Hakuna ugonjwa mbaya kama hofu watu hivi sasa tumejazwa hofu kubwa, tena tunaambiwa hii covid ya sasa ni hatari kuliko ile ya kwanza, cha ajabu wao bado ligi na michezo inaendelea kule kwao. Hapa ndio utagundua kwa nini walitaka idadi ya wagonjwa iwe inatangazwa kila siku tena iwe inatajwa kila siku badala ya kurecord kimya kimya kama inavyofanyika kwa magonjwa mengine, tena idadi ya wagonjwa iwe inaongezeka badala ya kushuka, na pia utashanga kwa nini mke wa Bilgate alitabiri Africa tutakufa kama kuku na pia utajiuliza ni kwa nini Biligate amekuwa akizungumzia utishio wa covid utadhani yeye ni waziri wa afya.
Mimi napongeza msimamo wa Mh. Rais asikubali kufuata mkumbo, wananchi tunapaswa kuchukua tahadhari na kuendelea na shughuli zetu kama kawaida. Ni ajabu kuona nchi za Africa zimeshindwa kudhibiti vifo vinavyotokana na malaria, njaa, mafuriko, na ajali za barabarani ambavyo ndio vinagharimu maisha ya raia kwa wingi eti leo wanatumia njia za matajiri wa magharibi kudhibiti na kujikinga na covid.
Corona itakuja na mengi, binafsi naiona kama hii issue imekaa kibiashara zaidi, sikatai kwamba hakuna coron, corona ipo ila kwa jinsi inavyopaishwa wengi wanakufa na kwa hofu. Embu tujiulize, mbona mafua yamekuwa tishio kwa wazungu miaka nenda rudi mbona hakuna chanjo yake? Sisi wa Afrika tukiugua mafua ndani ya siku saba yanaisha yenyewe. Kumbe kuna uwezekano wazungu wangeamua kututia hofu kwenye mafua basi na sisi tungeanza kufa kwa hofu ya mafua then tungeambiwa tumekufa kwa mafua.
Ifike mahala viongozi wetu wajitambue, kwa mujibu wa maandiko mamlaka yeyote yametoka kwa Mungu, tuliona awamu ya kwanza Mh. Rais alikataa lockdown dunia ikamshanga lakini baadae karibu dunia nzima ilifuata njia zake lakini sijaona hao WHO wakimpa tuzo. Naamini na kwenye hii awamu ya pili ataibuka kidedea tena.