China na Afrika zaimarisha ushirikiano wa kunufaishana wa kibiashara

China na Afrika zaimarisha ushirikiano wa kunufaishana wa kibiashara

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
VCG111533170738.jpg
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Idara Kuu ya Forodha ya China zinaonesha kuwa, katika miezi minane ya kwanza ya mwaka 2025, thamani ya jumla ya biashara ya nje ya China ilifikia yuan trilioni 29.57, ambalo ni ongezeko la asilimia 3.5 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

Mauzo ya China barani Afrika yaliongezeka kwa asilimia 25.9 katika kipindi hicho, na mauzo hayo kwa mwaka mzima yanatarajiwa kuzidi dola za kimarekani bilioni 200. Wakati huo huo, uagizaji wa China wa bidhaa kutoka nchi za Afrika, hasa nchi zilizoko nyuma zaidi kimaendeleo, pia uliongezeka kwa kiasi kikubwa. Katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika umeendelea kwa kasi.

Mwaka 2024, thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola bilioni 295.6 za Kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 4.8 ikilinganishwa na mwaka 2023, na kuweka tena rekodi mpya. China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 16 mfululizo, na muundo wa biashara kati ya China na Afrika unaboreshwa. Mauzo ya bidhaa kuu za China kwa Afrika yanabadilika kutoka mahitaji ya kawaida ya kila siku hadi “mambo matatu mapya”, ambayo nia pamoja na magari ya nishati mpya, betri za lithiamu, na bidhaa za photovoltaic. Maagizo ya bidhaa kuu za China kutoka Afrika pia yanageuka kutoka kwa malighafi ya madini hadi bidhaa za kilimo na bidhaa zilizosindikwa.

Ukuaji wa kasi wa biashara kati ya China na Afrika unatokana na sababu mbalimbali. Kwanza, ushirikiano wa miundombinu umekuwa kichocheo kikuu. Tangu kuzinduliwa kwa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, China imeshiriki katika ujenzi wa miradi mingi ya reli, bustani za viwanda na nishati barani Afrika, na kuongeza moja kwa moja mauzo ya nje ya mashine za ujenzi, vifaa vya chuma na vifaa vya usafiri wa reli. Katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu, mauzo ya mashine za ujenzi za China barani Afrika yaliongezeka kwa asilimia 63, na usafirishaji wa magari ya abiria uliongezeka maradufu.

Pili, uvumbuzi wa sera ya biashara ya China umeleta nguvu mpya ya kukuza biashara. China inatekeleza sera ya kutotoza ushuru kwa nchi zote za Afrika ambazo zina uhusiano nayo wa kidiplomasia, hasa kwa nchi zilizoko nyuma zaidi kimaendeleo. Sera hiyo imeongeza kwa kiasi kikubwa ushindani wa bidhaa za kilimo za Afrika katika soko la China. Katika miezi saba ya kwanza ya mwaka huu, bidhaa zinazoagizwa na China kutoka nchi zilizoko nyuma zaidi kimaendeleo barani Afrika uliongezeka kwa asilimia 10.2, jambo ambalo linaonyesha kuwa sera hii inapata matokeo makubwa. Bidhaa maalum kama parachichi za Kenya, kahawa ya Ethiopia, na pilipili kavu za Rwanda zimeingia kwenye maduka makubwa ya China, na kuboresha chaguo la wateja wa China, na kuleta vyanzo endelevu vya mapato kwa wakulima wa Afrika.

Tatu, ushirikiano wa mnyororo wa viwanda unachochea biashara kati ya China na Afrika. China imejenga bustani nyingi za viwanda barani Afrika, ambazo zimesaidia nchi za Afrika kuongeza thamani ya bidhaa zao. Kwa mfano, Bustani ya Viwanda ya TEDA nchini Misri imevutia makampuni 185 na kuleta ajira karibu 10,000. Viwanda vya alumina na chuma vilivyowekezwa na makampuni ya China nchini Guinea na Zimbabwe vimeongeza kiwango cha usindikaji wa ndani cha rasilimali za Afrika kutoka asilimia 15 hadi 45, na kuongeza thamani za rasilimali hizo kwa kiasi kikubwa.
 
Ujinga mtupu, Afrika tunauza nini China?

Wachina wamejaa Afrika wana vuna magogo wanauza china, wanachimba madini wanauza china, sisi tuna uza nini china?
 
Back
Top Bottom