China na Afrika zimekuwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja

China na Afrika zimekuwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
2.jpg


Nusu karne iliyopita, Wachina wapatao elfu 50 wake kwa waume walikwenda Afrika wakiwa wamejawa na moyo wa urafiki na kufanya kazi bega kwa bega na watu wa Tanzania na Zambia kujenga Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA). Zaidi ya Wachina 60 walipoteza maisha yao kwa kazi hii.

Katika ziara yake ya kiserikali nchini Tanzania Machi 2013, Rais Xi Jinping wa China alitembelea makaburi ya wataalamu hao wa China walioisaidia Tanzania, ili kuwaenzi Wachina waliojitoa muhanga ambao wamezikwa hapo. Katika hotuba yake, kwa mara ya kwanza Rais Xi alitoa dhana ya "Jumuiya ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja".

Katika Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2018, Xi Jinping na viongozi wa Afrika waliamua kujenga jumuiya ya pamoja kati ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja, ikiwa ni kama hatua mpya katika historia ya uhusiano kati ya China na Afrika.

Katika Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2021, Xi Jinping alipendekeza "kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya", ambapo jumuiya hii imekuwa ikiendelea kuboreshwa kwa kukuza maendeleo ya ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

Kwa miaka mingi, chini ya msukumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika na Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", China na Afrika zimekuwa jumuiya yenye majukumu, maslahi na hatima ya pamoja. Kwa upande wa siasa, mawasiliano ya hali ya juu yamebeba jukumu muhimu katika kuendeleza uhusiano kati ya China na Afrika. Tangu ziara yake ya kwanza barani Afrika kama rais mwaka 2013, Xi Jinping ameitembelea Afrika mara nne hadi sasa, akienda mashariki, magharibi, kaskazini, kusini, na katikati mwa Afrika. Kwa upande wa uwekezaji na uchumi na biashara, China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 12 mfululizo tangu mwaka 2009, imejenga miradi mikubwa ikiwemo Reli ya Mombasa-Nairobi na Kituo cha Mikutano cha Umoja wa Afrika ili kukuza mambo ya kiviwanda na kisasa ya Afrika na kufanya ushirikiano kati ya China na Afrika kuwa na matokeo na manufaa yanayoonekana.

Kwa upande wa mawasiliano kati ya watu na watu na utamaduni, China na Afrika zinahimiza maingiliano yasiyo ya kiserikali ya kiutamaduni, utafiti wa taasisi za kitaaluma za washauri bingwa na shughuli nyinginezo ili kuhuisha zaidi ushirikiano kati ya China na Afrika.

Kwa upande wa amani na usalama, China imetuma wanajeshi wa kulinda amani zaidi ya 30,000 barani Afrika, kutekeleza majukumu katika maeneo 17 ya Tume ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, na kuisaidia Afrika kuimarisha uwezo wake wa kujitegemea katika kulinda amani, utulivu na kukabiliana na ugaidi.

Katika uwanja wa kuishi pamoja kwa maelewano, China na Afrika zimeimarisha mawasiliano na ushirikiano katika masuala ya kiikolojia na ulinzi wa mazingira kama vile kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi, kutumia nishati safi, kuzuia na kudhibiti kuenea kwa jangwa na mmomonyoko wa udongo, na kulinda wanyama na mimea pori, ili pande zote mbili za China na Afrika ziweze kuwa mahali pazuri ambapo binadamu na mazingira ya asili wanaishi kwa mapatano.

China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea, na Afrika ni bara lenye idadi kubwa ya nchi zinazoendelea. Katika miaka kumi iliyopita, dhana ya "Jumuiya ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja" iliyopendekezwa na Xi Jinping imeonekana kwenye mchakato mzima wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika. Iwe ushirikiano kati ya China na Afrika ni mzuri au la, watu wa China na Afrika, ndio wana sauti zaidi.

Kushikana mikono ili kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika enzi mpya, hili sio tu ni suala linalohusu maslahi ya kimsingi ya watu wa China na Afrika, bali pia litakuwa sehemu muhimu ya jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya binadamu, yenye kuboresha maisha ya watu na kuleta ustawi kwa binadamu wote.
 
Wachina ni ndugu zetu wa Damu
 
Afrika imekuwa China ya China...kama ambavyo china ilikuwa China kwa Marekani+Ulaya.
(definition...China:Sehemu ya kupeleka viwanda kwasababu kuna cheap labor na raw materials)
 
Back
Top Bottom