Wakati mwingine tujifunze kuweka akiba ya maneno - kwani unafikiri Wachina na Warusi hawana GPS/GLONNAS guided rockets/shells Systems a.k.a. HIMARS ambazo ni bora zaidi kuliko hizo za Wamerikani au Uingereza. Mfano: ya Warusi inajulikana kama Tornado 9A52-4 ina lenga kwa shabaha zaidi (bull's eye), inabeba mara mbili idadi ya roketi zinazo bebwa na HIMARS, na range yake vile vile ni mara mbili na kikubwa zaidi Warusi hata Wachina wanazo maelfu ya silaha hizo na sio za kuokoteza kuokoteza kama za Zelensky.
Nilisha wambia kwamba mwanzoni mwa 1950s jeshi la Wachina waliwahi kupigana vikali na Jeshi la Merikani mpaka jeshi la Merikani wakarudishwa nyuma kutoka mji wa Pyongyang Korea kaskazini mpaka 38 parallel yaani latitude ya 38 kasikazini -chukueni ramani ebu angalieni umbali uliopo kutoka Pyongyang mpaka 38 parallel ndio mtaona kwamba Wachina si watu wa mchezo mchezo.
Mpaka sasa ni karibu miaka sabini imekwisha pita tangu vita isitishwe na umoja wa Mataifa, that was then,je,mnafikiri hivi sasa Uchina hipo umbali gani kwenye masuala ya silaha za maangamizi zinazo bebwa na land-based and submarine based ICBM, kumbuka Wachina walilipua bom lao la kwanza type ya thermonuclear mwaka 1960,siku hizi wanaunda ndege za kivita (jet fighters) ambazo hata jeshi la Amerika limekiri kwamba baadhi ya ndege hizo zinazidi za Kimerikani kiufundi na kwa kasi - hayo si maneno yangu tafuteni kwenye reliable mtapata.
Bottom line is: msipende pende kubeza beza mataifa shindani na USA kijeshi mkafikiri yatakuwa ni walkover in case jeshi la Merikani likihamua kuzishambulia kijeshi - Uchina ya leo sio ya mwaka wa 1947 mambo yamekwisha badirika sana Diniani, kwa bahati mbaya Uncle SAM haonekani kulitambua hilo, bado ana-wallow kwenye cold war mentality - sina shaka safari hii matokeo ya vita huko Ukraine ndio yatamzidua kutoka kwenye usingizi wa pono baada kupoteza taxpayer's money pamoja na silaha lukuki akijaribu kumsaidia Zelensky na jeshi lake wasizame.