China kurejesha raia wake kutoka Sudan kwathibitisha tena nia ya China ya kulinda raia wake vizuri

China kurejesha raia wake kutoka Sudan kwathibitisha tena nia ya China ya kulinda raia wake vizuri

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111434901233.png

Ndege ya kukodi ya China iliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing jumanne tarehe 2, ikibeba abiria zaidi ya 140 wa China waliorejea kutoka nchini Sudan. Kabla ya hapo, manowari za China zilizokuwa zikifanya kazi ya ulinzi katika Ghuba ya Aden zilikwenda Sudan na kuwachukua karibu raia 1,000 wa China, na hadi sasa, karibu raia wote wa China waliokuwa nchini Sudan wameondoka nchini humo. China pia imekuwa nchi iliyorejesha raia wake wengi zaidi kutoka nchini Sudan tangu nchi hiyo ikumbwe na migogoro.

Mwaka jana, kulikuwa na filamu iliyopata umaarufu sana nchini China iitwayo “Safari ya Maelfu ya Maili”. Filamu hiyo iliyotungwa kufuatia matukio ya kweli na kuelezea hadithi ya wanadiplomasia wa China kuwarejesha raia wa China kutoka kwenye nchi fulani ya Afrika ya kaskazini kwa kutumia juhudi zao zote.

Baada ya kutokea kwa mapigano ya ghafla nchini Sudan, serikali ya China ilikuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa raia wake nchini humo. Rais Xi Jinping wa China aliiagiza Wizara ya Mambo ya Nje, kwa kushirikiana na idara mbalimbali, kuongoza ubalozi wa China nchini Sudan kuanzisha haraka mchakato wa kuwaondoa Wachina walioko nchini Sudan, haswa maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mapambano ikiwemo Khartoum. Tarehe 22 mwezi Aprili, ubalozi wa China nchini Sudan na katika nchi nyingine jirani zilitoa taarifa ya dharura ya kuwahamisha Wachina nchini Sudan. Tarehe 26 mwezi huo, Jeshi la Ukombozi la Watu wa China liliagiza manowazri zake za kivita zilizokuwa zikifanya kazi ya ulinzi katika Ghuba ya Aden kwenda Sudan mara moja, ili kuwachukua raia wa China. Kulingana na ripoti, mchakato wa kuwajeresha watu kutoka nchini Sudan ni hatari zaidi kuliko iliyosimuliwa katika filamu. Kaimu wa balozi wa China nchini Sudan Zhang Xianghua, amekuwa akitekeleza majukumu yake akiwa amevaa nguo na kofia nzito zinazoweza kuzuia risasi. Amesema wakati wa kusaidia watu kuondoka, milio ya risasi ilikuwa inasikika mara kwa mara, na ndege za kivita zikirushiana makombora angani.

Hii siyo mara ya kwanza ya China kuwaondoa raia wake kutoka nchi zilizokumbwa na vita. Mwezi Februari mwaka 2011, mapigano makali yalizuka nchini Libya. China ilituma vyombo vya baharini, nchi kavu na anga vikiwemo ndege za abiria, meli za kibiashara, manowari, na mabasi kuwahamisha raia wake zaidi ya 32,000 kutoka Libya hadi sehemu zenye usalama. Mwezi Machi mwaka 2015, wakati vita ilipozuka nchini Yemen, manowari za kijeshi za China zilienda nchini humo kuwaokoa raia 621 wa China na raia 279 wa nchi nyingine 15.

Hatua hizo zimethibitisha kuwa, bila kujali Wachina wako wapi, na wanakabiliwa na hali gani, watapata msaada wa haraka na wenye nguvu kutoka kwa taifa lao. Aidha, hatua hizo pia zimethibitisha tena msimamo wa serikali ya China ya kuzingatia zaidi maslahi ya watu wake.
 
Kulinda na kuokoa raia gani?.. Na wakati selikari yenyewe ya China imeshiriki Kuwaua wachina wengi kwa kukandamiza uhuru wa kuabudu.

China chini ya CCP imetuhumiwa kufanya kwa kusimamia ukatili wa hali ya juu kwa raia wa kichina wasio na hatia walikuwa wana practice Falon Gon kwa kuwafanyia "organ harvesting"

Hundreds of thousands of Falon Gong Chinese have been executed since 1999 na CCP wanalijua hili. Wamekuwa wanavuna organs kutoka kwa raia wasio na hatia kama vile moyo, maini, figo, mapafu, n.k mpaka Leo hii watu wanawatafuta ndugu zao na hawajulikani wako wapi.

Halafu wewe upo hapa kuipaka rangi CCP.

Yoyote anaweza kufatilia unyama huu kupitia link hizi
""

""

No wonder why YouTube and others social medias are prohibited in mainland China.

Investigation imefanywa na wachina na madaktari wa kichina wenyewe kwa zaidi ya miaka 10 ambao pia walishiriki kwenye organ harvesting ya wachina wasiokuwa na hatia bila kujua.

Falon Gong ni aina ya imani ambayo inajumuisha ubora na uimara wa Afya ya miwili na roho ambayo inasisitiza "truthfulness, compassion, and tolerance" pia maditatation ni moja ya Falon Gong practice.

In China you are likely to be killed and your organ to be harvested by a Government managed military hospital if you caught practicing Falon Gong.
 
Back
Top Bottom