wanakudai 9800 inakuaje unaongeza 100 uliyonayo kwenye deni afu ikawa 9900? Deni la 9800 na sh 100 ulionayo hauwezi viongeza maana hili ni deni hiyo 100 ni hela unayo. Ukiamua kuwapa 100 hiyo wote watabaki wanakudai 9700. Get it?
 
Ili swali tayari limo humu. Yamo kama ma5 hivi, meng kiasi kwamba mengine yapo kwenye jukwaa la jokes
 
NAJUA WE MSOMI. HEBU NISAIDIE HILI SWALI.
umekwenda town umekuta nguo inauzwa 10,000/=. we huna ela, unaenda kukopa 5000 kwa dada na 5000 kwa kaka, unapata 10000 unaenda kupatana unauziwa kwa 9700 unarudishiwa 300, unaamua kupunguza den sh.mia kwa dada na sh.mia kwa kaka, unabaki na mia, dada anakudai 4900 na kaka anakudai 4900 ukijumlisha unadaiwa 9800 ukijumlisha na mia yako inakuwa 9900. sh.mia imeenda wp ili itimie elfu kumi? nasubir jibu,
 
umekwenda town umekuta nguo inauzwa 10,000/=. we huna ela, unaenda kukopa 5000 kwa dada na 5000 kwa kaka, unapata 10000 unaenda kupatana unauziwa kwa 9700 unarudishiwa 300, unaamua kupunguza den sh.mia kwa dada na sh.mia kwa kaka, unabaki na mia, dada anakudai 4900 na kaka anakudai 4900 ukijumlisha unadaiwa 9800 ukijumlisha na mia yako inakuwa 9900. sh.mia imeenda wp ili itimie elfu kumi? nasubir jibu,
 
Hiki kiswali sasa kimekuwa kama wimbo wa taifa.

Kila siku lazima kiletwe hapa. Mpaka sasa sijajua ni kwanini asee

Inaelekea watu wengi ni vilaza wa hisabati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…