Binafsi naona China wapo vizuri kwenye technology na Engineering kuliko taifa lolote hata US. Ukiangalia wao ndo wa kwanza kutengeneza hypersonic bombs, wametengeneza maglev trains ( treni zinazoelea) na pia wametengeneza treni zinazopita katikati ya majengo bila kuisahau Deepseek AI inayoongoza sasa hivi.
Nakubali China wanatengeneza fake items ila kwenye vitu serious kama meli wapo vizuri ndo maana wanapokea order nyingi.
Umenichekesha sana hadi Deep seekπππ
Kabla mzungu hajatengeneza, mchina hana akili ya kutengeneza kitu kipya.
Baada ya AI kuzinduliwa yeye akakopy na kutengeneza Deep seekππππ
Kwanini mchina hakuwa wa kwanza kutengeneza AI?
Mwenye akili timamu anijibu. Android OS inatumia application yenye extension ya .apk
Hiyo Harmony ya mchina ambayo haijulikani inatumia application yenye extension gani?
Ushawahi kutumia tv ya Hisense yenye Os ya Vidaa ya mchina na TV ya smart ya Android au Google na una Wifi? Ndiyo utajua Vidaa ni takakata.
Mchina yupo kwenye kucopy na kupaste ndiyo maana bidhaa zake ni Quantity na siyo Quality. Watu wananunua vitu vya kichina kwasababu ni bei ndogo na siyo Quantity. Hakuna muziki wa kichina wowote duniani unaweza kuishinda LG, Sony, JBL na Samsung. Hizi bei zake zimechangamka, zile takataka za kichina hadi 50,000 unapata.
Hisense, TCL na takataka zingine za kichina haziwezi kufika kwa Sony, LG na Samsung. Uliza Hisense nchi 100 na Sony, Lg au Samsung nchi 100. Ndiyo utashangaa. Weka tv ya Samsung na Hisense uone utofauti. Mchina anauza bidhaa zenye low quality na zenye bei. Unaangalia TV ya kichina Aziz Ki anaonekana ni mwaarabu
Howo, sharksman vs Scania, DAF na Benz ndiyo maana club zote duniani kubwa kuanzia Arsenal, Barcelona, PSG n.k huwezi kukuta wanatumia mabasi ya kichina.
Quality ina gharama na kwa umasikini wetu lazima uone mchina anatengeneza bidhaa qualityππππ TV ya Samsung nchi 100, ya mchina unanua 2 na chenji unabakiwa nayoπππ