Hivi karibuni, mikoa mingi ya China imetangaza kupandisha kima cha chini cha mshahara kwa mwaka 2021. Kwa mujibu wa kiwango cha sasa, Shanghai inaongoza kwa Yuan 2,480 kwa mwezi, sawa na dola za kimarekani 384. Kadri kima cha chini cha mshahara kinavyopanda, kipato cha wafanyakazi wenye kipato kidogo kinaongezeka. Hii ni hatua nyingine ya China kuongeza hisia ya usalama na uwezo wa kupata ajira kwa watu wenye kipato kidogo.
Kupandisha kima cha chini cha mshahara kinaongeza kipato cha watu wenye kipato kidogo
Baada ya kuondoa umaskini uliokithiri, pengine kuboresha maisha ya watu wanaoishi maisha magumu kiasi na kuongeza kipato chao itakuwa moja ya kazi za kuwasaidia watu maskini za China siku za baadaye. Janga la COVID-19 lililokuja ghafla limeathiri sana kipato cha watu waishio mijini na vijijini hapa China. Na ili kukabiliana nalo, serikali itapandisha kima cha chini cha mshahara, kitendo ambacho sio tu kinalingana na sera ya kupandisha kima hicho kila baada ya muda, bali pia ni kuhakikisha maisha ya watu wenye kipato kidogo, pamoja na kukidhi madai ya wafanyakazi ya kuongezewa mshahara.
Kuendeleza vijiji na kuboresha maisha ya watu wenye kipato cha chini
Waraka wa kwanza uliotolewa na Chama cha Kikomunisti cha China mwaka huu, umesisitiza kuendelea kukuza sehemu za vijiji ambazo tayari zimeondokana na umaskini, na kuwasaidia watu wenye kipato cha chini vijijini. Hali halisi ni kuwa serikali ya China siku zote imehimiza maendeleo yenye uwiano na uhamaji huria wa watu kati ya miji na vijiji, kustawisha vijiji kupitia huduma za kifedha, kuongeza usawa wa huduma za kijamii za kimsingi, kukamilisha usimamizi wa vijiji na kupunguza pengo la maendeleo na kipato kati ya watu wa mijini na vijijini. Teknolojia ya uchumi wa kidigitali imeongeza kwa kiasi kikubwa huduma za jamii za kimsingi, na kutimiza utoaji elimu na huduma za matibabu kwenye mtandao wa internet ili maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanufaishe watu wenye kipato cha chini na cha kati.
Kuimarisha utoaji elimu ya ufundi stadi ili kuongeza uwezo wa watu wenye kipato cha chini kupata ajira
Mapinduzi ya teknolojia ya raundi mpya yamepunguza madai ya ukosefu wa baadhi ya nafasi za ajira kwa uwezo wa ufundi wa wafanyakazi, lakini kwa upande wa pili pia yameongeza pengo la mshahara kati ya aina tofauti za kazi. Kipato cha watu wanaofanya kazi katika mashirika binafsi na wale wanaojiajiri kinaongezeka polepole, na hii ndio sababu ya mshahara wa kundi la watu wenye kipato cha chini kuongezeka polepole kuliko makundi mengine. Ndiyo maana, ni lazima kujenga na kukamilisha utaratibu wa kutoa elimu ya ufundi stadi kwa watu wenye kipato cha chini. Hii si kwa China tu bali hata kwa nchi za Afrika, elimu ya ufundi stadi inaweza kutoa uhai kwa soko la ajira linalokabiliwa na mageuzi ya kiuchumi na kiteknolojia.
Kwa muda mrefu, haswa baada ya kufanyika kwa mkutano wa 18 wa wajumbe wote wa Chama cha Kikomunisti cha China CPC, serikali ya China imejitahidi kutenga fedha, na kuwatambua kwa usahihi na kuwasaidia watu wenye kipato cha chini. Katika miaka mitano ijayo, China itaendelea kuongeza kipato cha watu wenye kipato kidogo, kupunguza pengo kati ya matajiri na maskini, na kufanya ongezeko la kipato cha wakazi kuendana na ongezeko la ukuaji wa uchumi.