Kwa muda sasa, China imekuwa ikiendeleza nguvu mpya bora za uzalishaji na kuvutia vyombo vya habari vya nchi nyingi za Afrika. Nguvu mpya bora za uzalishaji zinamaanisha uzalishaji wa kisasa unaoongozwa na ubunifu, ukiepuka njia za jadi za ukuaji wa uchumi, na wenye sifa za teknolojia ya juu, ufanisi wa juu, na ubora wa juu. Wataalamu na wasomi wengi wa Afrika wameelezea maoni yao kwamba, katika miaka ya hivi karibuni, hatua ya China kuendeleza nguvu mpya bora za uzalishaji inalingana na mikakati ya maendeleo ya Afrika, na iwapo pande zote mbili zitaweza kuimarisha ushirikiano wa ubunifu katika nyanja husika katika siku zijazo, itakuwa na umuhimu mkubwa katika kukuza ukuaji wa uchumi wa Afrika na kuleta maendeleo endelevu na fursa kwa Afrika.
Tovuti ya habari ya "Independent Online" ya Afrika Kusini hivi karibuni ilitoa ripoti kuhusu nguvu mpya bora ya uzalishaji ikisema, "China kuendeleza nguvu bora mpya ya uzalishaji kutaendelea kupanua uhusiano kati ya China na Afrika, na kuimarisha matokeo ya ushirikiano yaliyopatikana kati ya pande hizo mbili. Afrika inayozidi kuwa ya ubunifu inaweza kuchukua fursa mpya, na kuboresha uchumi." Ripoti ya gazeti la "Vanguard" la Nigeria iliyonukuu uchambuzi inaeleza kuwa, China kuendeleza nguvu bora mpya ya uzalishaji hakumaanishi kupuuza au kuacha viwanda vya jadi, bali ni kuhimiza viwanda vya jadi kubadilika kuelekea kuwa vya hali ya juu, vya kisasa na vya kijani. Kwa sasa, China inaendeleza kwa kasi miradi ya ubunifu wa kiteknolojia katika nyanja nyingi, na wataalamu wa Afrika wanatarajiwa kushiriki katika miradi hiyo, kupanua ushirikiano kati ya China na Afrika katika nyanja kama akili bandia, na teknolojia za anga za juu. Tovuti ya "Potential" ya Afrika ya Kati inasema kuwa, China imekuwa injini muhimu ya ukuaji wa uchumi duniani, na maendeleo ya hali ya juu ya China yataendelea kutoa nguvu kwa ajili ya kufufua uchumi wa dunia, na pia italeta fursa mpya kwa maendeleo ya nchi za Afrika.
Sababu kuu inayofanya nguvu mpya bora ya uzalishaji ya China kuvutia sana nchi za Afrika na vyombo vya habari ni kwamba, katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano kati ya China na Afrika katika nyanja mpya umepata matokeo halisi, haswa katika nyanja za uchumi wa kidijitali, maendeleo ya kijani, na kilimo cha kisasa, na Kama gazeti la "The Nation" la Nigeria lilivyosema hivi karibuni kuwa kutokana na msaada wa teknolojia na uvumbuzi kutoka China, njia za uzalishaji na maisha za Afrika zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa. China ni mshirika wa kuwajibika anayesaidia Afrika kukabiliana na changamoto.
Mkutano mpya wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika unatarajiwa kufanyika mwaka huu, na inaaminika kuwa pande zote mbili zitajadili kwa kina ushirikiano katika teknolojia za ubunifu na mafunzo ya vipaji, na kuchunguza njia za kisasa za maendeleo zinazofaa hali halisi za kila upande.