China yasamehe mikopo 23 ya nchi 17 za Afrika

China yasamehe mikopo 23 ya nchi 17 za Afrika

China keshapiga hesabu kaona deni lake lishajilipia kupitia bidhaa anazouza Afrika mfano bodaboda,mabus na malori na bidhaa mbalimbali za machinga. China anavuna faida toka lini china akawa na humanity hio ya kusamehee.Kasamehe Ili awaingize kingi wakope tena, watawala wa kiafrica wamelogezewa kwenye kukopa, maana kupitia kukopa Wanapata percentage zao pia ndio njia rahisi ya kutakatishia kodi zetu, wao wanakopa lakini wananchi awashirikishwi kwenye mipango ya matumizi ya mikopo hio.
 
Boda boda na machinga wa waafrika wamesaidia Sana kukuza uchumi wa China wakiwa kama madalali wa viwanda vya china piga idadi ya pikipiki na bidhaa zote wanaouza machinga wanamuingizia China bei gani kwa siku. So hata akisema kasemehee deni ni lugha tu lakini deni lilishajilipa kitambo kupitia forex exchange.
 
Machinga na bodaboda ni madalali wa viwanda vya china jumla ya pikipiki za china zilizopo afrika nzima soon zitalingana na population ya waafrika. Pesa nyingi Sana tunatuma china KILA siku toka afrika kwa ajili ya kununulia bidhaa. Hata idadi ya abiria wanaoutua viwanja vya China toka afrika wengi ni wafanyabiashara wanaopeleka pesa china kununua bidhaa, tofauti na Wachina wengi wanaotoka afrika wengi uondoka na pesa walizochuma afrika. So Mchina madeni yake yanajilipa kupitia unafair balance of payment. Huku afrika wachina wanakuja na utaalamu wanarudi kwao na pesa, sisi waafrika tunawapelekea pesa tunarudi na bidhaa. So wao ndio wanafaidika zaidi.
Ni SAwa na japan kusema anakupa msaada au mkopo ni ile ile pesa yako aliyoichukua kupitia kukuuzia gari na spare. Gari za Ulaya afrika ni chache nyingi ni kutoka kampuni za kijapani.
 
Uzuri wa China hapo atakuwa ashajilipa kifuatacho baada ya hapo atawakopesha tena ili ajilipe tena maradufu.

WaAfrica hakuna rafiki wakweli anayeweza kukupa hela duniani awe Mzungu, Mhindi, Muarabu, Mchina, Mrusi nk.

WaAfrica tufanye kazi tuijenge Africa tuachane na hii misaada.

Neno
 
Back
Top Bottom