Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China Jumanne ilitoa waraka wa “Jamii ya Binadamu Yenye Mustakabali wa Pamoja: Mapendekezo na Hatua za China”, ukisema miaka kumi iliyopita, Rais Xi Jinping wa China alitoa pendekezo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Kama jumuiya ya kwanza ya kikanda yenye mustakabali wa pamoja, China na Afrika zimetoa mfano wa kuigwa kwa ajili ya ujenzi wa jumuiya ya binadamu kama hiyo.
Nusu karne iliyopita, Wachina wapatao elfu 50 wake kwa waume walikwenda Afrika wakiwa wamejawa na moyo wa urafiki na kufanya kazi bega kwa bega na watu wa Tanzania na Zambia kujenga Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA). Zaidi ya Wachina 60 walipoteza maisha yao kwa kazi hii. Katika ziara yake ya kiserikali nchini Tanzania Machi 2013, Rais Xi Jinping wa China alitembelea makaburi ya wataalamu hao wa China walioisaidia Tanzania, ili kuwaenzi Wachina waliojitoa muhanga ambao wamezikwa hapo. Katika hotuba yake, kwa mara ya kwanza Rais Xi alitoa pendekezo la "Jumuiya ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja".
Katika Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2018, Xi Jinping na viongozi wa Afrika waliamua kujenga jumuiya ya pamoja kati ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja, ikiwa ni kama hatua mpya katika historia ya uhusiano kati ya China na Afrika. Katika Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2021, Xi Jinping alipendekeza "kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya", ambapo jumuiya hii imekuwa ikiendelea kuboreshwa kwa kukuza maendeleo ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili.
Kwa miaka mingi, chini ya msukumo wa pendekezo hilo, China na Afrika zimedumisha hali ya kuaminiana kisiasa. Tangu ziara yake ya kwanza barani Afrika kama rais mwaka 2013, Xi Jinping ameitembelea Afrika mara tano hadi sasa, akienda mashariki, magharibi, kaskazini, kusini, na katikati mwa Afrika. China inawaunga mkono watu wa Afrika kutatua masuala ya Afrika kwa njia za kiafrika na siku zote imetetea maslahi ya Afrika katika jukwaa la kimataifa. China ni nchi ya kwanza duniani kuunga mkono moja kwa moja na kujitolea kuhimiza Umoja wa Afrika kujiunga na G20. Wakati huo huo, mbele ya kashfa mbaya zilizotolewa na baadhi ya nchi za Magharibi dhidi ya ushirikiano kati ya China na Afrika, viongozi wengi wa Afrika na watu wenye ufahamu wamechukua hatua ya kukanusha kile kinachoitwa " mtego wa madeni" na " ukoloni mambo leo", zikiwa ni hatua madhubuti za kulinda jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.
Maendeleo ya pamoja ni lengo linalofuatiliwa na jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja na pia ni msingi wa kutatua matatizo yote. Kutokana na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC na "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ushirikiano wa kivitendo kati ya China na Afrika katika nyanja mbalimbali unaendelea kuzaa matunda. Idadi kubwa ya miradi mikuu kama vile Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Afrika, Barabara ya Nairobi Expressway, na Reli ya Mombasa-Nairobi imekamilika na kukabidhiwa, na hivyo kusaidia maendeleo ya viwanda na mambo ya kisasa barani Afrika. Wakati wa Mkutano wa 15 wa Viongozi wa BRICS uliofanyika Agosti mwaka huu, rais Xi Jinping na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini waliendesha kwa pamoja mazungumzo ya viongozi wa China na Afrika mjini Johannesburg kujadili “jinsi gani jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja inavyoweza kuhimiza mfungamano barani Afrika” na viongozi wa nchi nyingine za Afrika.
Kuna methali ya Kiafrika isemayo “anayefuatana nawe kwenye njia moja ndiye rafiki wa kweli”, ambayo inashabihiana na msemo wa Wachina wa kale usemao “Watu wawili wanapokuwa na nia moja, wanaweza kuvunja dhahabu”. Zikikabiliana na dunia yenye changamoto mbalimbali, China na Afrika zinapaswa kushirikiana zaidi. Katika miaka kumi iliyopita, China imetatua kihistoria tatizo la umaskini uliokithiri, kujenga jamii yenye maisha bora katika nyanja zote, na kuendelea kuhimiza maendeleo ya kisasa kwa mtindo wa China; huku uhuru wa kimkakati wa Afrika na ushawishi wa kimataifa umeendelea kuongezeka, na bara hilo linajitahidi kukuza mfungamano wa kiuchumi, uzalishaji wa viwandani na kilimo cha kisasa. China na Afrika zinapaswa kuendelea kujenga mfano kwa ushirikiano wa Kusini na Kusini na kukusanya nguvu zaidi kwa ajili ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika katika enzi mpya. Kama jarida la Uingereza la "African Leadership Magazine" lilivyosema hivi karibuni, "Uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika utaleta mustakabali mzuri kwa China, Afrika na dunia nzima."