Shida yangu siyo mnachokiabudu,swali langu ni kwa nini mnaloga wenzenu wakwame kimaisha
na kuwakaba usiku wakose usingizi ambao ni zawadi ya kila mtu kutoka kwa Mungu?
Mkiachana na dhana hiyo endeleeni na imani zenu za kuabudu miti maana hamvunji sheria.
Mbona ulichoandika hakieleweki my brother!! Ni nani alielogwa akwame kimaisha? Una ushahidi gani kuwa sisi ndio tuliomloga akwame kimaisha?
Unajua huu ujinga ulioandika hapa ndo unaotufanya wengi tuwaonge mkono wachina, pia tupingane na imani zenu ambazo mmeletewa ili mpambane na wenzenu (mwafrika kwa mwafrika au ndugu kwa ndugu).
Haiwezekani kila kitu ambacho kipo kinyume na matarajio yenu mkihusishe na uchawi. Mtu amekwama mwenyewe kimaisha aidha kwa sababu ya uzembe wake, elimu yake, uvivu wake, ujinga wake nk nyinyi mnakimbilia kuhusisha swala hilo na uchawi.
Mwisho wa siku anatokea mtu anakwambia kuwa yeye anaweza kukuombea ili kuutoa uchawi unaosababisha ukose kazi kumbe ndo anaenda kukupiga mazima yani hata kile kiakiba chako ulichoweka anakichukua na kukuacha solemba huna mbele wala nyuma.
Alioyafanya TB Joshua umeyasikia lakini? Nafikiri unakumbuka kuwa TB Joshua alikuwa kiongozi mkubwa wa kanisa, lakini kumbe alikuwa anabaka, anadhalilisha na kutapeli watu.
Sheikh Yahya kabla ya kufa katapeli watu kinoma nina imani hili pia unalijua.
Mungine kawawekea watu mafuta wakanyage wengine wakafa yeye akakusanya sadaka na familia yake, leo hii wanakula bata tu.
So mimi binafsi naamini Mungu yupo ni mmoja na wa kila mtu. Unaweza kumuomba ukiwa kazini, nyumbani, kitandani, kwenye gari na popote.
Hao miungu wa kwenye miti, wa waarab, wazungu, wayahudi mimi nawaona wa uongo tu.