(Quran 48:2 - 3)
2. Bila shaka Tumekupa ushindi ulio
dhahiri,
3. Ili Mwenyezi Mungu Akufunikie
makosa yako (unayosingiziwa) yali-
yotangulia na yajayo, na kukutimizia
neema Yake na kukuongoza katika njia iliyonyooka.
JIBU NI:
Neno (Tumekupa)ni katika nafsi ya kwanza wingi hali ya umilikishi.
Kwa nini wingi?Kwa sababu kuna mmiliki wa ujumbe na muagizwaji kufikisha ujumbe.
Mmiliki ni Mwenyezi Mungu na muagizwaji ni malaika.
Mfano:Mimi ni mmilika wa kampuni ambaye nimeajiri muhasibu katika kampuni yangu.Nimempa jukumu la kutafuta wateja ili wanunue bidhaa.
Ni dhahiri muhasibu katika kufikisha tangazo hili kwa watu atatumia kauli ya "KAMPUNI YETU) na siyo vinginevyo.Maneno kama TUNATOA,TANAWAJALI ,TUMEWASOGEZEA n.k ndiyo atayatumia muhasibu.
Sasa muhasibu katika mfano huu atakuwa ni mshiriki mwenzangu katika kampuni au ni mtumishi wangu?.
Umeweka Quran 9:30 inaysema:
30. Na Mayahudi wanasema: Uzeir
ni mwana wa Mwenyezi Mungu; na
Wakristo wanasema, Masihi ni mwana
wa Mwenyezi Mungu; hayo ni maneno
ya vinywa vyao tu, wanayaiga maneno
ya wale waliokufuru zamani. Mwenyezi
Mungu Awaangamize! Wanageuzwa
namna gani!
Katika Aya hiyo ya Qur'an 9:30,hakuna swali hapo kwa sababu kanuni nimekupa hapo juu katika maelezo ya ya Qur'an 48:2.
Zingatia Qur'an ni kitabu cha university na siyo chekechea.
Sent from my SM-G532F using
JamiiForums mobile app