Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Takwimu zinaonesha kuwa, akiba iliyothibitishwa ya madini muhimu barani Afrika inachangia takriban asilimia 30 ya akiba yote duniani, ikiwa ni pamoja na madini ya kimkakati kama vile kobalti, platinamu, lithiamu, na manganese. Wakati huo huo, uwezo mdogo wa utafutaji na usindikaji, na ukosefu wa miundombinu na uwekezaji katika nchi za Afrika umezuia maendeleo ya tasnia muhimu ya madini na ongezeko la mnyororo wake wa thamani. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, katika miaka ya hivi karibuni, nchi za Afrika na mashirika ya kikanda yameweka maendeleo ya sekta ya madini muhimu katika mikakati yao ya juu. Umoja wa Afrika ulitoa rasmi “Mkakati wa Madini Kijani wa Afrika” mwishoni mwa mwaka 2024, ukifafanua wazi nguzo nne, ambazo ni maendeleo ya madini, ujengzi wa vipaji na teknolojia, ongezeko la thamani, na usimamizi wa mambo ya madini, ili kufanya rasilimali za madini barani Afrika ziwe vichocheo vikuu vya maendeleo ya viwanda, mseto wa kiuchumi, na mabadiliko ya kijani.
Tukichukulia mfano wa Zimbabwe, nchi yenye akiba kubwa zaidi ya lithiamu barani Afrika, lakini kutokana na ukosefu wa uwezo wa usindikaji wa kina, inaweza tu kupata faida ndogo kupitia mauzo makubwa ya madini ghafi. Ili kubadilisha hali hii, serikali ya Zimbabwe ilisimamisha mauzo ya nje ya madini ghafi ya lithiamu mwezi Februari mwaka huu, ili kuhimiza maendeleo ya viwanda vya usindikaji.
Sera hiyo mpya inachukuliwa na nchi za Magharibi kama ishara ya “kuzorota kwa mazingira ya biashara,” lakini makampuni ya China yanaiona kama fursa ya ushirikiano wa kina. Makampuni ya China, yanayowakilishwa na Huayou Cobalt na China Mineral Resources, yameitikia mahitaji ya Afrika kwa uwekezaji mkubwa. Hata kabla ya sera mpya ya madini ya Zimbabwe kuanzishwa, Huayou Cobalt ilikuwa tayari imeanza ujenzi wa kiwanda cha kusindika lithiamu salfeti chenye uwezo wa uzalishaji wa tani 50,000 kwa mwaka.
Katika miaka ya hivi karibuni, China imeziunga mkono nchi za Afrika katika kuongeza thamani ya madini yake. “Mpango wa Utekelezaji (2025-2027)”, uliopitishwa katika Mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing wa mwaka 2024, unapendekeza wazi kuunga mkono ujenzi wa minyororo ya thamani na maendeleo ya utengenezaji na usindikaji wa kina wa madini muhimu barani Afrika, na kutoa msingi wa sera kwa ushirikiano wa kina kati ya pande hizo mbili katika uwanja wa madini muhim