Chief Mangungo 2.0 na Ujinga wa Mwafrika 2013..

Nimekuwekea hapa, sheria ya Uingereza inavyosema kuhusu hili swala.
Hizo act wala zisikutishe sana, kama kuna interest ya jamii wakiiona imedhulumiwa watatumia maandishi hayo hayo kukuanzishia na kukufungulia kesi. Kwanza watakuita kwenye parliamentary committee (hapo ndio most details za mkataba utajulikana) kuwahoji waziri na baadae mdhabuni wajue kama mchakato wa mkataba ulikuwa fair kwa taifa (sio committee zetu raisi anaweza zuia watu wasiende si ndio upuuzi wenyewe huo). Hapo sasa ndio watatoa interpretition zao za maandishi ya act na kila mtu alivyoelewa yeye na kukutafutia sababu ya kesi.

Mfano Starbucks, Amazon and google haya ndio makampuni kwa sasa ambayo wameyaamulia kuwa hayalipi kodi vizuri kutokana na faida wanazopata, jamaa walichofanya sio nje ya sheria za nchi lakini walibanwa mpaka kuonyesha nia yao ni kutolipa kadi kwa kutumia loopholes at their advantage. Aim hapo ni kuwaweka wazi hawa si wenzetu na kuwachafua for not being ethical (its their culture thing but it matters a lot), wananchi hapo watawachukia, mbona wenyewe wameomba kuongezea kulipa bila ya kubadilishwa sheria. Halafu kitakacho fuata ni kurekebisha hicho kipengele kilichopo.
 
Tunagawa bure bure kama hatuna akili nzuri. Kuna siku tutapojigundua kuwa tumekuwa wajinga tuliopitiliza, sijui tutamlilia nani. Ifike mahala sasa tuamue kuanza kufikiri seriously about what we need now and in the future.
 
Kwani waafrika wote wapo CCM hapa unaelezewa ujinga wa Mwafrika siyo ujinga wa Watanzania kama unavyotaka.
Wanaotawala lazima wawe werevu ili wasiendeleze ujinga. chifu mangungo alikuwa mtawala na sasa wapo watawala wanafanya kama Mangungo. sasa watawaliwa wanatiwa ujinga na kukubali au nao ni wajinga. maana kwa mujibu wa Mzee Mwanakijiji tayari watawala ni wajinga.
 
Mkuu mawazo yako ni mazuri and I wish ingekuwa hivyo katika ulimwengu wa Ukweli.

Mawazo gani?

1. Mimi na wewe tunakubaliana kuhusu reduction, refer post zangu zote( Isipokuwa wewe umeiita reduction, na mimi nimeiita Talking points)

Sijazungumzia reduction, nimezungumzia redaction. Big difference. Na wala redaction si talking points.

2. Hata Nchi ambazo freedom of Information iko juu na inaheshimika kama uingereza, inapokuja kwenye Mikata ya kibiashara huwa wana refuse kutoa Information. Sasa sijui wewe ndugu yangu una mfano wa nchi gani.

Kwa nini Uingereza iwe ndiyo yardstick yetu wakati hali yao ya uchumi si kama yetu, maendeleo yao ya elimu si kama yetu, historia yao si kama yetu?

Nimekuuliza kwamba je, nchi zote duniani zinafanya mikataba yake siri? Hukunijibu.

Mfano wa nchi ya dunia ya tatu yenye kutoa uhuru kabisa katika haya mambo unaweza kuwa pertinent kwetu zaidi kuliko wa Uingereza.

Halafu hata hao Waingereza wana semblance ya openness ambayo sisi hatuna.

Leo naweza ku Google mshahara wa mbunge wa Uingereza, na historia ya mshahara huo. Tanzania siwezi kufanya hivyo.

Nikitaka hata kuangalia pa kuanzia naweza. Kuna websites kama Home - Public Contracts Scotland

https://www.gov.uk/contracts-finder


Hawa jamaa wanatuambia tunaweza kupata habari za "previous tenders and contracts" contradicting what you are telling us kwamba hatuwezi in your point 2 above.

3. Confidentiality hata mimi naijua kabla ya kusoma UNCTAD wala document yoyote. Ndiyo maana nimeweka allowance for redaction of documents (siyo "reduction" kama ulivyonisoma wewe, which is something else) kwa hiyo unless una kitu kingine hujaniambia kipya kwa issue ya confidentiality.

Mkataba unaweza kuwekwa online na sehemu zilizo sensitive for business reasons una redact.

Wananchi wa Mtwara wana haki ya kujua kama serikali ina stipulate wawekezaji wa invest katika huduma za jamii kwa kiwango fulani kwa watu wa Mtwara huko.This is a standard practice, sasa ukiweka hilo wazi katika mkataba na ku redact sensitive figures kuhusu minutiate royalties detail ukampa mkuu wa upinzani na institutions nyingine on a need to know basis, tatizo liko wapi?

Tatizo langu ni pale mnaposema kuna issue ya confidentiality kwa hiyo mkataba mzima hauwezi kuwekwa wazi, watu wasijue hata muwekezaji ni nani kwa sababu ya confidentiality?

Confidentiality gani kama si wizi huu? Si ndo yale yale ya kuficha wizi wowote kwa guise ya "Usalama wa Taifa"?

Watu wanachukua hela Benki Kuu kwa Deep Green (how comical, deep green as in CCM? campaign money?) halafu wankwambia zimechukuliwa kwa "Usalama wa Taifa".

Ndio upuuzi ambao sitaki.

 
Wawekezaji wanasema ukilazimisha iwekwe wazi wataacha kuwekeza nchini na sisi tutaendelea kuwa maskini....at least that what watawala wetu wanasema.
Nasisi badala ya kuwakabiri watawala kisawasawa tumebaki na mijadala ya nani achinje mnyama, nani ananufaika na mfumo kristo, mtaala wa elimu uko wapi, ccm chama dume.........
 
Tulicheka na kusikitia ujinga wa akina Chief Mangungo wa Msovero lakini naona hawakuwa na tofauti sana na machifu(watawala)wetu wa leo!Ama niseme huenda wao kwa kutojua kusoma wanasameheka,hawa wetu ni vigumu hata kuamini kuwa wanajiuza kwa bei chee sana.
 
Leo naweza ku Google mshahara wa mbunge wa Uingereza, na historia ya mshahara huo. Tanzania siwezi kufanya hivyo.

Unataka kujua mshahara wa mbunge ili iweje?

Mshahara wa mtu ni confidential bana.

Ila kama unataka sana kujua basi nenda idara ya utumishi.

You catch my drift?
 
Nimekuwekea hapa, sheria ya Uingereza inavyosema kuhusu hili swala.

Kwa nini unanipa sheria ya Uingereza? Nchi yenye ma institutions, ma serious crime office, ma sheria yanayobana makampuni ya Kiingereza kutojiingiza katika rushwa nje, ma freedom of information law etc? Wao hata wakisema mikataba isiwe public wana compensating factors kibao ambazo sisi hatuna. Huwezi kutulinganisha.

Au unataka niitumie kama mfano?

Kwa kutumia sheria hii, mikataba yote ya serikali ingekuwa JF tayari. Hata kama ni katika a slightly redacted version.

Kwa sababu hata kama serikali haina website yake yenye mikataba hii in PDF, Invisible angekuwa na haki ya kuandikia email Wizara husika, akajieleza yeye ana forum inayojadili mustakabali wa mikataba ya Tanzania yenye Watanzania wengi, na kisheria wana "right to know" mpaka hapo itakavyokuwa demonstrated otherwise.

Serikali ndio ingekuwa na kazi ya kujenga case kwa nini wananchi wasipewe access kuona mikataba hii.

Si sasa hivi hata mwananchi akijenga a "need to know" basis, atakuwa at the mercy of the government kwa sababu mikataba ni "state secret" na wala si "trade secret" tu. Ukikamatwa unavujisha mikataba unaweza kupewa kesi ya uhaini!

Tunaenda kinyumenyume!
 
Unataka kujua mshahara wa mbunge ili iweje?

Mshahara wa mtu ni confidential bana.

Ila kama unataka sana kujua basi nenda idara ya utumishi.

You catch my drift?

Kipato cha mtu ni confidential, mshahara wa public servant ni public ndo maana kuna nagzi za mshahara serikalini na zinajulikana.

Ndo maana hata Obama mshahara wake watu wanaujua.

Nataka nijue mshahara wa mbunge kwa sababu mimi kama mwananchi mlipakodi ndiye ninayemlipa mshahara. Mbunge ni muajiriwa wangu. Mie ndo muajiri wake.

Sasa kama mbunge ni mfanyakazi wangu na mie ndiye namlipa mshahara kutokana na kodi yangu kwa nini nisijue namlipa kiasi gani ili niweze kuchekecha kwamba kazi anayofanya inastahili mshahara ule, nimuongeze au nimpunguzie??
 

Transparency inasaidia kuzuia kuweka vifungu vibovu. Sio lazima iwe wazi kwa watu wote, lakini kuwe na utaratibu wa watu kuweza kuiona na hasa kabla haijasainiwa, k.m. Na Kamati ya Bunge ya sekta husika na ya sheria.
 
Well hilo ni tatizo sugu kwa sasa at local and national level of our politics, lakini tusiwaangalie wananchi tu wanaoshabikia je wale waliosoma na kuwaingizia hayo mawazo in the first aren't they the main causes ya haya madai unayoyaita ya kipuuzi for the large part.

Maana sio mwananchi alienda kuishitaki serikali hapa ni taasisi yenye hela na huwezo wa kufanya hivyo ndio imechochea moto, kama kweli watu wameweka madai hayo kwenye katiba (including any other divisive demands) uoni wale wajuu ndio tatizo kubwa kuliko hawa wa chini remember people with inadequate knowledge can easily be influenced ndio sababu wengine tunaona kuna umuhimu sana wa viongozi juu kizingatia uzito wa kauli zao.

Like i said ngoja ni pumzike huu umjadala usije enda kivingine.

Ciao
 

Hii thread ushaiona? Ni ya tokea 2007.
 
Wawekezaji wanasema ukilazimisha iwekwe wazi wataacha kuwekeza nchini na sisi tutaendelea kuwa maskini....at least that what watawala wetu wanasema.

Hii ni issue ya kweli kabisa. Na mimi sitaki kuiunderestimate umuhimu wake. Nimeigusia in that piece. In no way am I suggesting a Chavismo/ Morales move on the part of our government, adopting an overly populist stance that would backfire in painting the country with an unnecessarily Marxist brush. Mwishowe wawekezaji wajiulize "tukiwekeza hapa hawa jamaa hawatataifisha kama alivyofanya Nyerere?". Sitaki hilo.

On the other hand, serikali yetu iko passive sana.

Wawekezaji wanataka kuwa kama miungu watu sasa? Wa dictate kila kitu?

Leo nilikuwa nasikiliza BBC kuna kampuni linachimba dhahabu Mali huko. Mali was among the 3 top gold producers in Africa last time I checked, with Ghana, Tanzania and South Africa in that same top 3-4 list. Jamaa wanaulizwa hivi nyie hamuogopi vita mko Mali tu mnachimba dhahabu? Jamaa anajibu anasema mwaka jana tumepata faida sana na tunaendelea kuchimba dhahabu. Watu wanataka biashara. Na as long as hamna demands ambazo si unrealistic (sometimes hata mkiwa na demands unrealistic, if it makes business sense to them) watakubali.

Sasa hapa ndipo unapokuja umuhimu wa ku negotiate details. Of course kama mnawaeleza wawekezaji kwamba "look, nchi yetu ina tatizo la rushwa, tunataka ku balance business interests zetu wote bila ku sacrifice transparency, tutaweka mikataba wazi lakini kuna some sensitive details / figures tuta redact waweze kuona watendaji wenye "need to know" tu". Sidhani kama kuna a legitimate organization itakataa hili.

Wanaweza hata kujitamba kwamba "tunafanya kazi na waafrika wenye a high level of transparency, hivyo hatuna rushwa". This is a selling point even to them in today's world. Hata wao kwao wanaandamwa wasifanye biashara kwa rushwa nje.Ndiyo mamabo ya serious crime office ya UK. Kuna sheria kama hizi pia Marekani.

Ona

US Foreign Corrupt Practices Act


http://en.wikipedia.org/wiki/Foreign_Corrupt_Practices_Act


UK Bribery Act 2010

http://en.wikipedia.org/wiki/Bribery_Act_2010
Kwa hiyo mimi sioni tatizo kama watu watataka kufanya homeworks zao.

Mambo mengi sana yanatokana na uzembe. Watu wanaona ku negotiate na wawekezaji tabu. Ngoja tufanya siri tu mkataba mzima kwa sababu wananchi wakiujua ulivyo mbovu hata bila figures, structure tu ya mkataba, litatimka vumbi.

Sasa kutaka uwazi katika hili kutaingiliaje uhuru wa kibiashara wa muwekezaji?
 
Mr. Kilanga ninakuunga mkono kwa 100%.
 
1.Hiyo iliuwa typo, na mimi nimemaanisha redaction, kwahiyo sidhani kama tunapishana hapo.

2.Hiyo website uliyoitoa inaonesha tender tu huwezi kuona mkataba halisi. Hiyo website ni part to ya compliance ya European Union procument Law ambayo inataka kila chi mwanachama watangaze tenda kwa kutumia e tendering. Hata Tanzania tunayo Tanzania Tenders Portal: Unaweza ukaona tenda zote za tanzania zilizopo na zilizopita. Hata hii tenda ya mafuta ilitangazwa.

3. Mimi ninafanya kazi serekali ya Uingereza na kwa nafasi niliyonayo , ninajua sheria Imesimama wapi. Na kwakifupi mkataba wowote wa kibiashara hauwezi kuwekwa hadharani.

4. Ninarudi tena, hata ukiitoa uingereza, International Law in all forms ( Hard law & Soft Law ) Haitoi mwanya kwa mkataba wa kibiashara kuwekwa hadharani.

5. Nimekueleza, Njia nzuri ni kulipa BUNGE MENO ya kuweza kupitia hii mikataba kabla haijasainiwa inapozidi certain threshould.

6. All your basics questions can be answered if you visit Tanzania Tenders Portal:
 
Ndo yale yale ninayoyasema.

Mshahara wa rais ni siri ya serikali!

Hata kama analipwa dola milioni kumi kwa mwezi hatujui!

Mshahara wa Rais hautakiwi uwe siri. There is no Commercial Interest on that.Na hivi ndio vitu common sence which you can advocate. Hata mshara wangu kwasababu ninafanya kazi serekalini upo Online.
 


Unajua hata Carl Peters naye alikuja kama "mwekezaji".. na lengo lake lilikuwa lile lile ..."faida"...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…