Wabongo tuna ushabiki mpaka kwenye vitu visivyotuhusu.
"US VS THEM" mentality kila sehemu.
Ushabiki wa kitoto namna hii unatufanya tushindwe kujadili hali ya mambo kama ilivyo.
Inapaswa uifahamu China kwanza, kisha utaelewa jinsi gani inafanya kazi, Matumizi ya nguvu kwanza sio tabia ya China, tofauti na Marekani (Na washirika wake wa Ulaya Magharibi) ambao wao Ubeberu na matumizi ya nguvu kwa masilahi yao ndio kitu kikuu (imperialism).
China wangekuwa na mindest ya US, Africa tungetawaliwa na Wachina kwanza kabla ya wazungu. Mchina anafanya biashara tangu karne ya 13, kipindi ambacho hata karatasi bado hazijafika Ulaya.
Hio reaction ya China kuivamia Taiwan baada ya ujio wa Nancy Pelosi, ndio kItu ambacho Strategists wa US walichokitaka
Lengo wapate justification ya kupambana na China vita ya kiuchumi, ikumbukwe kuwa Mataifa yoyote yenye silaha za Nyukilia, kamwe haziwezi kuingia vitani, hii ni kwa sababu ya MAD Doctrine ( Uhakika kuwa vita yoyote kati yao, itayarudisha matifa yao na dunia nzima zama za mawe)
So namna pekee ya kupambana ni through proxy war (Mfano Russia na Marekani over ukraine) na vita ya kiuchumi kama US na washirika wake hivi karibuni walivyofanya kwa Russia na Russia alivyoitikia kwa ku cut gas supply na kuwa karibu zaidi na BRICS members haswa China.
Kama ilivyokua British Empire kabla yake Marekani inadondoka, uchumi wa marekani umening'inia juu ya kamba nyembamba sana ya "Petro dollar system" inayo mpa upendeleo marekani wa ku print pesa out of nothing na kuendelea ku fund jeshi lake, so nchi pekee inayotishia Petro dollar system ni adui yake kama China
China anaifahamu hii trick, so kafanya kile unachotegemea kwa mwenye busara kufanya.
Badala ya kuivamia Taiwan kama USA alivyotaka, (Proxy war nyingine kati ya USA na China uwanja ukiwa Taiwan) China badala yake kawaonyesha Wamarekani kuwa in case of taiwan hawatokua na uwezo wa kuchangisha pesa ya kutuma silaha kama walivyofanya kwa Ukraine, cause unlike Russia sisi tunauwezo wa kukizunguka kisiwa kizima ndani ya siku chache tu.
So huwezi kutoa au kuingiza kitu bila kuivaa PLA.
So kama USA wapo tayari kurudi karne ya 7 kisa Taiwan, that's ok.