Nchi za magharibi hazijaamini hadi sasa kuwa Urusi imeweza kuhimili vikwazo lukuki vya kiuchumi, kinyume chake nchi za magharibi hususan ulaya magharibi ndizo zilizoumia zaidi. Ilitegemewa kuwa urusi itashindwa kuhimili na hivyo kushindwa kuendesha vita vyake dhidi ya ukraine.
Sio kweli, kwamba vikwazo havija athiri uchumi wa Russia utofauti ni kuwa uchumi wa Russia umeathirika tofauti na mataifa ya magharibi yalivyo tarajia lakini Russia ana safari ndefu sana ya kuendelea kushindana na hivyo vikwazo hata pale operation yake ya kijeshi itakapo tamatika hapo UKRAINE.
Jambo jingine unalo paswa kufahamu ni kuwa taifa la RUSSIA lime saidiwa kuvikabili vikwazo vya magharibi kwa kiwango kikubwa na maswahiba wake wakubwa wawili China & India, hasa hasa China maana China na RUSSIA uhusiano wao kiuchumi umekua maradufu wakati huu kuliko wakati wowote huko nyuma kabla ya OP.
Pia unapaswa kufahamu ni kwa nini RUSSIA mpaka sasa bado ana endelea kuhimili vikwazo alivyo wekewa na magharibi na uhusiano wake na China na India kwa sasa hasa hasa China ?
Kwa upande mwingine China japo ina uwezo wa kuivamia na kuishinda Taiwan kwa nguvu za kijeshi, lakini haina ubavu wa kuweza kuhimili vikwazo vya kiuchumi toka nchi za magharibi kama urusi ilivyoweza. Ndiyo maana China haina ubavu hata kidogo wa kuweza kuivamia Taiwan. Itabaki kupiga kelele tu na vitisho vya mazoezi ya kijeshi kuizunguka Taiwan. Mabeberu wa nchi za magharibi wanajua china hana ubavu huo wala hawezi kufanya yale ambayo urusi inafanya leo!!
Ki vipi China hawezi kuhimili vikwazo vya magharibi ?
Ulifuatilia trade war 2018 Kati ya U.S.A na China ?
1. Uchumi wa China unategemea uuzaji wa bidhaa za viwandani na soko lao kubwa ni nchi za ulaya na marekani. Kwa bahati mbaya hizi bidhaa si bidhaa za lazima kiasi kwamba nchi zikigoma kununua zitaathirika, lakini pia kuna bidhaa mbadala toka mataifa mengine.
Sio kweli, uchumi wa China hautegemei hicho kitu pekee. Ni vizuri unge jifunza kwanza kuhusu uchumi wao.
Hii ni tofauti kabisa na Urusi ambayo yenyewe huuza bidhaa ambazo ni za lazima katika maisha na bidhaa ambazo haziwezi kukosa soko duniani yaani mafuta na gesi!! Ukikataa kununua kwanza lazima uumie na utalazimika kuzitafuta kwa gharama zaidi! Mfano, Poland ilikataa kununua gesi ya urusi kwa sharti la kulipa kwa ruble. Lakini Poland ililazimika kununua gesi hiyo hiyo ya urusi kupitia kwa Ujerumani na kwa bei ya juu zaidi!! Hivi sasa nchi za ulaya wanalazimika kununua gesi kimiminika toka marekani ambayo kwanza haitoshelezi lakini pia ni gharama mara nne zaidi, wakati urusi inauza gesi kwa masoko mengine ya china na India.
Kama ingelikuwa gas na mafuta ya RUSSIA niya lazima kuyapata kutoka kwake asinge weka bei nafuu kwa nchi marafiki ili wanunue kwake.
China na India ununuzi wao wa mafuta na gas za bwerere kutoka RUSSIA kumemsaidia RUSSIA kwa kiwango kikubwa kupunguza makali ya vikwazo katika swala la nishati isinge kuwa hivyo RUSSIA ange kuwa katika hali mbaya sana katika nishati.
2. China inategemea pia viwanda vyake ambavyo vingi vipo huko huko marekani na ulaya! Viwanda hivyo vikipigwa marufuku China haina ubavu wa kuzalisha bidhaa nyingi kuweza kutosheleza masoko yake hata nje ya ulaya na marekani.
China ndio taifa kubwa duniani lenye viwanda vingi ndani ya ardhi yake kwa hiyo sio kweli kuwa viwanda vingi vya China vipo Ulaya na Marekani.
3. China haijitoshelezi kwa vyakula na bado hadi leo inategemea kuagiza vyakula toka mataifa mengine hasa marekani na ulaya. Wakinyimwa chakula na kwa vile ni wengi hawawezi kustahimili. Tofauti na Urusi inayojitosheleza kwa vyakula na sehemu kubwa kuuza nchi za nje.
Sio kweli, China ni taifa nambari moja katika sekta ya kilimo duniani.
Kwa kadri siku zinavyosonga mbele ndivyo uwezo wa China kuishinda Taiwan kijeshi unavyozidi kupungua maana Taiwan itauziwa silaha za maangamizi na za kujilinda!!
Ulifuatilia ripoti ya CIA kuhusu swala la Taiwan na China ?
Ndugu unapaswa kujifunza vitu kabla ya kuandika maswala ya kiuchumi ni maswala mapana sana. China ni taifa kubwa sana kiuchumi ukitokea mgogoro wowote utakao lihusisha hili taifa dunia ita athirika zaidi hata ya mara kumi inavyo athirika na huu mgogoro wa RUSSIA na UKRAINE.