China yafuta kodi zote kwa bidhaa ziingiazo kutoka Africa kasoro kwa nchi ya Eswatini

China yafuta kodi zote kwa bidhaa ziingiazo kutoka Africa kasoro kwa nchi ya Eswatini

Na wanazidi kujazana na kupanua miradi humu, wameshaona how stupid we are!
Kumbe mnajijua kuwa mko stupid?? Kwa mfano wewe kijijini kwenu hujawahi kuiona fursa yeyote.
 
Pamoja na ubaya wao, hiyo ni fursa zuri ya kuchangamkia kwa sasa.

Mzee Trump anaweka Tariffs Kila kukicha na huko Ulaya napo masharti Kibao angalau kuna soko kubwa linalotufaa Africa hapo China.
Huo ni mtego, maana yake na sisi Waafrika tuondoe tariffs.

Mfano sisi Tanzania mwaka 2024 tulinunua bidhaa za dola 4.78 billion kutoka China (30% ya manunuzi yote ya bidhaa za nje). Na tuliuza China bidhaa za dola milioni 700 tu ambazo ni copper ya Congo na mazao.

Sasa ukisema wameondoa kodi let's say 10% maana yake wametupunguzia milioni 70 USD, ila sisi tukiondoa tutawapunguzia milioni 478 USD.

Kenge ni nani hapo?
 
Tungekuwa tunajitambua na tuko aggressive basi tungefaidika na hii fursa regardless Faida atakayopata China... Maana Sisi Sana Sana tunapeleka mazao, maana Yake wachina watapata Kwa bei rahisi na wao watauziana nchini kwao Kwa bei nzuri au wakauza end product Ulaya Kwa bei nzuri maradufu maana Ulaya bei zao ziko vizuri...Mathalan kuhusu madini, mfano Yale madini yanayotumika kwenye tech, kampuni zao zitapata Kwa bei nzuri hivyo watazidi kwenda juu au kuleta ushindani Sana Kwa tech products ambazo wako nyuma, cost zikiwa ndogo ni afueni Sana Kwa giant kama China...

Yaani hapo China kacheza vizuri Tu, hasa kwenye madini na mazao ya kilimo na misitu, Sidhani kama tuna mkakati wowote wa maana wa kumfaidisha mtu wa mwisho, hapo atanyonywa mtu wa chini ili wazee wa connection wale.
 
China anatafuta kuja kutumia nchi za kiafrika kuuza bidhaa zake nchini Marekani baada ya kuzidiwa na tariffs na mchezo huu ameufanya nchini Lesotho.

Leo hii ili nguo za Lesotho ziingie nchini Marekani zinatozwa ushuru asilimia 40 hali ambayo imeiacha hoi nchi hiyo na wawekezaji wake wa kichina.

Vinginevyo Afrika hawana lolote la kufaidi kutokana na hatua hiyo ya China kwani bara hili sanasana huuza malighafi tu nchini China ambayo hata hivyo huingia nchini China bila kulipiwa ushuru kando ya hapo Afrika hawana chochote cha kuuza China kwa sababu Afrika haina any meaningful manufacturing base worth talking about.
 
Hakuna watu siwapendi kama wachina. Wakivamia mahali wanakula kama mchwa. Wanafika ambako huwezi kufikiria wanaweza kufika, madini ya Nchi hii wachina wanayachota kweli kweli.

Kwa mwenendo huu wa wachina kuvamia Kila mahali na kuchimba madini ( hasa dhahabu) sidhani kama miaka 10 ama 15 ijayo tutakuwa na dhahabu.
 
Hapo ni malighafi za wachina zinazozalishwa huku Africa waziingize katika soko lao China, kumbuka hizo malighafi zinazalishwa na wafanyakazi wa kichina huku Afrika hivyo china inakuwa imetafutia watu wake fursa za ajira. Ni sawa na wewe ukose shamba la kulima kisha uende kwa jirani umwambie nipe kipande cha shamba nizalishie mahindi hapa wakati navuna yangu kupelekwa kwangu nitaweza kukuruhusu na wewe uje utunze au uuze kwangu.
Una akili sana. mtego huu ni watu Smart pekee wanaweza kuunasua
 
Huo ni mtego, maana yake na sisi Waafrika tuondoe tariffs.

Mfano sisi Tanzania mwaka 2024 tulinunua bidhaa za dola 4.78 billion kutoka China (30% ya manunuzi yote ya bidhaa za nje). Na tuliuza China bidhaa za dola milioni 700 tu ambazo ni copper ya Congo na mazao.

Sasa ukisema wameondoa kodi let's say 10% maana yake wametupunguzia milioni 70 USD, ila sisi tukiondoa tutawapunguzia milioni 478 USD.

Kenge ni nani hapo?
Lakini hawajatuambia na sisi tuondoe wala kupunguza Tariffs, nadhani ni njia tu ya wao kukuza biashara na Africa.
 
Fuatilia mambo ujue kiundani. Ukipeleka bidhaa yako Ulaya inanunuliwa kwa bei kubwa hata zaidi ya mara 3 ya bei watakayokupa wachina. Kwa hiyo kiuhalisia hata ikiondolewa hiyo kodi, haikupi unafuu wowote wewe muuzaji, bali imelenga kuwanufaisha watu wao waingize bidha zilizonunuliwa kwa bei ya chini, kisha na wao waziuze kwa bei ya chini nchini China.
Kwani Ulaya hawatozi Kodi bidhaa kutoka Africa?..
 
Kwani Ulaya hawatozi Kodi bidhaa kutoka Africa?..
Nchi huwa zinaweka tarrifs kwa bidhaa ambazo zitaleta ushindani kwa wazalishaji wake walio ndani ya nchi yake, Ulaya hawawezi kuweka tarrifs kwenye maparachichi, chai na kahawa yetu tunavyowazuia kwa sababu hawazalishi, ugumu wa kuuza bidhaa Ulaya ni kufikia vigezo vyao vya usalama wa kiafya.
 
Kwa hiyo Ulaya na Marekani tariffs zao kwa nchi za Africa hazihusu kabisa bidhaa ghafi ?

Na siku wakiweka ujue wanakuadhibu sio?...
 
Kwa hiyo Ulaya na Marekani tariffs zao kwa nchi za Africa hazihusu kabisa bidhaa ghafi ?

Na siku wakiweka ujue wanakuadhibu sio?...
Kwanza mahitaji ya Marekani ni tofauti kabisa na Ulaya, US wanazalisha bidhaa nyingi sana ghafi na kwa wingi hadi na wao wanatafuta soko la nje(mfano soybeans, mahindi, ngano, pamba na nyama) tofauti na Ulaya halafu wana nchi nyingi za karibu za America ya Kusini, Mexico na Canada zilizo karibu mdomoni kujazia mahitaji yoyote muhimu wanayohitaji kwa hiyo hata malighafi za Africa zikiruhusiwa bila tarrifs bado ni mlima mrefu kuupanda.

Hata hivyo pamoja na hayo yote kabla ya mwendawazimu Trump kuingia anayeweka tarrifs hadi kwenye visiwa vya penguins tu au jinsi atakvyoamaka bado bidhaa za mazao kutoka Africa zilikuwa hazichajiwi tarrifs kuingia US.
 
Hiyo sio modus operandi ya China na wala haiihtaji ukoloni wa aina hiyo kwa sababu utamuingizia gharama tu zisizo za ulazima. Shida ya China ni malighafi, rasilimali, soko la bidhaa zake za viwandani, mahali pa kuwekeza mtaji, ajira na kupunguzia population yake. Mambo haya yote anayapata kwa urahisi sana katika Africa ya sasa kwenye nchi yoyote kwa sababu ya Magharibi kurudi nyuma Africa . China hawahitaji kuingilia siasa zetu wala kuleta majeshi yao.
Itafika mahali watafanya hivyo pindi wakinogewa na kuona maslahi yao yapo hatarini kwa namna fulni.
 
Lakini hawajatuambia na sisi tuondoe wala kupunguza Tariffs, nadhani ni njia tu ya wao kukuza biashara na Africa.
Marekani, Ulaya, Canada zikiweka tariffs kwa China nayo inaweka counter tariffs.

Ikiwa imeondoa basi huo ni mwanzo, baadae watakuja na kutaka sisi pia tuwaondolee ili waendelee kumwaga bidhaa zao kwetu na kutusababishia deficit kubwa.
 
Itafika mahali watafanya hivyo pindi wakinogewa na kuona maslahi yao yapo hatarini kwa namna fulni.
Inawezekana kama West itarudi kuwa mshindani wake thabiti au kutokee decline kubwa sana kwenye uchumi wake. China ni smart sana kwenye geopolitics na Taifa lenye ubinafsi wa Hali ya juu ndio maana inafanya biashara na kila taifa duniani ikipata maximum profit, haijali wewe ni Taifa la demokrasia au dikteta unayekata vichwa watu wako, una amani au uko vitani, haijali mazingira, haijali dini.
 
Back
Top Bottom