Tatizo lako mkuu unabisha tu makusudi kwakua unaona labda wengine hatujafikia literacy level yako ndio unatunyanyasa kwa points zako lakini moyoni unaelewa kabisa kuna mambo sio ya kubishana. Kwaio hauamini kama duniani kuna ulozi (nguvu za Giza)?
Sent from my CPH2059 using
JamiiForums mobile app
Tatizo lako hujibu maswali.
Nguvu ya giza ni nini na unajuaje hii ni nguvu ya giza si kitu kingine?
Unajuaje kwamba ulozi ni nguvu za giza?
Mfano, kwa mtu anayejua kemia, akawa na gesi anayoweza kupulizia watu wakafa bila yeye kuwagusa, kwa watu wasiojua kemia, wanaopenda kurahisisha mambo na kuyaita "nguvu za giza" kabla ya kuyaelewa, ni rahisi sana kusema hizo ni nguvu za giza. Wakati ni kemia tu hawajaijua.
Babu na bibi zetu waliofariki miaka 200 iliyopita, ukiwarudisha leo ukawaonesha usafiri wa ndege, TV, mawasiliano kwa simu, taa za umeme, magari, wataona uchawi mtupu.
Kumbe ni sayansi inayoelezeka naturally tu.
Sasa, na wewe hivyo unavyoviita nguvu za giza, kama vinatokea kweli, unajuaje ni nguvu za giza kweli na si vitu vinavyoelezeka tu bila nguvu za giza, ila wewe tu huvielewi?
Hujajibu swali hili.