Ndege itauzwa kama iko sokoni, kama haipo sokoni haitauzwa.
F-35 iko sokoni na inashinda tenda zote inazoshiriki, imeuzika units zaidi ya 1,000.
J-20 ya China haiko sokoni, huwezi sema haiuziki wakati haiuzwi. F-22 haipo sokoni vilevile.
Su-57 ya Warusi iko sokoni ila imedoda hakuna mwendawazimu anaweza nunua ndege hata injini yake maalum haina mpaka leo. Mpaka sasa Su-57 inatumia AL-41F1 injini ileile ya Su-35 na some Su-30 variants. Injini ya 4th gen kwenye 5th ni vichekesho.
Injini ya Su-57 ni Izdeliye AL-51 mpaka leo haijawa tiyari wako wanateseka uko kuunda.
Su-57 yenyewe hata squadrons kadhaa Warusi hawana, ukiwaambia wapige elephant walk wanapoteana. Sasa unalinganishaje vitu havina hadhi sawa.