Chimbuko na Upotofu wa kanisa la Waadventista Wasabato

Ukiachana na hoja ya siku ya kuabudu bado una uhakika ellen white hakinzani na maandiko? Na swali mbona unaapa tena ukimtaja kwa kumuamin kwamba ni nabii wa mungu?
Ndiyo.Sasa wewe ulete ushahidi wapi anapingana na maandiko
 
Mi nilidhani ungetoa maandiko kuonyesha Wasabato wamepotea ila wewe na dini yako ndo mko sahihi kwa mujibu wa Biblia!

Hayo makanisa mawili ya akina Ellen White kabla kidogo ya miaka ya 1844 waulizeni kabla yake walikuwa wanasali wapi? Hayo ndiyo makanisa takataka kabisa! Huyo Ellen G White si ndiye alisema Yesu atakuja ulimwenguni 22 Oktoba 1884. Mbona hakuja sasa na bado tunamsubiri? Je, Yesu hakusema siku ya mwisho wa dunia hakuna anayeijua akiwepo yeye? Bado mnadanganyana na matapeli kama hao? Kweli wajinga ndio waliwao jamani! Dini ya Yesu ilikuwepo karne kwa karne kabla ya hata akina Elllen G White wa miaka ya hivi karibuni ya 1884. Mbona mnajizima data? Hamjui hata hilo? Muulizeeni Ellen White huko aliko kuwa kabla ya 1884 mababu zake na mabibi zake walikuwa wanasali wapi? Na kwa nini Yesu Kristu hakuja hiyo tarehe 22 Oktoba 1884? Huyo alikuwa Kibwetere namba moja ukiacha yule wa Uganda. Endeleeni kupotea hadi mtakapokutana na moto mkali siku ya kiama pamoja na ndugu zenu wale Wasabato masalia waliosema wanaweza kufika Iraq bila passport na matokeo wakabakia kumwaga vinyesi pale Airport!
 
Lete ushahidi unaosema Ellen White alitabiri ujio wa Yesu mwaka 1844.Unamzungumzia Ellen White au William Miller?
 
Kama ni William Miller sema,tumweke pembeni Ellen White
 
Lete ushahidi unaosema Ellen White alitabiri ujio wa Yesu mwaka 1844.Unamzungumzia Ellen White au William Miller?

Siwezi kuleta ushahidi wa takataka kama hizo za akina Ellen G White! Na hao ndiyo walioharibu ustaarabu wa ulimwengu hadi tunaletewa dini za mashoga toka huko kwa akina Ellen White, Marekani! Kwa ujumla hakuna dini inayotokeaMarekani hapa ulimwenguni! Huko ni Sodoma na Gomola!
 
Lete ushahidi unaosema Ellen White alitabiri ujio wa Yesu mwaka 1844.Unamzungumzia Ellen White au William Miller?

Kasome kwenye vitabu vyenu vya utapeli utajua hilo! Hizo ndiyo dini tunaziita ‘wasabato masalia’ kama ya mbu! Takataka kabisa na ndiyo maana hazina hata waumini zaidi ya ‘masalia’.
 

Umeandika vingi ambavyo si sahihi kwa sababu ambazo unazijua mwenyewe, Miller alitabiri kuwa mwaka 1844 Yesu angerejea na waumini wa zama hizo wakaamini,

baada ya kutotokea wengi walikata tamaa ndipo Miaka ya baadae 1863 Ellen G White , James White na Joseph Bates wakaanzisha kanisa La Waadvetista wasabato, sasa ukiniambia lilianzishwa mwaka 1844 nakushangaa umegoogle wapi??

Kwa kifupi huna unachojua zaidi ya copy and paste, ni kweli kutokea kwa walioamini mafundisho ya Miller ndio walikuja kuanzisha Sabato lakini waliweka misingi tofauti na chanzo kikuu ni Biblia

Na hii ni mpaka kesho hata Milele, wasabato wana misingi 28 ya Kanisa na yote inatoka kwenye Biblia.

Wasabato hawaamini kitu kisichotoka kwenye Biblia na ndio maana chochote wanachoamini au kusadiki msingi mkuu ni maandiko matakatifu yaitwayo Biblia.
 
Lete ushahidi unaosema Ellen White alitabiri ujio wa Yesu mwaka 1844.Unamzungumzia Ellen White au William Miller?

Jiulize kabla ya hiyo dini ya wasabato masalia 1844 huyo Ellen G White alikuwa anasali wapi? Ukipata jibu utakurupuka mara moja toka ‘wasabato masalia’. Hakuna mkristo hata mmoja anaikubali hiyo dini! Ndiyo maana tunasali sabato siku ya jumapili na siyo jumamosi! Wapi kwenye biblia imeandikwa kuwa sabato ni jumamosi! Ukinipa jibu nitakutajirisha asubuhi!
 
Ndio maana nasema nyinyi wasabato sio wakristo
Bikira Maria alizikwa wapi?
Huwezi mfananisha na huyo nabiii wenu wa uongo alietabili mwisho wa dunia na akafeli
 
Nawaambieni, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitaijenga kanisa langu; na milango ya Jahannamu haitashinda. Nami nitawapa funguo za Ufalme wa mbinguni ; na chochote utakachofunga duniani kitakuwa cha mbinguni; na chochote utakachofungua duniani, kitafunguliwa mbinguni.
(Mathayo 16: 18-19)
 
Kwa hiyo kwa macho yako hapo umeona kaambiwa awe papa sio?Unajua maana ya papa lakini?Baba mtakatifu.Wapi Yesu anamwambia Petro wewe utakuwa papa wa kwanza?
 
Ndio maana nasema nyinyi wasabato sio wakristo
Bikira Maria alizikwa wapi?
Huwezi mfananisha na huyo nabiii wenu wa uongo alietabili mwisho wa dunia na akafeli
Nimekuambia NIONYESHE ALIPOTABIRI ELLEN KUWA MWISHO WA DUNIA NI MWAKA 1844.Lakini hadi sasa hukutoa!
2-Kama kaburi la Yesu halipo,ndo nini sasa!!Kaburi la Mathayo lipo?Lisipokwepo ndo inakuwaje yan,hebu eleza kidogo hapo
 
Sihitaji kutajirishwa.Ningekuwa nataka utajiri wa namna hiyo leo ningekuwa mchungaji wako,nakuuzia maji ya upako.Au ningekuwa padre wako nakufundisha kuabudu sanamu.Wengi mnajiita wakristo lakini niukristo bandia mlionao.Wasabato(wakristo wa kweli) ni wachache.Tangu Adam,MUNGU hakuwahi kuwa upande wa wengi ndugu yangu.Na hakuna nabii au mtume wa kweli aliyetoa ujumbe wa MUNGU ukapokelewa na watu wengi,no.Wengi wapo upande wa mwovu.Hata Yesu anasema;"ingieni kupitia mlango mwembamba.Maana njian ni nyembamba iendayo uzimani,na wachache huingia humo.Lakini mlango ni mpana na njia ni Pana iendayo upotevuni.Wengi huingia humo(Mathayo 7:14).
Mfano: kwenye gharika waliangamia wengi wakaokolewa watu nane tu,tena wa familia moja.
2-Kwa Rutu waliangamizwa wengi,wakaokolewa watu watatu tu,tena wa familia moja.Hata leo hii,wengi hamtaki kuisikia nuru.Mkiambiwa mnasema mnakashifiwa!
*Ikitokea watunza amri za MUNGU (Wasabato) tukawa wengi kuliko wakatoliki,nitahamia katoliki,maana wachache ndiwo wenye Nuru(kwa mujibu wa Yesu mnazareth).
 
Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii,naye Kristo Yesu ni jiwe kuu la pembeni(Efeso 2:20).Sasa kama imani yako sio ile ya mitume na manabii basi ni wazi uko mbali sana na Yesu ila hujatambua.Mungu akusaidie kuelewa
Nashukuru, pia na wewe Mungu akusaidie
 
Hilo andiko la kuja Yesu 1844 Ellen aposema unalo? Au hadithi tu
 
Hauko serious. Hata wenzio wataona unaangusha kambi kwa kuwela hoja nyepesi.
 
Mtoa maada kwanza jiulize ni kwa nini ulimwengu wa giza umetumia nguvu nyingi sana kuzima sabato lakini wanashindwa na imeendelea kuwepo ni kwa sababu ni ya Mungu hamna mwandamu anaeweza kuzima na kupoteza mipango ya Mungu.

Mungu mwenyewe alisema sabato ni agano la milele na mbinguni watu wote wataenda kuabudu mbele zake kwa hiyo unaweza kuandika maparagrafu mengi lakini unazunguka katika palepale neno litasimama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…