China yatuma ndege 38 za kijeshi mpakani mwa Taiwan

Hilo sio rahisi,wewe unafikiri kwa Marekani anaweka makambi kila kona ya Dunia? Sababu ili aweze kupigana vita zaidi ya moja kwa wakati mmoja.


Logistical issue zinasumbua hata mataifa makubwa tajiri si kwa si masikini tu peke yake mkuu

Logistical strains au long supply line ndio sababu moja wapo ya Mjerumani kupoteza katika Eastern Front wakati wa WWII ingawa zipo na sababu nyingine nyingine

Ingawa anyway naweza kuwa Wrong pia sababu mi mwenyewe na"digest" tu point -outs za analysts
 
Embu tuongee kwa mazingira ya sasa ikitokea vita pale Mashariki ya Mbali,Marekani atapata shida gani ya logistics?
 
Hao wachina wawaige warusi walivyo kwapua jimbo crimea kutoka ukrane. Wakizubaa hao taiwan watajiunga nato.
Ndivyo inavyotakiwa na kuna uwezekano ikawa hivyo japo Taiwan ni tofauti na jimbo la Crimea

Kwa Taiwan ni pagumu sababu Marekani inaweza kutoa saport ya silaha Jambo ambalo linaweza kupelekea vita vikubwa vinavyoweza kubadili kabisa historia ya dunia
 
Kivipi kisiwa cha Taiwan kinaweza kusababisha hili?
 
Unawachukulia poa Taiwan sio? Hapo mchina anapaogopa sababu anajua akigusa tuu ni total destruction kwake na kwa Taiwan.
Ondoa hofu. China inaweza kunyakua eneo lake halali la Taiwan kwa siku moja sema mataifa washirika wa Taiwan wanaweza kufanya makosa yatakayoyopelekea dhoruba kubwa dunia nzima
 
Embu tuongee kwa mazingira ya sasa ikitokea vita pale Mashariki ya Mbali,Marekani atapata shida gani ya logistics?

Vita na China ni vita kubwa mno kiasi kwamba hata hao ambao wana base zake its probably watakataa US asitumie US military bases in those countries

Na umbali ni mrefu sana kutoka US mpaka China via Maritime logistics
 
Hawa wavimba macho watakipata wanachokitafuta ila varangati litakuwa ni la kukata na shoka ambalo litaathiri dunia nzima kwa miaka mingi ijayo hasa kama varangati hilo litakuwa ni la muda mrefu.


 
Niliwahi sikia analysis moja inayosema kwamba China atategea kipindi ambacho USA ametingwa na uvamizi fulani wa nchi kubwa nyingine halafu yeye ndio anautumia muda huo kuivamia Taiwan na ataichukua sababu kwa sasa China yupo Mbali sana kijeshi
Naam! Ikitokea hivyo China itatumia mwanya huo.
Lakini tusisahau hata kama USA hatotingwa na uvamizi wowote, lazima China itataka na itafanya kuichukua taiwan kwa nguvu.
Sasa hatujui matokeo yatakuwa yapi maana hatujui ni nini Marekani itataka kufanya pale China itakapochukua uamuzi huo
 
Taiwan haiwezi kuwa sawa na Crimea au Kashmir, ni ngumu kumezwa kwa nguvu bila kutokea madhara au uharibifu.
China inaweza kupeleka jeshi kubwa kuliko raia wote wa Taiwan pamoja na vifaa vya kisasa vya kijeshi na kunyakua kwa siku moja. Labda tu Marekani atake kutia kiherehere ndipo vita vitageuka kuwa vya mafahali wawili au vya dunia nzima... Hili linawezekana
 
najaribu kuvuta picha marekani inapigana kuilinda new York ama mji wake, either mshirika wake mhimu yoyote sijui ni silaha gani itatumika kumkabiri adui.
hope dunia itakuwa suppressed tena toka siku za Nagasaki na iroshima.
Akifanya hivyo kumbuka maadui zake nao wanazo... Kwa kizazi hiki ukirusha bomu moja la nuclear wenzako watakurushia mabomu 20. Ukijibu kwa kurusha mabomu 50 wenzako watakurushia akiba yao yote maana watajua hakutakuwa na wakupona wala mshindi 😊😊😊
 
Wewe unaona mbali
 
hatupaswi kuipuuza china lakini ni uupuzi kudhani china anaweza mess up na Us na akabaki kama alivyo.
Wasipoogopana wote wataporomoana na kupotezana... Kumbuka wote wana nguvu na wote wana washirika wenye nguvu.

Vita vyao vya moja kwa moja vitakubadilishia hadi wewe historia yako
 
Kwa vita vikubwa kati ya haya mataifa makubwa hawahitaji kuwa karibu ndio wapigane
 
chief hatupaswi kutemegea china kuivamia Taiwan hivi soon labda hapo baadae endapo wataona calculations zao zimekaa sawa.
china hawezi kubali kurudi kwenye stone age et kisa anatafuta uzibiti dani ya tawain.. hapo alipo ka- sacrifice mambo mengi hadi kufika levo hiyo ya kiuchumi, ni ngumu kufanya uamzi hatari kama huo.
hayo mengine ni Show off tu na kutuma ujumbe kwa Taiwan na mshirika wake kuwa sasa china sio ileee ya kipindi kile.

kuivamia Taiwan ni suicidal decision kwa china, china hajui ni majibu gani Taiwan itatoa ama mshirika wake mkuu Us atajibu nini.
tusitegemee insu ya taiwan ikawa kama Afghanistan.
kesi ya Afghanistan na Taiwan ni vitu viwili tofauti.
 
Hawa wavimba macho watakipata wanachokitafuta ila varangati litakuwa ni la kukata na shoka ambalo litaathiri dunia nzima kwa miaka mingi ijayo hasa kama varangati hilo litakuwa ni la muda mrefu.
Usiwe na hofu kisiwa hicho kitaunganishwa na China moja kiulaini tu.... Marekani ikisogeza pua yake ndipo vita vitaathiri dunia yote.

Dunia ya sasa kambale ni wengi alafu ni wakubwa
 
Anachoona China ni kwamba akichelewa Taiwan itazidi kujiimarisha na silaha za Marekani.
Pia akiwahi kuivamia kuna uwezekano likawa ni jambo la hatari linaloweza kuiyumbisha China kwa kiwango kikubwa, ila kuna option wanayo ya kuwahi kuibeba taiwan huku wakiwa tayari kuingia vitani na Amerika pale itakapobidi.
Option hii hata Amerika anaiogopa maana itamgarimu kwa kiwango kilekile itakavyoigarimu China.

Naweza kukwambia Taiwan haitomaliza miaka 10.

Baadhi yetu humu tutalishuhudia hili! China yupo tayari kwa 100% hata kuiingiza dunia vitani kwaajili ya Taiwan kuliko Marekani ilivyo tayari kusimama na Taiwan kwa 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…