Nchi za magharibi hazijaamini hadi sasa kuwa Urusi imeweza kuhimili vikwazo lukuki vya kiuchumi, kinyume chake nchi za magharibi hususan ulaya magharibi ndizo zilizoumia zaidi. Ilitegemewa kuwa urusi itashindwa kuhimili na hivyo kushindwa kuendesha vita vyake dhidi ya ukraine.
Ki vipi China hawezi kuhimili vikwazo vya magharibi ?Kwa upande mwingine China japo ina uwezo wa kuivamia na kuishinda Taiwan kwa nguvu za kijeshi, lakini haina ubavu wa kuweza kuhimili vikwazo vya kiuchumi toka nchi za magharibi kama urusi ilivyoweza. Ndiyo maana China haina ubavu hata kidogo wa kuweza kuivamia Taiwan. Itabaki kupiga kelele tu na vitisho vya mazoezi ya kijeshi kuizunguka Taiwan. Mabeberu wa nchi za magharibi wanajua china hana ubavu huo wala hawezi kufanya yale ambayo urusi inafanya leo!!
Sio kweli, uchumi wa China hautegemei hicho kitu pekee. Ni vizuri unge jifunza kwanza kuhusu uchumi wao.1. Uchumi wa China unategemea uuzaji wa bidhaa za viwandani na soko lao kubwa ni nchi za ulaya na marekani. Kwa bahati mbaya hizi bidhaa si bidhaa za lazima kiasi kwamba nchi zikigoma kununua zitaathirika, lakini pia kuna bidhaa mbadala toka mataifa mengine.
Kama ingelikuwa gas na mafuta ya RUSSIA niya lazima kuyapata kutoka kwake asinge weka bei nafuu kwa nchi marafiki ili wanunue kwake.Hii ni tofauti kabisa na Urusi ambayo yenyewe huuza bidhaa ambazo ni za lazima katika maisha na bidhaa ambazo haziwezi kukosa soko duniani yaani mafuta na gesi!! Ukikataa kununua kwanza lazima uumie na utalazimika kuzitafuta kwa gharama zaidi! Mfano, Poland ilikataa kununua gesi ya urusi kwa sharti la kulipa kwa ruble. Lakini Poland ililazimika kununua gesi hiyo hiyo ya urusi kupitia kwa Ujerumani na kwa bei ya juu zaidi!! Hivi sasa nchi za ulaya wanalazimika kununua gesi kimiminika toka marekani ambayo kwanza haitoshelezi lakini pia ni gharama mara nne zaidi, wakati urusi inauza gesi kwa masoko mengine ya china na India.
China ndio taifa kubwa duniani lenye viwanda vingi ndani ya ardhi yake kwa hiyo sio kweli kuwa viwanda vingi vya China vipo Ulaya na Marekani.2. China inategemea pia viwanda vyake ambavyo vingi vipo huko huko marekani na ulaya! Viwanda hivyo vikipigwa marufuku China haina ubavu wa kuzalisha bidhaa nyingi kuweza kutosheleza masoko yake hata nje ya ulaya na marekani.
Sio kweli, China ni taifa nambari moja katika sekta ya kilimo duniani.3. China haijitoshelezi kwa vyakula na bado hadi leo inategemea kuagiza vyakula toka mataifa mengine hasa marekani na ulaya. Wakinyimwa chakula na kwa vile ni wengi hawawezi kustahimili. Tofauti na Urusi inayojitosheleza kwa vyakula na sehemu kubwa kuuza nchi za nje.
Ulifuatilia ripoti ya CIA kuhusu swala la Taiwan na China ?Kwa kadri siku zinavyosonga mbele ndivyo uwezo wa China kuishinda Taiwan kijeshi unavyozidi kupungua maana Taiwan itauziwa silaha za maangamizi na za kujilinda!!
Ipo mikononi kwa U.S ki vipi ?Tuliwahi kusema humu, nguvu ya uchumi wa China ipo mikononi mwa US ila tukapuuzwa.
China wana tofautiana na U.S pakubwa sana kiuchumi, kisiasa hata kijamii.US amejaribu kufanya kila taifa likifungamana na yeye basi liwe na nguvu kubwa kiuchumi. Na hiki amefanikiwa mno, China alipofika hawezi kutembea tofauti na US anavyotaka.
Kuongezeka maradufu ushirikiano kiuchumi kati ya China na Russia.Ukitaka kuamini hili, JIULIZE CHINA AMEMSAIDIA VIPI SWAHIBA WAKE WA MUDA MREFU RUSSIA KTK VITA HII?
China alitoa msaada wa kibinadamu ambao hata Russia amekuwa akitoa huko huko Ukraine.Mwezi March 2022 China alitoa msaada kwa serikali ya Ukraine kukabiliana na Russia. Mchina ameshajua utamu wa pesa, hana muda tena na upuuzi wa ubabe wa kijeshi, hilo amemuachia Russia.
China hawazi vita anawaza uchumi, kupigana waachie hayawani
Mkuu una shamba ukalime tuu . Maana wadanganyika tukishakuwa na mahindi na maharangwe ma mbogamboga basiSijui umetumia data gani kutokumpa China heshima yake kwenye swala la uchumi wa dunia ya Leo ivi upo sawa kweli kichwani.
Russia hajatetereka sana na vikwazo kwanza sababu kuna nchi nyingi zimekataa kushiriki kwenye vikwazo vilivyoweka na nchi za magharibi nchi nyingi zimekataa kuumiza wananchi na chumi zao kuanzia nchi za OPEC zilikataa kuongeza uzalishaji wa mafuta hii ikampa access ya uhitaji wa mafuta ya Russia sokoni, kumbuka Russia alikuwa namba mbili au tatu wa export wa mafuta ghafi duniani baada ya saudia Arabia na USA kumtoa msambazaji na mzalishaji mkubwa kama uyuu si jambo dogo kama wengi wanavyodhani ndyo maana ukaona mafuta yakapandaa kuliko kawaidaa,
China na India zimekuwa backup kubwa kwake kumbuka izi ni nchi zenye eneo kubwa na watu wengi na uchumi wao ni mkubwa sana kupata punguzo LA ununuzi wa mafuta imekuwa jambo kubwa kwao has a kipindi ambacho mafuta yalipandaa hadi dola 180 kwa pipa moja Ila wao walikuwa wanalipata kwa dola75 hadi 90 hali hii imefanya azidi kujipatia mapato yasiyokuwa na ugumu kuendesha vita na kugharamia huduma nyingine .
Nchi za magharibu bado zinanunua mafuta mbolea gesi kwa wingi kutoka Russia kuliko nchi nyingine duniani ivyo kupunguzaa ukali wa vikwazo kwa russia.
Tukija kwa China dunia ikitaka ipate maumivu makubwa ambayo yatapelekea mdororo wa kiuchumia kwa nchi nyingi ni kuwekewa vikwazo vya kiuchumi kwa china kama alivyopewa Russia dunia haitakaa salama ata kidogo nchi nyingi zitapitia mdororo wa kiuchumi na si kidogo
Kwanza China ndyo exporter mkubwa wa bidhaa zote za viwandanj duniani anachukua zaidi ya asilimia 20% duniani India,Vietnam ni ngumu kucover ili gepu kuwekewa vikwazo kwa nchi kama hiii aisee hali ya maisha itakuwa ngumu kuliko hii ya vita ya Russia.
China ni mkopeshaji mkubwa duniani nyuma ya USA kuwekewa vikwazo kuna hatari kubwa kwenye uchumi wa dunia kibajeti kwa nchi nyingi, miradii kusimama, makampuni kufilisika, kuongezeka kwa ukosefu wa ajira mwisho ni watu kuingia barabarani kuwatoa viongozi wao ivi vyote vitapata nchi nyingi sana ayo ni machche katika mengi usiichukulie China kama Russia ni ngumu sana kuitenga China na uchumi wa dunia ngumu sana usiisi Marekani alishindwa kuzuia bidhaa za China kuingia kwake ila madhara ni makubwa kuliko faidaa inflation ambayo wangeipata hangekaa wasahau
Wewe ndio mjingaWe ni mjinga sana uchumi wa china ni almost trillion 18 ya GDP unafananisha na Russia ambao hata trillion 2 ya GDP haijafika ujinga ni tatizo kubwa sana Tanzania
Maajabu ni Russia kaweka majimbo matano kibindoni Ila bado anayapigania Hana uthibiti nayo hayo ndo maajabu
Yote unayoyajua kuhusu wao ni kwa sababu wao wameamua kukujuza ,wasiyotaka uyajue hutokuja kuyajua had mda mwafaka wakaoamua wao kuyaweka wazi,Unachosema ni sahihi kabisa!
Mara nyingi, vyombo vya habari vya nchi za magharibi vimekuwa na uwezo na ujasiri wa kukosoa ama kutangaza masuala hasi kuhusu serikali za nchi zao kitu ambacho ni tofauti kabisa na media za upande mwingine (Urusi, China, Korea Kaskazini n.k.).
Tusiyoyajua yanajulikana kwa sababu ya uwepo wa sheria na taasisi imara zenye kulinda sheria hizo, ambazo zimepiganiwa na wananchi wenyewe kwa muda mrefu sana katika historia.Yote unayoyajua kuhusu wao ni kwa sababu wao wameamua kukujuza ,wasiyotaka uyajue hutokuja kuyajua had mda mwafaka wakaoamua wao kuyaweka wazi,
Hakuna uhuru kama uzaniavo
Hiyo GDP husaidiwa na Uuzaji na Ununuaji nje ya nchi.We ni mjinga sana uchumi wa china ni almost trillion 18 ya GDP unafananisha na Russia ambao hata trillion 2 ya GDP haijafika ujinga ni tatizo kubwa sana Tanzania
Maajabu ni Russia kaweka majimbo matano kibindoni Ila bado anayapigania Hana uthibiti nayo hayo ndo maajabu
Mbona wameanza fokeana, aviation sector inakufa Putin kamuwakia DeputTukiweka ushabiki pembeni,
Ukweli ni kwamba tunajua majanga ya nchi za magharibi kwa sababu ya uhuru wa vyombo vya habari uliopo.
Kama urusi nayo ingekuwa na uhuru kama huo, pengine kuna majanga ya kutisha ndani ya Urusi.
vyombo kawa rt, tass na sputnic huwa hawatoi habari zozote mbaya ndani ya urusi.
Malekani hawezi kumuwekea vikwazo china kama URUSI.Nchi za magharibi hazijaamini hadi sasa kuwa Urusi imeweza kuhimili vikwazo lukuki vya kiuchumi, kinyume chake nchi za magharibi hususan ulaya magharibi ndizo zilizoumia zaidi. Ilitegemewa kuwa urusi itashindwa kuhimili na hivyo kushindwa kuendesha vita vyake dhidi ya ukraine.
Kwa upande mwingine China japo ina uwezo wa kuivamia na kuishinda Taiwan kwa nguvu za kijeshi, lakini haina ubavu wa kuweza kuhimili vikwazo vya kiuchumi toka nchi za magharibi kama urusi ilivyoweza. Ndiyo maana China haina ubavu hata kidogo wa kuweza kuivamia Taiwan. Itabaki kupiga kelele tu na vitisho vya mazoezi ya kijeshi kuizunguka Taiwan. Mabeberu wa nchi za magharibi wanajua china hana ubavu huo wala hawezi kufanya yale ambayo urusi inafanya leo!!
Sababu kuu kwa nini China haiwezi kuhimili vikwazo vya kiuchumi vya mabeberu:
1. Uchumi wa China unategemea uuzaji wa bidhaa za viwandani na soko lao kubwa ni nchi za ulaya na marekani. Kwa bahati mbaya hizi bidhaa si bidhaa za lazima kiasi kwamba nchi zikigoma kununua zitaathirika, lakini pia kuna bidhaa mbadala toka mataifa mengine.
Hii ni tofauti kabisa na Urusi ambayo yenyewe huuza bidhaa ambazo ni za lazima katika maisha na bidhaa ambazo haziwezi kukosa soko duniani yaani mafuta na gesi!! Ukikataa kununua kwanza lazima uumie na utalazimika kuzitafuta kwa gharama zaidi! Mfano, Poland ilikataa kununua gesi ya urusi kwa sharti la kulipa kwa ruble. Lakini Poland ililazimika kununua gesi hiyo hiyo ya urusi kupitia kwa Ujerumani na kwa bei ya juu zaidi!! Hivi sasa nchi za ulaya wanalazimika kununua gesi kimiminika toka marekani ambayo kwanza haitoshelezi lakini pia ni gharama mara nne zaidi, wakati urusi inauza gesi kwa masoko mengine ya china na India.
2. China inategemea pia viwanda vyake ambavyo vingi vipo huko huko marekani na ulaya! Viwanda hivyo vikipigwa marufuku China haina ubavu wa kuzalisha bidhaa nyingi kuweza kutosheleza masoko yake hata nje ya ulaya na marekani.
3. China haijitoshelezi kwa vyakula na bado hadi leo inategemea kuagiza vyakula toka mataifa mengine hasa marekani na ulaya. Wakinyimwa chakula na kwa vile ni wengi hawawezi kustahimili. Tofauti na Urusi inayojitosheleza kwa vyakula na sehemu kubwa kuuza nchi za nje.
Kwa kadri siku zinavyosonga mbele ndivyo uwezo wa China kuishinda Taiwan kijeshi unavyozidi kupungua maana Taiwan itauziwa silaha za maangamizi na za kujilinda!!
Kama ilivyo kwa Urusi kama ingechelewa zaidi kuivamia ukraine, ingekuta ukraine imejiimarisha zaidi kijeshi.
China inatia huruma lakini haina jinsi zaidi ya kulalamika!! Lakini ni afadhali kutokuthubutu kuliko kuthubutu halafu ukafilisika!!
Kwa Urusi tunavyozungumza, keshaweka kibindoni tayari majimbo matano ikiwemo Crimea na Ukraine hana jinsi zaidi ya kulia lia kwa mabeberu kuomba misaada ya fedha na silaha!! China ubavu huo hana vinginevyo itaaibika!!