China imeondoa ushuru kwa bidhaa za Tanzania

China imeondoa ushuru kwa bidhaa za Tanzania

Tujiulize hao wachina wenyewe wanapata nini hawawezi kusamehe Kodi kizembe ndio tuamue kama ni jambo jema au tumepigwa
Acha kua mtu wa kupinga kila kitu wafanyabashara wamefurahi sana kutokana na hii issue ya kusamehewa Rais Samia Suluhu anaendelea kupambana ili kumarisha uchumi wa Tanzania na wananchi
 
Nasisi tufanye ZERO TRAFFIC kwa bidhaa zao pia ili i fuq[emoji2959] both side sio tu wao wazoe KAHAWA NA KOROSHO, NA MAPARACHICHI YETU alafu sisi tusifaidi chochote kutoka kwao
 
Bidhaa zilizondelewa kodi asilimia kubwa wachuuzi wake humu bongo ni kutoka china.

Kifupi wachina wamejitafutia soko uchinani
 
Bidhaa zilizondelewa kodi asilimia kubwa wachuuzi wake humu bongo ni kutoka china.

Kifupi wachina wamejitafutia soko uchinani
Na sisi wabongo wachuuzi za bidhaa za china tumeshindwa kupewa soko kwa bidhaa za china hapa tz kwa kigezo cha kukingia vifua bidhaa/viwanda vya ndani!!!? NANI ANANYONYWA HAPA!!?
 
Alafu kuna lipuuzi huko linakuja kudai Samia asipongezwe
Tutampongeza nae aachie Free port/ zero tariff bidhaa kutoka china, tofauti na hapo atakua kesha tuuza, sisi tutafaidika nini na bidhaa kutoka china kama za kwetu kwao ni free ila za kwao kuja huku ni kulipia!!?
 
Nasisi tufanye ZERO TRAFFIC kwa bidhaa zao pia ili i fuq[emoji2959] both side sio tu wao wazoe KAHAWA NA KOROSHO, NA MAPARACHICHI YETU alafu sisi tusifaidi chochote kutoka kwao
Tanzania tunapokea bidhaa nyingi sana kutoka wewe unataka ufaidikaje mjomba
 
Hii ni offer au kuiweka nchi kwenye vitanzi vizito
Wewe sio mfanya biashara lakini wafanyaiashara wakubwa wanajua faida ya hii kitu kaa kwa kutulia ule mema ya nchi mzee Rais Samia Suluhu anajitahidi kila siku kutuinua kiuchumi
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, Kwa mara ya kwanza Jamhuri ya watu wa China imepitisha uamuzi wa kuondoa kodi (Zero-Tarrif) kwa asilimia 98 ya bidhaa zinazotoka Tanzania kuanzia Mosi Disemba 2022. Msamaha huu kwa bidhaa za Tanzania ni matokeo ya juhudi za Rais Samia katika kukuza diplomasia.

Bidhaa zilizoondolewa ushuru ni pamoja na bidhaa za bahari, Korosho, Parachichi, Karafuu, Kahawa, bidhaa za madini, Tumbaku, bidhaa za ngozi n.k, China ni soko lenye watu zaidi ya bilioni 1.4 ikiongoza Duniani na pia ikiwa na pato ghafi (GDP) linalo kadiriwa kuwa zaidi ya Dola Trilioni 17.

Kwa mujibu wa Takwimu zilizopo, katika kipindi cha Mwezi Octoba 2022 ukilinganisha na kipindi kama hiki mwaka
2021, Tanzania imeendelea kuimarisha uwezo wake wa kuuza bidhaa nje(Export) ambapo kiwango kimeongezeka kutoka Dola Bilioni 9.4 hadi Dola Bilioni 11.6. Kasi hii ni kubwa na inayotoa tumaini kubwa.

Pia, katika maeneo mengine kiuchumi serikali chini ya Rais Samia inaendele kufanya vizuri, mfano katika Mfumuko wa Bei, kiwango kimeendelea kuwa cha 5.4% (Single digit index), ni nchi chache Duniani zenye kiwango hiki.

Na Sisi tumewapa nn ?
Fatilia na Hilo ujue
 
Na Sisi tumewapa nn ?
Fatilia na Hilo ujue
Kila anachofanya Rais Samia Suluhu lazima kilete matokeo chanya lakini kwakua wewe unaangalia in negative way hauwezi kuona lakini sisi wafanyabiashara tunasema Rais Samia Suluhu ametufungulia milango ya kibiashara
 
Tanzania tunapokea bidhaa nyingi sana kutoka wewe unataka ufaidikaje mjomba
Wale wafanyabiashara wa vitenge kimewakuta nini!? Kodi iliyokuwepo na ukilinganisha na wanayotakiwa kulipa sshv unaijua!!? Kama wao wamefanya zero tariffs kwann ss tusifanye hivyo ili na sisi tunufaike
 
Tutampongeza nae aachie Free port/ zero tariff bidhaa kutoka china, tofauti na hapo atakua kesha tuuza, sisi tutafaidika nini na bidhaa kutoka china kama za kwetu kwao ni free ila za kwao kuja huku ni kulipia!!?
Umeongea kitu ambacho haukijui China inauza bidhaa nyingi sana Tanzania ukisema China ilete bidhaa zao for free watakua wanatunyonya sana lakini sisi tunapeleka vitu vichache sana kwaiyo think twice Rais Samia Suluhu anatufungulia milango ya biashara acha kulalamika kwa kitu usichokijua
 
Neocolonialism kweli hatari, sa hii ni taarifa ya kufurahisha kwa mwenye akili kweli? kasome vizuri SAPs then uje uandike upya, kwa kufanya hivyo sisi pia tunatakiwa tufanye the same, mko na viwanda vipi vya kuzalisha bidhaa za kwenda kuuza CHINA kama sio malighafi!???...[emoji706]

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Hizo ni ramli zako tu. Umekaa kupenda habari mbaya tu kwa Tanzania

Back
Top Bottom