Hayawi hayawi sasa yamekuwa, Kwa mara ya kwanza Jamhuri ya watu wa China imepitisha uamuzi wa kuondoa kodi (Zero-Tarrif) kwa asilimia 98 ya bidhaa zinazotoka Tanzania kuanzia Mosi Disemba 2022. Msamaha huu kwa bidhaa za Tanzania ni matokeo ya juhudi za Rais Samia katika kukuza diplomasia.
Bidhaa zilizoondolewa ushuru ni pamoja na bidhaa za bahari, Korosho, Parachichi, Karafuu, Kahawa, bidhaa za madini, Tumbaku, bidhaa za ngozi n.k, China ni soko lenye watu zaidi ya bilioni 1.4 ikiongoza Duniani na pia ikiwa na pato ghafi (GDP) linalo kadiriwa kuwa zaidi ya Dola Trilioni 17.
Kwa mujibu wa Takwimu zilizopo, katika kipindi cha Mwezi Octoba 2022 ukilinganisha na kipindi kama hiki mwaka
2021, Tanzania imeendelea kuimarisha uwezo wake wa kuuza bidhaa nje(Export) ambapo kiwango kimeongezeka kutoka Dola Bilioni 9.4 hadi Dola Bilioni 11.6. Kasi hii ni kubwa na inayotoa tumaini kubwa.
Pia, katika maeneo mengine kiuchumi serikali chini ya Rais Samia inaendele kufanya vizuri, mfano katika Mfumuko wa Bei, kiwango kimeendelea kuwa cha 5.4% (Single digit index), ni nchi chache Duniani zenye kiwango hiki.