China imeondoa ushuru kwa bidhaa za Tanzania

China imeondoa ushuru kwa bidhaa za Tanzania

Kila anachofanya Rais Samia Suluhu lazima kilete matokeo chanya lakini kwakua wewe unaangalia in negative way hauwezi kuona lakini sisi wafanyabiashara tunasema Rais Samia Suluhu ametufungulia milango ya kibiashara

Mchina hafanyi mambo bure bure,

Angalia Kenya angalia Zambia
 
Ukiona hivyo ujue serikali ya tanzania nayo imekubali kuwaachia wahalifu wooooote wa kichina waliokuwa wanashikiliwa kwa makosa mbalimbali waliyofanya humu nchini ikiwemo ujangili....!
Akiwemo na huyu au??
 
Attachments

  • B628E55E-800F-4911-A338-ABC96E174626.jpeg
    B628E55E-800F-4911-A338-ABC96E174626.jpeg
    131.6 KB · Views: 5
Afadhali nianze kuwapelekea mayai ya kware
Naam utawapelekea Kware ila wauza nyanya, vitunguu swaumu, smart phones na all junks huenda wakakosa kuuza chochote kwa kukosa / kushindwa ku-compete kwa soko la ndani kuwa flooded na chinese junk products (cheap) wakati wewe soya yako au kware wako huko Uchina waki-compete na American and all other products world over (na wewe kwa kutumia huu umeme wa Makamba, maji na pumba / chakula cha kuokoteleza, freights za bei ya juu ya Kg n.k. unadhani uta-compete ? Juzi tu hapa wauza mayai walianza kulia lia mayai kutoka Kenya bei rahisi wanashindwa kuuza;

Am all for Fair Trade ingawa kinachotokea duniani sasa Trade is neither Free nor Fair..., Na TBS yetu tunavyoijua tuwe aware tusianze kuletewa hata products mbovu ki-afya

Kumbuka pia kuna Mkataba kama huu na European Unions, to put it mildly ni kama wewe una duka la Mangi jirani yako akafungua supermarket yenye bidhaa za bei ya kutupa kutokana na uwezo wake wa kununua Jumla Jumla.., guess what will happen (unless umuuzia duka lako ageuze car park)
 
B247A294-1B11-4AC6-9722-E31DF642F9C9.jpeg

Sio Tanzania tu iliyoachiwa kupeleka kwa zero, kuna nchi kumi maskini duniani zimepewa hiyo privilege na wanampango wa ku extend hiyo programme kwa nchi zote ambazo ranked very poor.

Halafu awajasamehe kodi na wala uwezi lipa kodi ya bidhaa unayo import popote duniani, well kuna fees ya kuingiza bidhaa hiyo ndio wamesamehe ila ukiuza ndani ya soko la China utalipa kodi kama kawa.

Haya ndio mambo yaliyomkera Dr Bashiru kila kitu mama kafanya ata sera za wengine tunasingizia nguvu.

Nimeona mkuu wa mkoa Kilimanajaro akipokea watalii na kusifia ‘royal tour’, dah.
 
Alafu kuna lipuuzi huko linakuja kudai Samia asipongezwe

Sasa apongezwe wakati anatimiza wajibu wake? Serikali kuepeleka maji sehemu ni wajibu wake , serikali kujenga barabara ni wajibu wake, serikali kujenga shule ni wajibu wake sio hisani, serikali kutoa mbolea ya ruzuku ni wajibu wake, serikali kulinda amani ni wajibu wake sio hisani kwa mwananchi, yaani kazi ya mwananchi ni kulipa kodi, na sio kuisifu kwa mapambio serikali, acheni uchawa wenu
 
Bidhaa zilizondelewa kodi asilimia kubwa wachuuzi wake humu bongo ni kutoka china.

Kifupi wachina wamejitafutia soko uchinani

Mawakala wanaonunua hayo mazao ni wachina wenyewe miaka na miaka, yaani kwa ufupi wanataka wapate bidhaa hizo kirahisi kwa manufaa yao wajinga watakwambia tumsifu rais aliyeenda kufanya udalali wa mazao na sio kuleta wawekezaji wajenge viwanda vijana wa kitanzania wapate ajira hapana yaani wanasikitisha sana hawa nahisi wanadhani kila mmoja ni mjinga kama wao walivo wajinga
 
Hiyo ni ndoano wanaondoa ushuru wa hizo bidhaa hivo na wewe utalazimika kutochaji ushuru kwenye bidhaa hizo pia yaani wanachukua bila kulipa ushuru, halafu wenye mitaji ya kununua ni wao wenyewe na watajipangia bei gani wanunue dunia ya leo unapewa kuuza malighafi unachekelea kosa upambane uexport bidhaa kutoka viwandani kwako ili upate faida kubwa
 
Naam utawapelekea Kware ila wauza nyanya, vitunguu swaumu, smart phones na all junks huenda wakakosa kuuza chochote kwa kukosa / kushindwa ku-compete kwa soko la ndani kuwa flooded na chinese junk products (cheap) wakati wewe soya yako au kware wako huko Uchina waki-compete na American and all other products world over (na wewe kwa kutumia huu umeme wa Makamba, maji na pumba / chakula cha kuokoteleza, freights za bei ya juu ya Kg n.k. unadhani uta-compete ? Juzi tu hapa wauza mayai walianza kulia lia mayai kutoka Kenya bei rahisi wanashindwa kuuza;

Am all for Fair Trade ingawa kinachotokea duniani sasa Trade is neither Free nor Fair..., Na TBS yetu tunavyoijua tuwe aware tusianze kuletewa hata products mbovu ki-afya

Kumbuka pia kuna Mkataba kama huu na European Unions, to put it mildly ni kama wewe una duka la Mangi jirani yako akafungua supermarket yenye bidhaa za bei ya kutupa kutokana na uwezo wake wa kununua Jumla Jumla.., guess what will happen (unless umuuzia duka lako ageuze car park)
Mbona kama umeshashindwa kabla ya kujaribu?
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, Kwa mara ya kwanza Jamhuri ya watu wa China imepitisha uamuzi wa kuondoa kodi (Zero-Tarrif) kwa asilimia 98 ya bidhaa zinazotoka Tanzania kuanzia Mosi Disemba 2022. Msamaha huu kwa bidhaa za Tanzania ni matokeo ya juhudi za Rais Samia katika kukuza diplomasia.

Bidhaa zilizoondolewa ushuru ni pamoja na bidhaa za bahari, Korosho, Parachichi, Karafuu, Kahawa, bidhaa za madini, Tumbaku, bidhaa za ngozi n.k, China ni soko lenye watu zaidi ya bilioni 1.4 ikiongoza Duniani na pia ikiwa na pato ghafi (GDP) linalo kadiriwa kuwa zaidi ya Dola Trilioni 17.

Kwa mujibu wa Takwimu zilizopo, katika kipindi cha Mwezi Octoba 2022 ukilinganisha na kipindi kama hiki mwaka
2021, Tanzania imeendelea kuimarisha uwezo wake wa kuuza bidhaa nje(Export) ambapo kiwango kimeongezeka kutoka Dola Bilioni 9.4 hadi Dola Bilioni 11.6. Kasi hii ni kubwa na inayotoa tumaini kubwa.

Pia, katika maeneo mengine kiuchumi serikali chini ya Rais Samia inaendele kufanya vizuri, mfano katika Mfumuko wa Bei, kiwango kimeendelea kuwa cha 5.4% (Single digit index), ni nchi chache Duniani zenye kiwango hiki.

Undugu wetu uendelee.
 
Hakuna bidhaa tunayozalisha kuingiza kwenye soko la china zaidi ya kusafirisha malighafi kwenda kwenye soko.
Ila kama Nchi yetu ikisamehe ushuru kama China kwenye bidhaa zinazoingia, sisi ndio wenye hasara.
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, Kwa mara ya kwanza Jamhuri ya watu wa China imepitisha uamuzi wa kuondoa kodi (Zero-Tarrif) kwa asilimia 98 ya bidhaa zinazotoka Tanzania kuanzia Mosi Disemba 2022. Msamaha huu kwa bidhaa za Tanzania ni matokeo ya juhudi za Rais Samia katika kukuza diplomasia.

Bidhaa zilizoondolewa ushuru ni pamoja na bidhaa za bahari, Korosho, Parachichi, Karafuu, Kahawa, bidhaa za madini, Tumbaku, bidhaa za ngozi n.k, China ni soko lenye watu zaidi ya bilioni 1.4 ikiongoza Duniani na pia ikiwa na pato ghafi (GDP) linalo kadiriwa kuwa zaidi ya Dola Trilioni 17.

Kwa mujibu wa Takwimu zilizopo, katika kipindi cha Mwezi Octoba 2022 ukilinganisha na kipindi kama hiki mwaka
2021, Tanzania imeendelea kuimarisha uwezo wake wa kuuza bidhaa nje(Export) ambapo kiwango kimeongezeka kutoka Dola Bilioni 9.4 hadi Dola Bilioni 11.6. Kasi hii ni kubwa na inayotoa tumaini kubwa.

Pia, katika maeneo mengine kiuchumi serikali chini ya Rais Samia inaendele kufanya vizuri, mfano katika Mfumuko wa Bei, kiwango kimeendelea kuwa cha 5.4% (Single digit index), ni nchi chache Duniani zenye kiwango hiki.
Harafu utasikia Mama anasafiri sana Hakuna analofanya..

Sio tuu China Bali US imetoa soko la cashnut za Tanzania na zimeanza kuuzwa huko..

Badala ya kulaumu,kulalamika na upuuzi mwingine watu wachangamkie fursa..

Ikumbukwe Miaka 5 iliyopita Hali ya kilimo ilikuwa mbaya na Wakulima wapipata hasara ya karne..

Safi Sana mh.Rais Samia 👇
 
Attachments

  • Screenshot_20221115-145046.png
    Screenshot_20221115-145046.png
    178.3 KB · Views: 3
  • Screenshot_20221113-101839.png
    Screenshot_20221113-101839.png
    111.3 KB · Views: 5
Mbona kama umeshashindwa kabla ya kujaribu?
Kujaribu nini tena ? Naangalia kama nchi na track record ipo vipi...; Sijiangalii mimi kama mimi naangalia mfumo mzima; naangalia watu wote...

Mfano Walmart akifungua supermarket hapo mtaani kwenu in one day wauza mboga mboga sokoni na cornershops zote zitakufa kifo cha kawaida..., Sio mbaya kama wakileta ajira na kununua mazao kwa wakulima ili wauze (ila utaona production chain yao; wenyewe ndio retailers na wholesalers) na kazi za kufagia na ku-stack shelves hazitachukua watu wote...

Sisemi hili lisifanyike nasema huu sio mwarobaini..., mwarobaini ungekuwa kwa hao wauza mbogamboga ku-form cooperatives na ku-add value na kuweza kuuza na sio ndani tu kuuza mpaka nje unless otherwise the future ni scary kuliko hata kipindi cha manamba (hapo mlipewa ujira hata kama ulikuwa ni duni); tunapoelekea kwa one country being the dumping ground of others junk and marginalization of others ni hatari wewe usishangae ukitaka kupeleka product yako Ulaya wakasema ni low quality yao ikaingia na kuuzwa kwa bei ndogo kuliko yako huku (kinachobakia ni wewe kuwapelekea raw materials ili watengeneze alafu wakuletee kwa bei ya juu)

Swali linakuja kwani sisi hatuna matumbo kwanini hizo korosho tusile wenyewe (jibu litakuja buying power) kwahio huenda solution sio rahisi wala one dimensional kama unavyoweza kufikiri...
 
Juhudi za Rais Samia Suluhu maana bila ziara yake tusingepata offer hii
acha upuuzi wewe juhudi gani alizofanya.

Pongezi ziende kwa wananchi wa Tanzania walio katika sekta hiyo huku wakikomaa na kupambana kusukuma uchumi wa nchi.

huyo Rahisi wako kafanya kitu gani?
Alaaaa
 
acha upuuzi wewe juhudi gani alizofanya.

Pongezi ziende kwa wananchi wa Tanzania walio katika sekta hiyo huku wakikomaa na kupambana kusukuma uchumi wa nchi.

huyo Rahisi wako kafanya kitu gani?
Alaaaa
Punguza jazba mzee juhudi ni za Rais Samia Suluhu akishilikiana na wananchi
 
Back
Top Bottom