China imeufunga huu mwaka kwa kishindo kikubwa imekuwa nightmare kwa watengeneza silaha wa Marekani na dalali wao Pentagon

Kama walishafanya official unveils kwenye Zhuhai airshow ni suala la muda tu kuingizwa rasmi jeshini

J-35A kwa ajili ya PLAAF (Air force) na J-35 kwa ajili ya PLAN (Navy)

Hata J-20 iliingia baadaye baada ya muda ni kawaida kwa China kufanya hivyo

Ila huwa wanaanza kutoa details matumizi yake mapema
 
Marekani hajawahi kufanya test flight ya 6th Gen tuletee ushahidi wa picha au video, kwanza mpango wenyewe wa NGAD uko paused sidhani kama wameresume
Wakati SR-71 Blackbird inakuwa launched kulikuwa na ushahidi hata wa jina tu la ndege, achana na picha?

Siku F-117 Nighthawk inakuwa launched jeshini, kabla ya hapo kulikuwepo ushahidi wa picha? Hadi jina waliipa F- wakati ilitakiwa iwe B-.

U-2 Dragonlady ilianza kuruka 1955, hata raia wa Wamarekani wenyewe walikuja kujua kuna ndege kama hiyo mwaka 1960 ambapo Warusi walijua.

Marekani ina testing ground, jangwani uko. Hakuna photographer wala ndege zao hawazipitishi kwenye makazi ya watu wakiwa wanafanya testing. Ndege zote za Marekani huwa zinaonekana kwenye matukio maalum yaliyopangwa. Sio kama Wachina watu wapo wanakunywa supu, wanaona ndege angani wanapiga picha.
 

SinoTech at its best
 

Kumchukulia poa mChina kumemgharimu sana mMarekani
 
Marekani haina airshow, military parade wala weapons expo. Ndio maana huwezi ona silaha zake zimepangwa zipigwe picha.

J-35 ni jibu la F-35C na B ambazo zimeruka miaka zaidi ya 10 nyuma.
J-20 ambayo bado haijakamilika ni jibu la F-35 ambayo ni matured kwa miaka zaidi ya 10.
 
Wakumbushe US hawezi kutangaza mambo yake. Akili nyingi
 
Hiyo LHD yenye EMALS ni maendeleo mazuri kwa Wachina. Hawajawahi kuwa na carrier yenye EMALS, Marekani Ford class ina EMALS mwaka 9 sasa kutoka kampuni ya General Atomics.
Tunazungunzia Amphibious assault ships sio carriers.

Amphibious za Marekani hazina catapult wala well deck hazina uwezo wa kubeba dozens of fixed wing aircraft na drones

Mchina hajaanza kuwa na EMALS kwenye hii type 076 alianza tangu kwenye Fujian carrier hii ni mara ya pili kutumia EMALS
 
J-20 haijakamilika nini? No J-35 ni jibu kwa F-35A
 
Mkuu usisahau Marekani waishafanya majaribio ya 6th generation fighter jets September 2020.

Marekani hua hawana matangazo sana kwenye mambo yao.

Wao wana kitu kinaitwa Next Generation Air Dorminance (NGAD) NGAD will include attributes such as enhanced lethality and the ability to survive, persist, interoperate, and adapt in the air domain, all within highly contested operational environments. No one does this better than the U.S. Air Force, but we will lose that edge if we don't move forward now," Kendall said.

Marekani anatumia 3.6% ya bajeti kwenye ulinzi, kumbuka Marekani analinda Dunia nzima😂. Kambi za kijeshi kila kona ya Duniani hadi angani (Us Space Force).

China anajitahidi ila bado ana vitu vingi vya kujifunza kutoka kwa bwana mkubwa.

Ile ya Bwana Elon ya kudaka rocket angani ikiwa inatembea kilomita 27,500 kwa saa ama mile 17,000 kwa saa China wataiweza lini?
 
China huwa hafanyi research, ukiona katoa kitu ujue ameshaona mchoro mahala. Yeye matoleo yake ukiyafuatilia utagundua kwa Euro na US ni ngazi ya research, tena hata hawajafika hatua ya kuomba vibali vya majaribio.
Anapenda kuwa wa kwanza ku release halafu sokoni havidumu hata wiki mbili.
Silaha zake nyingi hata hezibollah waliona hazifai, wakaona ni bora hata ya kombeeo na manati
 
Okay sikukumbuka kama Fujian pia inayo EMALS, basi sasa China inazo meli mbili zenye EMALS tech ambayo waliyozindua 2 years ago.

Marekani inazo meli 4 zenye EMALS tech aliyozindua miaka 9 nyuma.

Amphibious ships za Marekani hazilazimiki kuwa na EMALS sababu F-35B ni STOVL, then nyinginezo ni helicopters.
China hawana STOVL aircraft hivyo lazima wakurupuke kuzinasa ndege zisidumbukie majini maana hii sio carrier. Current assault ship ya Marekani ni America class na inaweza beba ndege 20 hadi 25 kulingana na mixture ya F-35B na naval helicopters kama King Stallion (ambayo Wachina hata wauze, hawawezi kuwa na helicopter kama hii).

America class ikiwa na ndege, nyingine ziko ndani kwenye deck
 
J-20 kaifanyia first flight 2012 hadi leo haina injini yake😂

Sasa hawa wameona ndege mara ya kwanza leo washaanza kushangilia, watasubiri hadi 2030s uko. Wakati Marekani tests zake ni majangwani uko Area 51 na Arizona.
 
Hii bado ni ndogo hata kwa toleo la China lililopita la type 075, za China zina uwezo wa kubeba zaidi ya hii na ni modern za Marekani hazijadizainiwa kubeba drones
 
J-20 kaifanyia first flight 2012 hadi leo haina injini yake😂

Sasa hawa wameona ndege mara ya kwanza leo washaanza kushangilia, watasubiri hadi 2030s uko. Wakati Marekani tests zake ni majangwani uko Area 51 na Arizona.
Unawadanganya wasiojua J-20 inatumia WS-15 engine zinazotengenezwa na Shenyang kampuni ya China

F-35 mpaka leo engine zina hitilafu na hakuna marekebisho ya engine yamefanywa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…