China imetoa variant nyingine ya J-35 sababu J-35 mpaka leo haipo introduced jeshini. Hakuna squadron yoyote yenye J-35, hivyo bado ni ndege ya majaribio. J-35 imefanya first flight mwaka 2012, J-35A imeruka mwaka jana tu hapo. Bado ipe miaka angalau minne ndio ikubalike jeshini.
Hata stealth J-20 bado haijafikia malengo, bado haijapata stealth engine yake halisi. Mpaka baadae wakifanya modernization ya units kama 200 za J-20 za sasa au watoe variant nyingine yenye stealth engine.
Kuhusu 6th generation fighter, tiyari Marekani inayo NGAD ambayo miezi kadhaa nyuma ilitajwa imefanya test flight ila sasa mashabiki wa China wanalazimisha picha na taarifa zaidi, jambo ambalo Pentagon hawajatoa kwahiyo ushahidi hamna. B-21 Raider ilienda kimyakimya mpaka mwaka jana ikaonekana. Na ni 6th generation bomber ya kwanza duniani.
NGAD imesimama, sio kwamba imesitishwa watu wasijidanganye.
Hiyo LHD yenye EMALS ni maendeleo mazuri kwa Wachina. Hawajawahi kuwa na carrier yenye EMALS, Marekani Ford class ina EMALS mwaka 9 sasa kutoka kampuni ya General Atomics.
Pia Marekani hawapendelei meli ndogondogo, hawataki helicopter carriers kama za Waturuki, Wakorea, Wajapan na Wafaransa na sasa Mchina kaja na hii.
Hizo drones zipo nyingi Marekani. MQ-28 Stingray ya Boeing hii itakuwa refuering tanker ya kwanza ambayo ni drone na inatua kwenye carrier
View attachment 3188626
X-47B ya Northrop Grumman watengenezaji wa B-2 na B-21 iko juu hapo. Chini ni MQ-28
View attachment 3188625
Kuhusu AWACS, Marekani hawana drone AWACS na sioni kama inawezekana.
China ndio kwaza wanafanya testing ya AWACS yao ya kwanza, nyingine zote walikuwa wananunua airframes Urusi. US kwenye submarine hunting, AWACS na reconn wako vizuri.
Pia Marekani ina total displacement kubwa kuliko China. Ila China ina meli nyingi kuliko Marekani, maana yake China ina meli ndogo nyingi. Alafu Marekani ina presence kila bahari kuu duniani kasoro kusini mwa Afrika.