China yavunja rekodi tena yazindua treni ya umeme yenye kasi kubwa zaidi Duniani

China yavunja rekodi tena yazindua treni ya umeme yenye kasi kubwa zaidi Duniani

Check your fact boy,
Treni za Tazara zinaongozwa na nani? Ni hao wachina,delay , derailment , wizi , kila kitu hovyo.
Na mambo mengi njiani huko hadi Kapiri mposhi.wanapiga deal zao.
Kubeba abiria ni mwamvuli tu.
Nazungumzia za kwao China, kwa upande wa TAZARA sijui sana mabadiliko yaliyofanyika na kinachoendelea. Kwani management yote ni Wachina?
 
Hii ndiyo mchongoko wa kweli ile ya Kadogosa ni butu kabisa
Ya Kadogosa ni Mkorea, alitakiwa ampe kandarasi Mchina. Angeleta mchongoko wenyewe basi hata upande wa mabehewa angempa Mchina tuinjoi

Si umeona haya mabehewa ya Kenya ya first class mkono wa Mchina unasafiri kiboss kabisa comfortable
20241231_074720.png
 
We panda hizo, mi siamini chochote cha mchina.
Kuna kitu kinaitwa exposure, ukikosa hii utakua unaamini vile vilivyokuzunguka tu, kumbe huko duniani mambo tofauti.

Mkuu badilisha mtizamo... Vinginevyo utakua unajipotosha, kwanini ni kwasababu bidhaa za kichina unazoziona huku bongo ni wametukadiria uwezo wute wa kumudu gharama, pia wafanyabiashara wa kiafrika hasa Tanzania wanachukua mzigo China ile ya bei nafuu(grade 3) ila wakifika huku wanatupiga bei kama ya bidhaa ya grade 1 wanafanya hivyo kutengeneza faida kubwa.

Ila ukitaka vitu bora kutoka China vipo na ndio vingi huvioni huku bongo kwasababu hatuna uwezo wa kumudu gharama zake hivyo hata watu wamasoko wa makampuni mbalimbali huko China hawaoni kipaumbele ku supplies bidhaa hizo huku hivyo wanafocus ulaya nk.

Mfano. Simu za kichina hapa bongo, mbongo ukimuuliza atakwambia ni tecno infinix na itel lakini je unajua kuna simu kutoka China huko duniani zinashindana na kina iPhone pixels na Samsung kwa kila kitu na bado simu za kichina zinawatoa jasho.

Sisi hao wachina walishatufanyia utafiti wakagundua mazingira na uwezo wetu ndio maana kwenye maonyesho wanatuletea maguta pikipiki ya miguu mitatu nk. Vitu ambavyo ni vya ubora wa hari ya chini mno na shida sio wao shida ni sisi hivyo wametukadilia uwezo wetu wameamua watusaidie na vimekua msaada mkubwa mno kulingana na uwezo wetu bila hivyo usafiri wa baiskeli kubebea watu ungekuepo hadi Leo.
 
Hayo ni maendeleo binafsi ya mtu au kampuni usiyakejili siajabu wewe kitu ulichofanikiwa ni kuzindua boksa mpya tu
Sijakejeli, nimeeleza hali halisi ya mahali tulipo kiteknolojoa na kiuchumi.

Kama unaona kuna sehemu kuna kejeli, please bold the sentence and quote it with my name on a tag
 
Kwa mara nyingine tena China imeonyesha ina high tech kwenye high speed train kwa kuzindua treni yenye kasi ya 450km/hr mnamo Desemba 29

Kwa sasa inashikilia rekodi ya kasi kubwa zaidi duniani. Treni hilo limepewa jina la CR 450 limezinduliwa jijini Beijing

Litakuwa na safari kati ya Beijing na Shanghai (1200km) Katika majaribio limetumia masaa 3 tu.

1200km ni sawa na umbali wa kutoka Dar mpaka Kigoma (Kasulu), imagine usafiri kwa masaa 3 tu ni kama umepanda mwewe wa ardhini

Improvements in speed, energy efficiency, interior noise reduction and braking performance
View attachment 3189081View attachment 3189082View attachment 3189083View attachment 3189084View attachment 3189085View attachment 3189087

View attachment 3189091View attachment 3189092
View attachment 3189093View attachment 3189094

Fast, On time, Comfortable. China never stops!!! Always breaking the rules and setting new standards
Dah!...SGR yetu tuiboreshe kwa kuiletea treni kama hii
 
Tazara walijenga na tunawalipa mpk leo, ilikua nchi ya kijamaa, sasa ni ya kibepari.
Hamna ubora kwenye kila kitu wao wanajali hela tu.
Wanakuuzia kitu chenye life span ndogo kikifa utupe ununue kipya.
Unauziwa kutokana na budget yako na mategemeo yako, hata ukitaka guarantee mchina anakupatia
 
Kwa spidi iliyotumika kukata umbali huo abiria hwajatoka na kizungu zungu kweli?
Haina kizunguzungu kwani kwenye ndege unasikia kizunguzungu?

Unaweza kuweka glass ya maji au chupa kwenye meza na hainguki

Kuna kipindi Putin alienda China akawa na mazungumzo na Xi Jinping kwenye treni ya mwendo kasi huku ikiwa kwenye motion alishangaa kuona hata vikombe vya chai na glass za maji mezani havianguki wala kutisika

Na walikalia viti vya kawaida tu sio vilivyotengenezewa kwenye treni na havikuwaangusha

Ndiyo uone train zs HSR za China jinsi zilivyo smooth ikiwa kwenye mwendo

 
Unauziwa kutokana na budget yako na mategemeo yako, hata ukitaka guarantee mchina anakupatia
Hamna hiyo kitu wewe guarantee si karatasi tu, kwa kipindi nanunua nokia 95 slide ilikua hela ndefu.
Ndo kuja gundua duka la mchina simu ya hovyo tu, maana nilikua na toleo la zamani toka UK.
Narudisha kakataa kubadili risiti ipo guarantii ipo.
 
Back
Top Bottom