China na Tanzania zashindwa kuafikiana kwenye ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, Ujenzi wakwama

miaka 50 ijayo bandari ya dar itakuwa pafinye sana,Bagamoyo ilikuwa imefocuss miaka 100 mbele sio miaka 5 ijayo
Nina imani serikali imekaa na kuona si zaidi ya miaka 20 ijayo, itakuwa na uwezo wa kujenga yenyewe hiyo bandari, kuliko kuingua deni litakalogharimu miaka 99 kulilipa.

Kwa sasa tuhangaike na hizi bandari tatu kwanza, maana hata zenyewe hazifanyi kazi kwa uwezo wake wote.
 
Umedadavua vizuri sana
Labda sasa tuyafahamu hayo masharti ambayo kwetu sisi yamekuwa magumu kumeza
Mwenye kujua masharti hayo aje atuambie ili tuyaweke kwenye mzani
 
Nimeshindwa kuelewa JK aliwakaribisha vipi hawa wachina..! Yani Mradi wa Trillion 23...!!! Bajeti yetu ya mwaka mzima
Ahadi ya kwanza ya mwana TANU:
Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa
 
Huo urafiki wa China na Tanzania upo midomoni tu,mioyoni haupo!
China hawezi kuwekeza fedha zake sisi tunufaike.Lazima anatengeneza faida kubwa kupitia mradi huo.
Wataalamu wetu wawe makini sana kuangalia namna nchi yetu itanufaika na mradi huo mkubwa wenye manufaa kwa pande zote mbili.
 
Je sisi wenyewe hatuwezi kuufanya huo mradi badala ya kutawaliwa kwa sababu ya huo mkataba ?
 

Mbona umekazania " China dept trap" repeat dept trap!! buzz word hii imekuwa manufuctured na media za magharibi na sisi tuna swallow line, hook and sinker za propaganda za magharibi bila ya kutafakari kwa kina kuhusu lengo la Ulaya na USA kuhusu crusade zao dhidi ya taifa la Uchina.

Mataifa unayo yataja hapa kwamba yamepigwa vilivyo na mikataba ya ndio sivyo ya Uchina - tupe ushahidi wa kuonyesha kwamba Serikali za Mataifa hayo yaliwahi kufikisha malalamiko yao mbele ya vyombo vya Kimataifa - hakuna kitu kama hicho - tunacho shuhudia sisi ni media za magharibi kulalamikia ujio wa Wachina barani Afrika na Asia as if Continental Africa is owned by west, yaani wazungu ndio wenye hati miliki ya bara la Afrika.

Tukishirikiana /shikamana na Wachina tutafika mbali kimaendeleo tukiendekeza ujinga wa magharibi kwa kuwa tunaletewa CocaCola/Pepsi, chewing gum na colgate basi Taifa letu tutabaki wasindikizaji wa maendeleo daima duni.
 
Wote ni wale wale, kupata faida kwa kuwalaghai viongozi waroho wa kiafrica.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…