Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

Chenge ashikiliwa polisi kwa ajali ya gari iliyosababisha vifo

- Ahsante Mkuu kwa hii habari, naona ndio basi tena shughuli hii imeisha Mungu Aibariki Tanzania.

William.

Malecela J. W

Damu za watu huwa hazimwagiki bure, tuna mifano mingi Marehemu Dito yuko wapi? Simwombei mabaya homeboy Chenge ila hii mikosi kuna makubwa yatamkuta.

Masa
 
ushauri wangu wa bure, isije ikatokea nasi mmoja wetu akagonga na kukimbilia polisi kujisalimisha, tutakwisha, tutaisaidia polisi haswa,huyo alikuwa mh. chenge. mkuu halisi amesema kwamba kuna jamaa yake amekaa ndani wiki 2.

RIP wadada!
 
Chenge kaachiwa kwa dhamana na ameondoka ndani ya gari aina ya Toyota Harrier namba T193 AYL.

Taarifa za kipolisi zinasema mwenye Bajaj ndiye alikuwa na makosa na huenda ndiyo sababu iliyopelekea yeye kukimbia (anageuziwa kibao?)

Kuna walinzi waliokuwa eneo la tukio, huenda hawa wakatoa msaada wa hali halisi. Walinzi hao wanasema kwamba, dereva wa Bajaj alipona gari la Chenge linamfuata upande wake akalikwepa na kuruka ndipo kina dada wa watu waliokuwa wakitokea Club Maisha wakajikuta hawana msaada na kugongwa wakiwa pekee bila dereva. Kwa kuwa dereva hajulikani alipo, kila kitu kitamuelemea yeye na huenda akionekana ataambulia vijisenti akanunue Bajaj zake kadhaa (asiajiriwe tena).

Kuna habari kwamba kina dada hao wanatokea mkoani Mwanza na leo walikuwa waelekee Zanzibar kwa ndege kufanya shopping kabla ya kurejea kwao, mmoja akitajwa kuwa Bi harusi mtarajiwa

Invisible,

Sijaelewa kabisa hapo nilipo-bold blue!

Ina maana ni uso kwa uso ama wote walikuwa wanaelekea same direction?
 
JF Imeingiliwa na spin master wengi,na asilimia kubwa wanakurupuka bila kuleta hoja kwanza.

Tumekimbilia kumsema chenge tu kwa kutumia hisia kuwa ni fisadi bila kuangalia uhalisia na ukweli wa tukio lenyewe,inatia shaka kwa watu wengi kujadili mambo bila ya kuwa na data zozote!

Tumeanza hadi kufikia kuhisi haki haiwezi kutendeka,tumejenga tabia ya kutoaminiana,tunaogopana na kusemana,tumekuwa wepesi wa kufitini ,tusio na upole wa kunyamaa..what if dereva wa bajaj ndiyo mwenye makosa?au kwa kuwa hana mali?tumekuwa na tabia ya kubaguana.

Invisible , ungetakiwa ufanye utafiti na ujue namba za bajaj ni zipi,alafu nenda pale TRA wakupe jina la mwenye usafiri huo then atafutwe na aeleze jina la dereva wake..

Hatua itakayotakiwa kufuatwa ni polisi kuanza kumsaka dereva,na kwa kuwa serikali ina mkono mrefu itampata.

Mie naamini hata yule dereva wa mama mbatia anaweza kupatikana..

Lets stop being speculators,na mwalimu wenu namuonya aache kuwafundisha hadithi!
 
Kwa hiyo at least ataonja Keko? Naona faraja.

Mkuu wangu Jasusi,

Usione faraja mtu mwingine anapopata matatizo hata kama ni adui yako. Muhimu tu ni kuomba mkono wa sheria ufuate mkondo wake.
 
I told you mwenye Bajaj atakuwa mkosa tu,na ndipo tunapolekea,na ikiwa ataponea chupuchupu basi gari lachenge litakuwa na brake failure ,na mambo yatawaokoa wote wawili.
Niligonga mtu mwaka wa 1974 na kulivamia guzo la taa ,niliteremka ndani ya basi kama radi inavyoshuka na kwenda kukata waya za brake,polisi walipofika walikagua na mafuta ya brake yanavuja ,wakaandika statement kuwa si kosa langu bali ni la brake failure na baadae niliponafasika nao nikawakatia chao bima ikalipa guzo la taa na kuwapatia chochote wafiwa ,Bongo mwisho.Ujue tu namna ya kuzungumza na watu hongera ZZM.
 
Kesi ndogo sana ,nawaonea huruma waliopoteza maisha...Mungu awapumzishe salama...ila kwa vijicenti anamaliza fasta hy kesi hakuna kitu hapo...mtaona...hata hawezi kulala leo....
 
ungetakiwa ufanye utafiti na ujue namba za bajaj ni zipi,alafu nenda pale TRA wakupe jina la mwenye usafiri huo then atafutwe na aeleze jina la dereva wake..

Hatua itakayotakiwa kufuatwa ni polisi kuanza kumsaka dereva,na kwa kuwa serikali ina mkono mrefu itampata.

Jembe,

Kuna post moja wapo hapo juu inasema mmiliki wa Bajaj amishafika kituoni kuhojiwa!! Tanzania ninayoijua mimi mwenye fedha na madaraka wakati wote hushinda kesi....na kama dereva wa Bajaj angekufa makosa yote angesingiziwa marehemu. Chenge saa 9 usiku alikuwa anatoka wapi na gari lisilo na bima? makaburini ama viwanja peke yake bila mkewe wala dereva?
 
JF Imeingiliwa na spin master wengi,na asilimia kubwa wanakurupuka bila kuleta hoja kwanza.

Tumekimbilia kumsema chenge tu kwa kutumia hisia kuwa ni fisadi bila kuangalia uhalisia na ukweli wa tukio lenyewe,inatia shaka kwa watu wengi kujadili mambo bila ya kuwa na data zozote!

Tumeanza hadi kufikia kuhisi haki haiwezi kutendeka,tumejenga tabia ya kutoaminiana,tunaogopana na kusemana,tumekuwa wepesi wa kufitini ,tusio na upole wa kunyamaa..what if dereva wa bajaj ndiyo mwenye makosa?au kwa kuwa hana mali?tumekuwa na tabia ya kubaguana.

Invisible , ungetakiwa ufanye utafiti na ujue namba za bajaj ni zipi,alafu nenda pale TRA wakupe jina la mwenye usafiri huo then atafutwe na aeleze jina la dereva wake..

Hatua itakayotakiwa kufuatwa ni polisi kuanza kumsaka dereva,na kwa kuwa serikali ina mkono mrefu itampata.

Mie naamini hata yule dereva wa mama mbatia anaweza kupatikana..

Lets stop being speculators,na mwalimu wenu namuonya aache kuwafundisha hadithi!

Mkulu wangu Gembe, heshima mbele sana,

- Baaada ya kuambiwa kwamba Chenge alikuwa anatafuta kitichake bungeni saaa tisa za usiku, tena kimwagia unga unga kwenye viti anavyofunua ni haki yetu wananchi ku-speculate anything kinachomhusu, kwa sababu hatumuamini tena,

- Ingawa bado una hoja nzito lakini ya kumhusu chenge ni fair game ku-speculate.

Respect!

FMEs!
 
Udogo wa kesi hii umezuka vipi?

Watu wangapi wako jela kwa kosa la kugonga na kuua?

Kama kuna sheria 2, za Mafisadi na za walalahoi juu ya tukio moja hilo nalikubali, kwa sababu ni wazi sheria ya Mafisadi itatumika.

Fisadi akipiga mtu risasi ya kichwa mchana kweupe mbele ya halaiki ya watu bado hana cha kujibu mbele ya mahakama mpka Mungu aingilie kati.

Kuua ni kosa la jinai lenye kujigawa mafungu mawili.

1 kuua kwa kusudia.
2 Kuua bila kukusudia.

Kuua haijawahi kuwa kesi ndogo, mtu au kikundi cha watu kisilete uongo hapa.
 
Last edited:
Mkuu wangu Jasusi,

Usione faraja mtu mwingine anapopata matatizo hata kama ni adui yako. Muhimu tu ni kuomba mkono wa sheria ufuate mkondo wake.

Mtz,
Hujui madhara aliyotufanyia (binafsi) huyu mtu bwana.
 
Mkulu wangu Gembe, heshima mbele sana,

- Baaada ya kuambiwa kwamba Chenge alikuwa anatafuta kitichake bungeni saaa tisa za usiku, tena kimwagia unga unga kwenye viti anavyofunua ni haki yetu wananchi ku-speculate anything kinachomhusu, kwa sababu hatumuamini tena,

- Ingawa bado una hoja nzito lakini ya kumhusu chenge ni fair game ku-speculate.

Respect!

FMEs!
FMES,
Navyomfahamu Chenge ni mtu wa kilaji na inawezekana alikuwa anatoka pale elders club,ntampigia kumuuliza the whole story!
 
Mbingu ni zako ee bwana, na nchi yako ndiye uliyeumba kila kitu kilichomo, binadamu na kile kinachoonekana na kisichoonekana!
 
Kwa mujibu wa gazeti la Alasiri, habari hii inaandikwa kuwa Mheshimiwa Chenge alikuwa akiendesha kwa kasi (alikuwa amekaribia nyumbani kwake), kabla Bajaj haijamchomekea (Bajaj ikiingia barabarani ghafla). Mheshimiwa Chenge alipoona hivyo, alishindwa ku-control gari lake, na hatimaye akagonga Bajaj hiyo na kusababisha ajali hiyo na hatimaye vifo vya watu wawili.

My take: Kwa muda huo wa saa 10 asubuhi, ni wazi kuwa kama alikuwa akirudi nyumbani, atakuwa alikuwa akiendesha gari akiwa amechoka sana na uwezekano mkubwa ni kuwa alipatwa na usingizi akiwa anaendesha. Inawezekana pia kuwa alikimbilia nyumbani kutoa taarifa na kutokana na mshituko, hakujua cha kufanya kwa haraka.

Saa 10 asubuhi kuna magari katika barabara nyingi za Dar, ni muda ambao watu wanaosafiri asubuhi na wengine kuwahi makazini wanakuwa njiani. Muda huo pia ni mapema asubuhi na jua huchomoza muda mfupi sana kutoka muda huo. Sidhani kuwa Mhe. Chenge alikusudia kukimbia ajali hiyo kwa namna yoyote (kukwepa lawama, tatizo ama chochote kama hicho). Nadhani aliona ni vyema kwanza kutoa taarifa nyumbani (ambapo alikuwa amekaribia sana kufika) na hatimaye kulishughulikia tatizo lililomkuta.

Ajali ni kitu kinachoweza kumpata yeyote. Japokuwa ajali nyingi ni za kizembe kuliko bahati mbaya (hivi bahati inaweza kuwa mbaya?).
 
Mbingu ni zako ee bwana, na nchi yako ndiye uliyeumba kila kitu kilichomo, binadamu na kile kinachoonekana na kisichoonekana!

Uwaokoe watanzania walio mandondocha,wape ujasiri wa kujua uovu wa viongozi,

Eeh baba naomba uwape kichaa wale wote wenye tamaa ya ufisadi,

Mungu baba uliye na nguvu na mamlaka.,tuepushe na Rais huyu kwa kuwa anatupeleka kubaya

Yehova el shalai,tuna watu wanajiona watatu watakakitu,waondoshe mbali kwa kuwa wamejaa uovu

Bab,Namuombea Mzee mwanakijiji,mpe nguvu na hekima,ujasiri na upeo,mepushe na wana wa mafisadi.

Kristo uliye mfalme ibariki jamiiforums,iwe mfano,iwe na wajenga hoja,iepushe na laana ya tabia ya kibaguzi.

Siku zote umekuwa mwema na kunijibu maombi yangu,na sasa naomba utende ikupasavyo na kwa maoni yangu

Naomba haya yote,mimi Gembe mwenye upeo zaidi ya walevi wa madaraka..kwa jina la yesu.Amen
 
1539.jpg

1538.jpg

1536.jpg

1527.jpg

1523.jpg

Polisi akiokota mabaki ya bajaji bila kuvaa gloves

1521.jpg

1520.jpg

1528.jpg

Sakata lingine lilikuwa kwa familia ya Chenge hasa upande wa mtoto wake wa kike ambaye aliondoka kituo cha Polisi na kwenda nyumbani kubadilisha nguo mara ya kwanza alikuwa amevalia suruali na brauzi , akaenda kubadili na kuvaa gauni jambo liliwashangaza baadhi ya watu waliofurika hapo polisi,
Pia muda wote alikuwa bize akiongea na simu huku akiwa amevalia miwani meusi.

Mbingu ni zako ee bwana, na nchi yako ndiye uliyeumba kila kitu kilichomo, binadamu na kile kinachoonekana na kisichoonekana!

Ameni MKJJ,

Madereva wote walikimbia,tumegunduwa mmoja wapo hakuwa na insurance kwa miaka miwili,na raia wema wamekufa kutokana na ajali ambayo inaweza kuwa imesababishwa na matatizo ya ulevi.

Nimeshindwa kabisa kuielewa taarifa ya mwisho ya Invisible kwasababu amesema kuwa dereva wa Bajaj aliliona gari la Mh Chenge likimfuata upande wake,ikiwa na maana kuwa hawakuwa upande mmoja kama ilivyosemwa hapo awali.

Na pia kwenye maelezo hayo,hakuna pahali ambapo wamesema kuwa ni nani haswa aliwagonga kina dada hao na inavyoonekana ni kwamba maadai yao ni kuwa wakina sdada hao hawakuwa kwenye Bajaj bali walikuwa kando ya barabara,kwamba Mh Chenge aliigonga Bajaj pamoja na kina dada hao,sasa dereva mwenye Bajaj makosa yake yapi hayo? Kukimbia? Chenge na yeye si alikimbia? Na kama polisi walipata taarifa kuwa ni Chenge,then inawezekana walimwambia kuwa dereva mwingine kakimbia ama inawezekana pia walimshurutisha kukimbia moja kwa moja ili kumake deal smooth.

Kama dereva alifuatwa upande wake,then whats the implications?

Na hata kama huyo dereva hajapatikana,bado kuna ushahidi wa kutosha tu wa kupress charges,kuna aliyekuwa akiendesha bila insurance,akiwa mlevi na kwenda kuigonga Bajaj na raia wema kina dada wa watu,pia hakusimama na alikwenda polisi kesho yake.
Sasa complications nyingi hazina mpango,hata kama familia ya marehemu ikiamua ku settle,bado kuna mashtaki madhubuti kabisa ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania dhidi ya Mh Chenge,hapo ndo kutakapokuwa kwenye shida,na si civil lawsuit ama anything else kama vile kusettle na family. Sheria za wenzetu kama USA, hata kama wenye kesi wakijitoa bado federal inaendelea na kesi yake...Ila bongo sidhani,maana ya ufisadi hajaguswa ndiyo iwe hii?
 
Uwaokoe watanzania walio mandondocha,wape ujasiri wa kujua uovu wa viongozi,

Eeh baba naomba uwape kichaa wale wote wenye tamaa ya ufisadi,

Mungu baba uliye na nguvu na mamlaka.,tuepushe na Rais huyu kwa kuwa anatupeleka kubaya

Yehova el shalai,tuna watu wanajiona watatu watakakitu,waondoshe mbali kwa kuwa wamejaa uovu

Bab,Namuombea Mzee mwanakijiji,mpe nguvu na hekima,ujasiri na upeo,mepushe na wana wa mafisadi.

Kristo uliye mfalme ibariki jamiiforums,iwe mfano,iwe na wajenga hoja,iepushe na laana ya tabia ya kibaguzi.

Siku zote umekuwa mwema na kunijibu maombi yangu,na sasa naomba utende ikupasavyo na kwa maoni yangu

Naomba haya yote,mimi Gembe mwenye upeo zaidi ya walevi wa madaraka..kwa jina la yesu.Amen
una maana hata sisi hapa ni Mandondocha?
 
Back
Top Bottom