China inabadilisha ukiritimba wa soko la magari barani Afrika

China inabadilisha ukiritimba wa soko la magari barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG31N1239957919.jpg


Chombo maarufu cha habari kuhusu nishati mpya Cleantechnica hivi karibuni kilisema “sekta ya magari ya umeme ya China inayoendelea kwa kasi inaleta athari kubwa kwa Afrika na kukuza mageuzi ya nishati ya kijani."

Jijini Nairobi, Kenya, ukienda kwenye uwanja wa ndege, huenda unaweza kutumia usafiri wa basi la chapa ya BYD ya China; nchini Ethiopia, magari mapya ya umeme yanayotengenezwa nchini China yanazidi kupendwa katika soko la magari; nchini Rwanda, Kampuni ya Go Kabisa imeingiza kwenye soko gari la chapa ya China Geely aina ya SUV, na kuwaletea watumiaji chaguo la gharama nafuu; na nchini Ghana, makampuni mbalimbali yanatoa zaidi ya magari 20 ya umeme yaliyotengenezwa na China sokoni. Je, kwa nini magari ya umeme ya China yanazidi kupokelewa na wateja barani Afrika?

Jibu ni kwamba, nchi nyingi za Afrika zimetunga na kutekeleza mipango inayohusiana na magari ya umeme, na kuhimiza makampuni na watu binafsi kuendesha magari ya umeme, ikiwa ni kitendo cha kuchangia kupunguza utoaji wa gesi ya kaboni. Hali halisi ni kuwa, Afrika ina mazingira fulani ya asili ya kuendesha sekta ya magari ya umeme, kwa mfano, bei za umeme katika baadhi ya nchi za Afrika kama vile Ethiopia ni za chini, na hivyo kutoa mazingira kwa ajili ya maendeleo ya magari ya umeme.

Wakati huo huo, Afrika ina maliasili nyingi muhimu katika uzalishaji wa betri na vipengele muhimu vya magari ya umeme. Kwa mfano, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC ni mojawapo ya nchi zenye utajiri wa cobalt duniani, na Afrika pia ina kiasi kikubwa cha lithiamu, nikeli na rasilimali nyingine za madini.

Lakini kwa nini nchi za Afrika zinapendelea magari ya umeme ya China kuliko yale ya nchi nyingine? Moja ya sababu muhimu ni kwamba ushirikiano kati ya China na Afrika katika nyanja ya nishati mpya kwa miaka mingi umeweka msingi muhimu kwa magari ya umeme ya China kufungua soko la Afrika. China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 15 mfululizo na imefadhili miradi mikubwa ya miundombinu, ikiwa ni pamoja na miradi mingi ya nishati mpya.

Hivi karibuni shirika la habari la Reuters lilinukuu ripoti ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Boston nchini Marekani na kueleza kuwa "China ina fursa ya kipekee ya kuchangia mapinduzi ya nishati barani Afrika." Aidha, katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na uungaji mkono mkubwa wa serikali ya China, nchi hiyo imeongoza dunia katika sekta ya magari ya umeme. Takwimu zinaonyesha kuwa magari ya China yaliyouzwa nje ya nchi yalifikia milioni 4.91 mwaka 2023, likiwa ni ongezeko la 57.9% kuliko mwaka uliotangulia, na kuongoza duniani, ambapo mauzo ya magari ya umeme yalikuwa milioni 1.2, likiwa ni ongezeko la 77.6%.

Kwa hivyo wakati magari ya umeme yanayotengenezwa nchini China yakiendelea kupata umaarufu katika nchi za Afrika, tatizo la ukiritimba wa soko la magari la Afrika linaweza pia kutatuliwa. Kama Mubeswane Masilo, mtafiti wa heshima katika Kituo cha Utafiti wa Kukosekana kwa Usawa kwa Nchi za Kusini katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand nchini Afrika Kusini, alivyosema: "Kwa sababu magari ya China ni ya bei nafuu na yenye ubora kuliko chapa za Japan na nchi za magharibi, magari ya China yatapata fursa ya kuchukua hadhi ya kuongoza.”
 
Back
Top Bottom