Chimbuko la vitambi linatoka wizara ya elimu na afya, siyo jeshi la polisi

Chimbuko la vitambi linatoka wizara ya elimu na afya, siyo jeshi la polisi

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Jeshi la Polisi wamekuwa wakinyooshewa vidole juu ya vitambi. Lakini shida inatoka wizara ya elimu na afya. Shida ya vitambi na msururu wa magonjwa yasiyoambukizwa chimbuko lake ni wizara ya elimu kutoa elimu mbovu kwa watu kwenye chakula na wizara ya afya kutotoa mwongozo sahihi.

Tulitegemea kila Mtanzania katika elimu ya msingi ajue anahitaji kutunzaje mwili wake tangu tukiwa watoto wadogo.

Ukisoma ni vitu gani viko kwenye mitaala kuanzia elimu ya msingi na kujiuliza hayo yaliyoandikwa kwenye mitaala yanamsaidiaje Mtanzania kujua:
  1. Ale nini kwa siku na asile nini ili kulinda afya yake?
  2. Afanye nini zaidi ya kula au aepuke nini ili kulinda afya yake?
Hakuna kitu, elimu yetu ni definitions na types basi!

Haya ndiyo kipimo cha kupima ubora wa elimu yetu na unaweza kushangaa maboresho yanakuja na hoja za mtoto aendelee kujifunza upuuzi ule ule ila aongezewe na ushonaji, umeme, ujenzi, useremala. Eti ndiyo maboresho ya elimu.

Hii huwa tunaita the viscous circle of poverty, ambayo kutoka tunahitaji a big push na siyo system ileile kuendelea katika cicle ileile.
 
Hivi mwanajeshi unapata wapi ujasiri wa kuwa na kitambi🙆🙆🙆
 
Vitambi vipo hadi kwa wale jamaa wa mabaka mabaka..Kuna mjeda huku mtaani kwetu ana kitambi unaweza dhani ni mjamzito ukiimuangalia haraka haraka
 
Hivi mwanajeshi unapata wapi ujasiri wa kuwa na kitambi[emoji134][emoji134][emoji134]
Hakuna vita

Ni officer huna majukumu makubwa unaamuru tu

Posho na mishahara

Kitimoto na bia

Moyo umeelea


Kwa nini usitoke kitambi
 
Back
Top Bottom