Kinachofanya China asiivamie mpaka saivi ni nn?
Mzee hii ishu sio rahisi kama unavyofikiria.
Ungejua yanayoendelea China main land usingeongea haya.
Migomo ya mara kwa mara, watu wanakatwa pesa Zao za mishahara na pensheni bila sababu hivyo vitu China saivi vimekuwa ni vya kawaida.
Maswala ya vita huwa hayana prediction, unaweza kuwaza Hivi halafu mambo yote yakaenda tofauti kabisa na unavyowaza.
Jeshini tu PLA la uchina Kuna tatizo rushwa lililo kithiri, unajua hadi vyeo vya kijeshi China watu wananunua? Sasa hiyo ni mbaya sana na inashusha morali.
Kwa kifupi China ina mapungufu mengi sana, nakushauri watafute wachambuzi wa maswala ya Geopolitics Mr. George G Chong na Mr Peter Zein wasikilize hao jamaa wameishi China na Hong Kong for more than 25 years wamezunguka China main land kwenye makampuni ya selikari ya China na private wanachambua vizuri sana madhaifu ya China.
Huu mgogoro kwa kifupi utaleta matokeo mabaya sana kwa China.
1. Sio wajibu wako kuwapangia China ni muda gani sahihi wa kuvamia Taiwan, wala Taiwan sio priority ya kwanza ya China. Kwahiyo kutovamia haimaanishi hawawezi, Mwakinyo kukataa pambano na Mandonga haimaanishi hamuwezi.
2. Issue sio rahisi, haijawahi tokea vita rahisi. Vita zote unazoona duniani huwa ni maamuzi magumu. There is no easy or short war na kila anayejua lolote kuhusu vita anajua hili.
3. Yanayoendelea China mainland huyajui peke yako, katika nchi nafuatilia inaanza Uturuki inafuata China ila katika majeshi nafuatilia China ni ya kwanza. Kwahiyo siandiki kama mashabiki lialia wa mpira.
4. Migomo, lockdown, pension, housing, unemployment, restrictions na government intervention kwenye investments, firewall, mass surveillance, authoritarianism ya Xi na matatizo mengine mengi ya China nimeyazingatia sana kabla ya kuandika. Pension haifyatui risasi, marubani wa jeshi hawatoshindwa kuendesha fighters kisa mabilionea wa China wamezuiwa na CCP kuwithdraw pesa wakimbilie Western countries kwenye uhuru.
Nazi Germany wakati inaanzisha Operation Barbarossa dhidi ya USSR kwani Wasovieti walishindwa kupigana kisa Stalin jeshini alifanya The Great Purge ya late 1930s? Stalin kwa mkono wake mwenyewe aliua Wasovieti zaidi ya milioni 6 kwa mass containment, akaua mamia ya maofisa wa jeshi, akatumia Cheka kuua komredi wenzake wa Bolshevik, akaanzisha Gurags kule far East na kuwafunga waandishi wapendwa na wanasiasa kisa wamemkosoa. Akafunga huduma za kidini zote, sio kanisa katoliki wala kanisa pendwa la serikali lile Orthodox. Ujerumani ilipovamia matokeo si unayajua mwenyewe.
Unajua mazingira gani wananchi wa Japan walipitia kabla ya IJN kuvamia Pearl Harbour na kuanzisha vita dhidi ya Marekani. Mbona walipigana vita kali miaka mitatu tena Wajapan wakajitoa hadi muanga na suicide missions zao za kamikaze attack na banzai charges. Kuna nchi ambayo raia wakishirikiana na jeshi kwenye WW2 kuizidi Japan?
5. Nani kakwambia vita haina prediction? Vita ina prediction na military schools na institutions duniani ndio kazi zake hizo. Marekani hadi wana wargames wanalipa hela nyingi private companies zidevelop hypothetical scenarios.
Prediction kuwa sahihi au sio sahihi ni jambo lingine, na kuna options nyingi. Usahihi wake utategemea ni information kiasi gani unayo na uwezo binafsi wa kuichakata kutoa hitimisho.
6. China wana mapungufu mengi kama nchi nyinginezo, hakuna nchi haina mapungufu. Au basi waambie Waarabu kwamba Israel kwa sasa ina mapungufu kisiasa, maandamano, kesi za rushwa za vigogo, mgogoro wa Wakristo & Waislamu na Wayahudi na unyanyasaji kwa raia wenye asili ya Kiarabu kwahiyo waivamie uone.
Kununua vyeo vya kijeshi haimaanishi walionunua ni vilaza completely, kwanza ni asilimia ngapi ya vyeo vinanunuliwa au umeambiwa vyote wananunua. Morali ya kipindi cha amani sio ya kipindi cha vita, inanishangaza kuona unatarajia China wanajeshi wasiwe na morali.
Airbases za Taiwan zote zinajulikana, ground facilities baaadhi zinajulikana, highways kwa ajili ya emergency runways zinajulikana, naval bases na submarine pans, fixed radar installations, shore based defense lines kule Western sides. Vyote hivyo kwenye eneo linazidiwa sana ukubwa na Tabora, then useme jeshi superior la China lisiwe na morali kwa kisa cha kuokoteleza eti maofisa wananunua vyeo.
Amka usingizini wewe. Taiwan haitoshinda vita kisa China ina matatizo, na uache kukimbilia Marekani badala utaje hiyo Taiwan kwanza. 82nd Airborne Division ambayo ndio hutakiwa kuwa standby muda wote haiwezi peke yake kuipiga China, US Marines wakiongezeka hawawezi, hata Pacific Fleet yote ikija haiwezi mpaka ije task force. Sasa task force na logistics zake mpaka zikamilike kufanya uvamizi kwa China, Taiwan ishatekwa muda sana.
Narudia kusisitiza, hii ni CHINA vs TAIWAN. Marekani sio guarantee itakuja na ikija ni vita nyingine hiyo yenye mazungumzo tofauti na haya.